Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Ashiriki katika Uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na... Chapa
26/02/2016
Elections 2016Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo Ijumaa ameshiriki katika dakika za awali kabisa za kuanza zoezi la kupiga kura za Majlisi ya 10 ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na Baraza la Tano la Wanavyuoni Wataalamu (linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu). Ayatullah Udhma Khamenei amepiga kura yake katika kituo jongefu nambari 110 katika Husainia ya Imam Khomeini (quddisa sirruh), mjini Tehran.
Baada ya kupiga kura, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumza machache akisema, uchaguzi ni jukumu na vile vile ni haki ya taifa na kuongeza kuwa: Uchaguzi ni jambo kubwa, ni jambo la kheri ambalo daima ni muhimu na katika baadhi ya nyakati umuhimu wake unakuwa mkubwa zaidi na ni suala ambalo limeusiwa pia katika mafundisho ya Uislamu kwa ajili ya kutia kasi utekelezaji wa mambo ya kheri.
Aidha amesisitizia wajibu wa kuongeza kasi katika kutekeleza majukumu na kusimamisha haki na kuongeza kuwa: Kama tulivyosema huko nyuma, wananchi wote wa Iran; kila mtu ambaye anaipenda Iran na Jamhuri ya Kiislamu na aliye na hamu ya kuona kunapatikana ustawi, heshima na utukufu wa taifa, hana budi kushiriki katika uchaguzi.
Vile vile amewataka wananchi washiriki katika uchaguzi kwa nia ya kheri na kwa lengo la kuongeza itibari zaidi kwa nchi na kwa uhuru kamili wa nchi yao pamoja na kujibu mahitaji ya kuwa na heshima ya taifa na kusisitiza kuwa: Matokeo ya kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi ni kupatikana heshima na uhuru wa kitaifa hasa kwa kuzingatia kuwa sisi tuna maadui ambao daima wanakodolea macho ya tamaa chaguzi zinazofanyika humu nchini; hivyo kushiriki kwetu kwenye uchaguzi kunapaswa kuwe kwa namna ambayo itamvunja moyo na kumkatisha tamaa adui.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa: Wananchi wanapaswa kuwa makini, wawe na busuri na muono wa mbali na wapige kura zao kwa macho yaliyo wazi kwani kufaya hivyo ni katika kazi za kheri na njema ambazo mbali na kupata matunda mazuri ya muda mfupi na ya muda mrefu hapa duniani, kutawafanya wananchi wapate ujira bora pia Siku ya Kiyama.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameelezea matumaini yake kuwa taifa la Iran mara hii pia - kwa kushiriki kwao kwa wingi na inavyotakiwa katika uchaguzi, kama walivyofanya kwenye chaguzi zilizopita - watapelekea nchi yao izidi kupata maendeleo na heshima.
 
< Nyuma   Mbele >

^