Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Miongozo ya Kiongozi MuadhamuAlipoonana na Maafisawa "Kongamano la Mashahidi Wanamichezo Nchini" Chapa
02/02/2016
A group of Professional athletes met with Ayatollah Khamenei Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoyatoa wakati alipoonana na waendeshaji wa "Kongamano la Mashahidi Wanamichezo Nchini Iran" mkutano ambao ulifanyika tarehe 11 Januari 2016, yamesambazwa leo asubuhi katika kongamano lenye maudhui hiyo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Michezo wa Azadi, jijini Tehran.
Katika mkutano huo, Ayatullah Udhma Khamenei alipongeza ubunifu wa kuvutia wa kuwaenzi mashahidi wanamichezo nchini Iran na kusisitiza kuwa: Ni jambo la lazima kuifanya jamii nchnii ielewe ni kiasi gani watu wa kila namna walivyojitolea muhanga maisha yao katika njia ya dini na Mapinduzi ya Kiislamu na kwamba watu hao hawakutoka katika tabaka fulani tu la watu, bali watu wa matabaka yote wameshiriki kwenye jambo hilo adhimu la kimaanawi.
Amelitaja suala la kuwaenzi mashahidi wanamichezo nchini kuwa ni kunazitia nguvu nyoyo na kuimarisha fikra ya kimapinduzi na kuongeza kuwa: Kijana mwanamichezo ni kigezo kwa sehemu kubwa ya vijana na kwamba maadili, mienendo na mtindo wake wa maisha unaweza kuwa na taathira kwa vijana na unaweza kuingoza jamii kuelekea kwenye kuthamini mambo ya kidini, kimaadili na kimaanawi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja neno la lugha ya Kifarsi la "Pahlevan" kuwa ni lakabu yenye ubora wa namna yake katika fasihi ya jadi na ya kitaifa kwa Iran na huku akiwaenzi wanamichezo ambao wanafanya vitendo vizuri katika maeneo yao ya michezo amesisitiza kuwa: Fakhari kubwa zaidi inayopindukia fakhari ya kusomwa wimbo wa taifa au kupandishwa juu bendera ya nchi baada ya kupatikana ubingwa katika medani fulani ya michezo, ni kitendo cha mwanamichezo ambaye anakataa kupigana mweleka na mpinzani Mzayuni au yule mwanamichezo wa kike ambaye anasimama juu ya jukwaa la ubingwa akiwa amevaa "chadoro" au hijabu kamili ya Kiislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei ameyataja mambo hayo kuwa ni mithili ya kwenda kwenye medani ya vita na kuonesha moyo mkubwa wa kimapambano wa Muirani Muislamu katika medani tofauti. Ameongeza kuwa: Vitendo hivyo vinaonesha utambulisho wa taifa na ni jambo linaloimarisha dhati yao na hiyo ni silaha madhubuti kwao iliyo imara mithili ya chuma cha pua ambayo inawasaidia kusimama kidete na kutozubaishwa wala kushindwa na wimbi la mawazo chapwa na hisia danganyifu, na kwa kweli inabidi kuzifanya medani zote za michezo zielekee upande huo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ni jambo zuri sana kuwaenzi wanamichezo ambao wanalinda waziwazi matukufu ya kidini katika medani ya michezo. Ameongeza kuwa: Moja ya kazi ambazo inabidi zifanywe ni kuwaenzi wanamichezo ambao wanaanza michezo yao kwa kutaja jina la Mwenyezi Mungu na wale wanamichezo ambao wanapomaliza pambano wanaporomoka chini kusujudu kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Amesema, jambo hilo ni nembo ya utambulisho na ndiyo shakhsia ya Iran ya Kiislamu na kusisitizia udharura wa kutiwa nguvu suala hilo na kuelezea matumaini yake kuwa, kadiri siku zitakavyosonga mbele, ndivyo maeneo na medani za michezo zitakavyokuwa safi zaidi na zenye uwazi zaidi.
 
< Nyuma   Mbele >

^