Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Azerbaijan Chapa
23/02/2016
AzerbaijanAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni (Jumanne) ameonana na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan na huku akigusia uhusiano mzuri wa kisiasa na mambo yanayoziunganisha pamoja nchi mbili za Iran na Azerbaijan hususan masuala ya pamoja ya kidini na kimadhehebu ya mataifa haya mawili amesema kuwa: Kueneza mafundisho ya Kiislamu na kuheshimiwa nembo na shaari za kidini ni mambo ambayo yanawavutia wengi na kuleta uungaji mkono wa wananchi katika kukabiliana na vitisho mbali mbali.
Katika mazungumzo hayo, Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawaangalia watu wa Azerbaijan kwa jicho la ndugu zake yaani zaidi ya rafiki na jirani zake na kuongeza kuwa: Utulivu wa kisiasa na kiusalama pamoja na uhenezi na ustawi wa jamii yote ya wananchi wa Azerbaijan ni muhimu mno kwetu na licha ya kuwepo maelewano ya huko nyuma baina ya mataifa ya nchi hizi mbili, inabidi mabadilishano ya kibiashara na ushirikiano katika sekta tofauti uimarishwe zaidi baina ya pande hizi mbili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia mambo mengi ya pamoja ya kimadhehebu baina ya wananchi wa Iran na Azerbaijan na kusisitiza kuwa: Itikadi za Kiislamu na Kishia za wananchi wa Azerbaijan ni rasilimali yenye thamani kubwa, na kadiri serikali ya nchi hiyo inavyoheshimu nembo na itikadi hizo za kidini za wananchi na kuzipokea vizuri zaidi na zaidi, ndivyo itakavyoweza kupata uungaji mkubwa zaidi wa wananchi na kuwafanya wananchi hao wasimame kidete kukabiliana vilivyo na uadui wa baadhi ya madola ya kibeberu.
Amesema, suala la kukabiliana na fitna ya makundi ya kitakfiri yanayoeneza chuki kati ya mataifa tofauti duniani litawezekana kwa kuimarisha harakati za Kiislamu na kuongeza kuwa: Katika upande wa kidini, eneo la Azerbaijan lina historia ndefu na ni chimbuko la baadhi ya maulamaa wakubwa wa Kiislamu na kwa upande wa watu pia, jamii ya Azerbaijan ni ya watu wenye welewa na wenye mwamko na kwamba iwapo serikali itatilia hima suala la kusaidia harakati za kidini; suala hilo litakuwa na faida kubwa kwake katika kupata mapenzi na uungaji mkono wa watu hao.
Ayatullah Udhma Khamenei ameunga mkono pia matamshi ya Rais wa Azerbaijan kuhusu uhakika kwamba chanzo cha vitisho vingi dhidi ya nchi hizi mbili ni kimoja na kuongeza kuwa: Kueneza mafundisho ya Kiislamu na ya Kishia kutapelekea kupata nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu na msaada wa Maimamu watoharifu (Alayhimus Salaam) katika kukabiliana na matatizo na vitisho mbali mbali.
Katika mazungumzo hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan amezungumzia uhusiano wa karibu uliopo baina ya Tehran na Baku na kusema kuwa, mazungumzo aliyofanya katika ziara yake ya nchini Iran ni mazuri na yenye mafanikio. Ameongeza kuwa: Utamaduni, dini na historia ya pamoja ni kiunganishi madhubuti sana baina ya Iran na Azerbaijan.
Amegusia pia kutiwa saini zaidi ya hati 10 za ushirikiano baina ya Tehran an Baku na kusema kuwa, uhusiano wa pande hizi mbili ni wa kidugu na uko katika hali nzuri sana.
Ameongeza kuwa: Hivi sasa kumeshapigwa hatua nzuri katika upande wa ushirikiano wa kibiashara, uchukuzi, nishati na viwanda, na kuongeza kuwa: Sasa hivi tunafanya juhudi za kuhakikisha kunakuwa na umoja na uhusiano madhubuti zaidi baina ya pande mbili katika nyuga zote.
Rais wa Azerbaijan aidha amesema kuwa, Tehran na Baku zina misimamo mimoja katika masuala ya kimataifa na kuongeza kuwa, Iran ina nafasi muhimu sana katika kuleta usalama na utulivu duniani na sisi tunauhesabu usalama wa Iran kuwa ni sawa nsa usalama wetu.
Bw. Ilham Aliyev amesema kuwa, vitisho vinavyozikabili nchi hizi mbili ni vya aina moja na vinatoka katika chanzo kimoja na kuongeza kuwa: Katika ziara yake hii ya nchini Iran wameafikiana kuongeza ushirikiano wao na Iran katika kupambana na ugaidi hadi usalama na amani itakapoenea kwenye eneo hili zima.
Vile vile amesisitizia umuhimu wa kuheshimiwa matukufu ya Kiislamu na kuzungumzia kazi zinazofanywa na serikali yake katika kuimarisha mafundisho ya dini ya Kiislamu nchini humo na kuongeza kuwa, katika kipindi cha tangu kupata uhuru Azerbaijan kumeshajengwa misikiti elfu mibli nchini humo ambapo nusu nzima ya misikiti hiyo imejengwa katika kipindi cha utawala wake.
Rais wa Azerbaijan amelaani harakati zilizo dhidi ya Uislamu na sababu za uadui wa maadui wa taifa hilo wanaopenda kuharibu itikadi za kidini za wananchi wa nchi hiyo na amemwambia Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba: Uislamu na Ushia nchini Azerbaijan unapendwa sana na wananchi na kwamba kuwepo shakhsia na watu muhimu kama wewe kwenye eneo hili kunazidi kutupa nguvu na nishati kubwa zaidi.
 
< Nyuma   Mbele >

^