Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Wanamaji wa Jeshi la Sepah Waliowakamata Wanajeshi wa Marekani Chapa
24/01/2016
IRGCAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, mchana wa leo (Jumapili) ameonana kwa karibu na wanajeshi vijana wa Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ambao walisimama imara na kishujaa kukabiliana na kuwakamata wanajeshi wa Marekani walioingia kinyume cha sheria katika maji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Vile vile Ayatullah Udhma Khamenei katika hotuba yake fupi ameitaja hatua hiyo inayopasa kupongezwa ya Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni ya kishujaa iliyoandamana na imani isiyotetereka na kuongeza kuwa: Kazi yenu ni nzuri mno, ni ya kuvutia na mumeifanya kwa wakati unaofaa kabisa na kwa hakika inabidi kusema kuwa tukio hilo ni kazi ya Mwenyezi Mungu Ambaye aliwavuta Wamarekani hadi katika maji yetu ili iweze kuchukuliwa hatua mliyoichukua na kuwakamata wanajeshi wa Marekani wakiwa wameweka mikono vichwani kama tulivyoona.
Katika hadhara hiyo, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewasalisha pia hadhirina sala za Adhuhuri na Laasiri.
 
< Nyuma   Mbele >

^