Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Wananchi wa Azerbaijan Mashariki Chapa
17/02/2016
People of East Azerbaijan met with the Leader of the RevolutionAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumatano) ameonana na matabaka mbali mbali ya maelfu ya wananchi wenye shauku na hamasa kubwa wa mkoa wa Azerbaijan Mashariki na huku akilishukuru kwa udhati wa moyo wake taifa kubwa la Iran kwa kuunda hamasa kubwa ya Bahman 22 mwaka huu (Februari 11, siku zinapofikia kileleni sherehe za maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran) na kusema kuwa, hamasa hiyo inathibitisha kuweko mwamko, azma na nia ya kweli na kutotetereka wananchi wa Iran. Aidha amesisitiza kuwa, uchaguzi wa tarehe 26 mwezi huu wa Februari nao ni dhihirisho la mwamko wa taifa la Iran na kulinda mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na uhuru na heshima ya taifa na kuongeza kuwa: Kwa kujitokeza kwa wingi na kwa mwamko, welewa na muono wa mbali wananchi katika uchaguzi huo, kutakuwa ni kinyume kikamilifu na malengo ya adui.
Katika mkutano huo uliofanyika wakati huu wa kukaribia maadhimisho ya harakati ya wananchi wa Tabriz ya tarehe 29 Bahman 1356 (Februari 18, 1978) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewashukuru wananchi wa Azerbaijan kwa imani yao thabiti, mwamko, nishati na kusimama kwao kidete katika nyakati tofauti muhimu sana za historia ya Iran hususan katika kipindi cha Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitizia wajibu wa kubakishwa hai kumbukumzu za siku za kihistoria za Mapinduzi ya Kiislamu. Aidha ameashiria kuwa, Bahman 22 (Februari 11) ni miongoni mwa siku hizo muhimu mno na kuongeza kuwa: Kwa mujibu wa ripoti zenye ushahidi thabiti za vituo vyenye itibari duniani, kiwango cha ushiriki wa wananchi katika maadhimisho ya Bahman 22 mwaka huu kote nchini Iran kimeongezeka sana ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma.
Ayatullah Udhma Khamenei amewashukuru kwa udhati wa moyo wananchi kwa kushiriki kwa wingi mkubwa katika maandamano ya kuadhimisha Bahman 22 na kusisitiza kuwa: Ongezeko hilo la kiwango cha watu walioshiriki kwenye maandamano hayo limeshuhudiwa licha ya kufanyika njama nyingi za mabeberu za kujaribu kuyasahaulisha maadhimisho hayo au kuyafifiliza katika akili na nyoyo za wananchi. Amesema, licha ya kuwepo njama zote hizo, lakini zimeshindwa kutia doa hata dogo katika nia ya kweli na isiyotetereka ya wananchi wa Iran.
Baada ya hapo amezungumzia uchaguzi wa Februari 26 na kusisitiza kuwa: Adui ameandaa ratiba maalumu ya kufanikishia njama zake kupitia uchaguzi, hivyo taifa la Iran ambalo ndilo mmiliki halisi wa nchi hii linapaswa kujua baadhi ya mambo ili kutoruhusu zitimie nia mbaya za adui.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbushia uhakika kwamba, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kukatwa mikono ya Marekani na utawala wa Kizayuni nchini Iran ilikuwa ni aibu kubwa sana kwao na ndio maana katika kipindi chote hiki cha miaka 37 ya tangu kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu, maadui hao hawajaacha hata mara moja kufanya njama zao dhidi ya harakati yenye kasi ya taifa la Iran na kuongeza kuwa: Tangu mwanzoni kabisa mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, njama za mabeberu zimelenga kwenye kuzuia kufanyika kabisa chaguzi nchini Iran na wamechukua hatua mbali mbali za kujaribu kufanikisha njama zao hizo, lakini kwa vile wamekata tamaa kikamilifu kuhusu kuzuia kufanyika uchaguzi nchini, katika miaka ya hivi karibuni wameanzisha njama za kuzusha shaka na wasiwasi kuhusu uwazi na uhalali wa changuzi hizo ili kwa njia hiyo waweze kujipenyeza humu nchini.