Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Azuru Haram ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) Chapa
30/01/2016
 Ayatollah Khamenei visiting the Shrine of Imam KhomeiniAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumamosi) amezuru Haram ya Imam Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyoko kusini mwa Tehran; ikiwa ni katika maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu maarufu kwa jina la sherehe za Alfajiri Kumi ambapo tarehe ya leo inasadifiana na siku aliporejea nchini Iran Imam Khomeini (quddisa sirruh) kutokea Ufaransa. Ayatullah Udhma Khamenei amemsomea Faatiha mwasiishi huyo mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezuru makaburi ya mashahidi wa tarehe ‘Saba Tir' katika eneo la makaburi ya mashahidi huko Behesht Zahra (kusini mwa Tehran) na kuziombea dua za kheri roho za mashahidi hao akimuomba Allah awapandishe daraja za juu ya utukufu.
 
< Nyuma   Mbele >

^