Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Ghana Chapa
14/02/2016
The President of Ghana meeting with Ayatollah Khamenei Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni ameonana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana na huku akiashiria nukta chanya na zinazoungwa mkono na Iran za kustawisha uhusiano wake na nchi za Afrika tangu mwanzoni kabisa mwa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo hii amesema kuwa, madola ya kibeberu duniani yanapinga kuweko uhusiano mzuri baina ya Iran na nchi za bara la Afrika na madola hayo ndiyo chanzo kikuu cha vita, mapigano na kuzuka makundi ya kigaidi na kwamba suluhisho la matatizo yote hayo ni nchi zilizo huru duniani kuzidi kuwa na uhusiano wa karibu na kuongeza ushirikiano baina yao.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa, manufaa ya madola ya kiistikbari yanapatikana kwa kuanzisha fujo na vita vya kila aina katika maeneo tofauti duniani na kusisitiza kuwa: Makundi ya kigaidi katika eneo letu hili na barani Afrika yameanzishwa na kulelewa na mashirika ya kijasusi ya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni (wa Israel).
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia matamshi ya Rais wa Ghana kuhusiana mateso wanayoyapata wananchi wa Syria kutokana na ugaidi kwa kuuliza swali kwamba inakuwa vipi magaidi wanakabidhiwa marundo kwa marundo ya silaha za kisasa na pesa nyingi na kuongeza kuwa: Chanzo cha matatizo yote hayo ni madola ya kibeberu yanayoongozwa na Marekani huku utawala wa Kizayuni (wa Israel) ukiwa ndilo dhihirisho la wazi la ushetani.
Amesema msimamo na siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ambazo ziko wazi kabisa kuhusiana na Syria ni kuunga mkono juhudi za amani na kuongeza kuwa: Sisi daima tumefanya juhudi za kuhakikisha kuwa kadhia hiyo inamalazika kwa manufaa ya taifa la Syria na tunaamini kuwa, "cheti" cha kutibu matatizo ya taifa hilo hakiwezi kutoka nje ya nchi hiyo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Wamarekani na wazungu wa Ulaya hawana haki ya kuwapangia na kuwaainisha wananchi wa Syria nini cha kufanya, bali ni taifa pekee la Syria ndilo linalopaswa kuchukua maamuzi kuhusu mustakbali wake.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, njia ya kuweza kutatua suala la Syria na kukabiliana na matatizo kama vile ugaidi na mateso waliyo nayo wananchi wa Palestina inaweza kupatikana kupitia kustawishwa ushirikiano wa karibu na mkubwa zaidi baina ya nchi huru duniani na kuongeza kuwa: Iran na Ghana zina mambo mengi ya kuweza kushirikiana na ni matumaini yetu kuwa ziara hii itafungua milango ya kuweko ushirikiano mkubwa zaidi baina ya nchi mbili.
Vile vile amewaenzi mashujaa na wanamapambano waliopigania uhuru barani Afrika waliosimama imara kupambana na wakoloni na waistikbari na kusema kuwa: Shakhsia hao wakubwa ndio walionyanyua juu utambulisho wa bara la Afrika duniani.
Katika mazungumzo hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais John Dramani Mahama wa Ghana amegusia namna Iran ilivyo na ustaarabu tajiri na mkongwe na jinsi ilivyo mstari wa mbele katika masuala ya kielimu na kusema kuwa, matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu yanatoa msukumo mkubwa wa kujenga dunia iliyojaa amani na amma kuhusiana na kadhia ya Palestina amesema: Mateso ya taifa la Palestina yanayatia wasiwasi mataifa yote duniani na inabidi mataifa ya dunia yashirikiane na yafanye kazi kwa pamoja katika kutetea na kulinda haki za taifa la Palestina.
Ameashiria pia vitendo vya makundi ya kigaidi barani Afrika na katika eneo la magharibi mwa Asia na huku akiipongeza Iran kwa kupambana vilivyo na ugaidi amesema kuhusu kadhia tata sana ya Syria kwamba: Siasa zinazohusiana na mambo ya nje za Iran zimesimama katika mstari sahihi wa kuheshimu haki ya mataifa yote duniani kujiamulia yenyewe mustakbali wao na ni matumai yetu kuwa kadhia ya Syria itapatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kutumia mchango mzuri wa Iran katika kupambana na ugaidi.
Vile vile Rais John Dramani Mahama wa Ghana ameishukuru Iran kwa misaada yake kwa wananchi wa nchi yake na kuongeza kuwa: Natumia fursa hii kuyawakilisha mataifa yote ya Afrika, kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu kutokana na mchango wake wa kuunga mkono harakati mbali mbali za ukombozi barani Afrika hususan harakati ya ukombozi ya kupambana na ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Aidha rais huyo wa Ghana amegusia mazungumzo yake aliyofanya katika ziara yake ya mjini Tehran na kutiwa saini hati kadhaa za maelewano akiongeza kuwa: Tuko tayari kuongeza ushirikiano baina yetu na Iran katika nyuga na sekta tofauti.
 
< Nyuma   Mbele >

^