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Njama za maadui kuhusu uchaguzi wa Februari 26 tayari zimeanza kwa kujaribu kulipaka matope Baraza la Kulinda Katiba na kuyaweka chini ya alama ya kuuliza maamuzi ya baraza hilo, wakati baraza hilo ni moja ya nguzo kuu katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ambao unapingwa vikali mno na Wamarekani tangu awali kabisa ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Vile vile amesisitiza kuwa, matokeo ya kutilia shaka maamuzi ya Baraza la Kulinda Katiba ni kusingizia kuwa uchaguzi haukuwa wa haki na wa kisheria na kuongeza kuwa: Wakati unapoenea uongo huo wa kudai kuwa uchaguzi haukufanyika kwa haki na kisheria, inakuwa na maana kwamba hata Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) ambayo imetokana na uchaguzi huo, nayo haitakuwa na uhalali wa kisheria.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Lengo la njama hiyo ya kijanja ni kuitumbukiza Iran kwenye ombwe la sheria na pengo la kutokuwepo Bunge katika kipindi cha miaka minne ijayo, ndio maana tukasisitiza kwamba wananchi wanapaswa kuwa macho kabisa kuhusu suala hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia watu waliomo ndani ya Iran wanaojaribu kulipaka matope Baraza la Kulinda Katiba kwa kuzungumza maneno yale yale yanayozungumzwa na maadui na kuongeza kuwa: Wengi wa watu hao huwa hawajui hata wanachokisema, hivyo si sahihi kuwatuhumu kuwa ni wasaliti, lakini wenyewe watu hao wanapaswa kuelewa kuwa, kitendo chao cha kutoa sauti ile ile inayotolewa na adui ni kukamilisha njama hatari sana za adui.
Amesisitiza kuwa, moja ya malengo ya kambi ya kiistikbari ni kuutilia shaka na kuuweka chini ya alama ya kuuliza uchaguzi na kuyanyima mataifa ya Waislamu duniani faida za tukio la aina yake, la kibunifu na lenye mvuto wa kipekee la demokrasia ya kidini. Vile vile amezungumzia nafasi muhimu sana ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, wakati bunge linapopasisha sheria huwa linaweka reli ya kupita treni la serikali na la chombo cha utekelezaji wa sheria nchini hivyo kuchagua wabunge kwa kuwa na welewa mzuri na muono wa mbali ni muhimu mno na kuna taathira kubwa katika kuielekeza nchi kwenye harakati nzuri.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Kama bunge litashughulikia ustawi wa maisha ya wananchi, uadilifu wa kijamii, ustawi wa kiuchumi, maendeleo ya kielimu na kiteknolojia, uhuru na heshima ya taifa, basi kazi ya bunge itakuwa ni kuweka reli ya kuelekea kwenye ufanikishaji wa malengo hayo, lakini kama bunge litatekwa na siasa za Magharibi na Marekani, na kutojali wananchi na badala yake kujali mrengo fulani tu wa mamwinyi na watu wanaopenda anasa, basi uwekaji wa reli wa bunge hilo utaisukuma nchi kwenye njia mbaya na yenye madhara makubwa.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia maneno ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) ambaye alikuwa analihesabu bunge kuwa chombo kinachoongoza mambo yote na kusema: Maana ya kuongoza mambo yote si kwamba Bunge linaingilia kazi za serikali zilizoainishwa na katiba, bali ni umuhimu mkubwa wa Bunge katika kuainisha njia sahihi ya harakati ya nchi kuelekea kwenye ufanikishaji wa malengo yake matukufu.
