Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kupewa Nishani ya Ushindi Makamanda wa Sepahkwa Kuwakamata wanajeshi wa Marekani Chapa
31/01/2016
IRGCAdmirali Ali Fadavi, Kamanda wa Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na makamanda wengine wanne wa jeshi hilo wamepata fakhari ya kupewa nishani ya ushindi na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na kuongoza operesheni ya kishujaa na ya haraka ya kukamata boti za Marekani na wanajeshi waliokuwemo ndani yake baada ya kuingia katika maji ya Iran kiyume cha sheria katika eneo la kisiwa cha Farsi cha Iran.
Aidha Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amekubaliana na suala la kupandishwa cheo makamanda na maafisa wengine wa jeshi hilo walioshiriki katika operesheni hiyo kama ilivyopendekezwa na komandi kuu ya vikosi vya ulinzi nchini.
 
< Nyuma   Mbele >

^