Ameendelea na hotuba yake kwa kuzungumzia pia umuhimu wa kimsingi na wa kiusuli wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kusema: Umuhimu wa nafasi ya Baraza la Wanavyuoni Wataalamu umo katika kazi yake ya kumuainisha Kiongozi Muadhamu ambaye ni mchukuaji maamuzi mkuu na muwekaji mkuu wa sera za nchi hivyo kuchagua wajumbe wa baraza hilo, ni jambo muhimu mno.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kama wajumbe wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu watashikamana vilivyo na Mapinduzi ya Kiislamu, kuwatumikia wananchi, kuzielewa vyema njama za adui, kusimama imara kukabiliana na njama hizo katika wakati unaofaa, basi maamuzi yatakayochukuliwa na wajumbe hao yatakuwa kwa namna nzuri inayotakiwa, lakini kama wajumbe wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu hawatakuwa na sifa hizo, basi maamuzi na kazi zao zitakuwa kinyume kabisa na inavyotakiwa.
Ayatullah Udhma Khamenei ameasiria pia namna vyombo vya kipropaganda vya kambi ya kiistikbari vilivyojikita kwenye kuendesha propaganda mbaya dhidi ya baraza hilo na kuongeza kuwa, lengo lake la kusisitizia mara kwa mara umuhimu wa kuwa macho na kuwa na busuri na muono wa mbali na welewa wa kutosha wananchi katika uchaguzi, ni suala hilo kwamba, wasije wakatoa mwanya wa kufanikishwa malengo na matakwa ya adui.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mara nyingine tena amelitaka taifa la Iran kujitokeza kwa wingi mno kwenye uchaguzi na kuulinda mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na uhuru na heshima yao ya kitaifa na kusisitizia ulazima wa kuwa macho sana mbele ya kambi hatari sana inayokabiliana na taifa la Iran inayofanya mambo yake bila ya kujali wala huruma na ambayo iko chini ya ushawishi na ubeberu wa kanali za Kizayuni.
Ameongeza kuwa: Siasa za Marekani na za serikali nyingi za nchi za Ulaya ziko chini ya ubeberu wa kanali hiyo na kwamba hata hatua zilizochukuliwa na Wamarekani katika kadhia ya nyuklia ya Iran nazo inabidi zitathminiwe katika fremu hiyo hiyo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Baada ya kupita kipindi kirefu cha mazungumzo na hatimaye kufikiwa makubaliano ya nyuklia, kwa mara nyingine kiongozi mmoja wa Marekani hivi karibuni amesema kuwa, watahakikisha kuwa hakuna wawekezaji wowote wa kimataifa watakaothubutu kuwekeza nchini Iran!
Amesisitiza kuwa, matamshi ya namna hiyo yanaonesha ukubwa wa kupindukia mipaka wa uadui wa Marekani dhidi ya taifa la Iran. Ameongeza kuwa: Moja ya malengo ya watu ambao miaka miwili iliyopita walikuwa wamo katika timu ya Iran ya mazungumzo ya nyuklia na ambao kwa hakika wamefanya kazi kubwa, ni kufungua njia za uwekezaji wa kiuchumi nchini Iran, lakini Wamarekani leo hii wanataka hata suala hilo nalo lisifanyike.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Hii ndio maana ya kusema muda mwingi kuwa, Wamarekani si watu wa kuwaamini hata kidogo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia malalamiko yanayotolewa na wanasiasa wa Marekani dhidi ya nara na kaulimbiu ya "Mauti kwa Marekani" inayopigwa na wananchi wa Iran kwenye maandamano mbali mbali na kusema kuwa, wakati nyinyi Wamarekani matendo yenu ni kama haya na vitendo vyenu vyote vya huko nyuma na vya hivi sasa vinaonesha uadui wenu mkubwa dhidi ya taifa hili, mnataraji mtapata majibu gani ghairi ya haya kutoka kwa wananchi wa Iran?
Ameongezaa kuwa: Tab'an wakati unapoonana nao katika vikao vya pande mbili utaona wanakuchekea, wanakupa mikono na utasikia maneno mazuri kutoka kwao, lakini yote hayo ni mambo ya kawaida kwenye mikutano ya kidiplomasia na ya pande mbili, na hayana taathira yoyote katika uhalisia wa mambo.
Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Uhakika wa mambo ni kwamba, baada ya kufanyika mazungumzo ya muda mrefu na kufungwa mikataba na kumalizwa mambo yote, hivi sasa tena Wamarekani wanasema, haturuhusu wawekezaji wawekeze nchini Iran na wanatoa vitisho vipya vya waziwazi dhidi ya taifa hili.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Huu ndio uhakika wa Marekani, na haiwezekani kufumbia macho wajibu wa kukabiliana vilivyo na na adui huyo.
Aidha amewaambia wananchi kwamba: Taifa azizi la Iran, huo ndio uhakika na uhalisia wa upande unaokabiliana nanyi, hivyo mnapaswa kuwa macho na kuchukua tahadhari kubwa mbele ya adui huyo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa: Utatuzi wa matatizo yaliyopo nchini utatokana na kuwa macho wananchi, kulinda misukumo ya kiimani na kiitikadi katika jamii, kuwatumia vizuri vijana wenye moyo na waumini na kujiimarisha ndani ya nchi kiimani, kiuchumi, kielimu na katika taasisi za uongozi na usimamiaji wa mambo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia pia ulazima wa kulinda umoja na mshikamano na kuwa na sauti moja wananchi katika kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu na misingi na malengo yake matukufu na kusema kuwa: Viongozi wenye mapenzi ya mustakbali mzuri wa nchi, nao wanapaswa kufanya juhudi za kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kupitia kuwatumikia vizuri wananchi na kuziamini nguvu kazi na uwezo wa ndani ya nchi.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa, uchumi wa kimuqawama na wa kusimama kidete, hauna maana ya kujenga ukuta wa kuizunguka nchi. Ameongeza kuwa, uchumi wa kimuqawama ni uchumi wa kujiimarisha ndani kwa ndani na kuruhusu vitu vya nje kuchangia uimarishaji wa kiuchumi, yaani ni uchumi unaotegemea taifa kwani kama uchumi hautokuwa na msingi wake mkuu ndani ya nchi, hauwezi kufika popote.
Amesema, kuwa na miamala ya kiuchumi ya nchi nyingine duniani ni jambo zuri na kusisitiza kuwa: Tab'an miamala hiyo inabidi ifanyike kiutaalamu na ipelekee kupata nguvu misingi ya ndani ya nchi ya kiuchumi na hilo haliwezekani kama wananchi hawatokuwa imara na kama viongozi nchini hawatafanya mambo yao kwa welewa mpana.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mwishoni mwa hotuba yake kwamba: Kwa uwezo na taufiki ya Mwenyezi Mungu, vijana wa Iran kuna siku wataona kwa macho yao namna Marekani na hata atakayekuwa na nguvu kubwa kuliko Marekani wasivyoweza kufanya ‘ghalati' na upuuzi wowote mbele ya taifa la Iran.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Mojtahid Shabestari, mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) mkoani Azerbaijan Mashariki ambaye pia ni Imam wa Ijumaa wa Tabriz amezungumzia ghera na imani thabiti ya kidini ya wananchi wa Azerbaijan katika vipindi mbali mbali muhimu na nyeti na kusema kuwa, harakati ya Februari 18, 1978 ya wananchi wa Tabriz ilikuwa ni nukta muhimu mno katika historia ya Mapinduzi adhimu ya Kiislamu na inaonesha mwamko, busuri na muono wa mbali walio nao wananchi wa Azerbaijan ambao ni watiifu kwa Wilaya.
Imam wa Sala ya Ijumaa wa Tabriz amelitaja suala la wananchi kujitokeza kwa wingi sana katika uchaguzi kuwa ni dhihirisho la nguvu za kimaanawi za Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Wananchi walio macho wa Azerbaijan, pamoja na wananchi wa maeneo mengine yote ya Iran, tarehe 26 Februari watajitokeza kwa wingi na kwa mwamko mkubwa kwenye vituo vya kupigia kura ili kwa mara nyingine tena waweze kujenga hamasa ya kubakia milele katika historia ya taifa lao.
 
< Nyuma   Mbele >

^