Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Uswisi Chapa
27/02/2016
http://turkish.khamenei.ir//images/stories/20160227.jpgAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo jioni (Jumamosi) ameonana na Rais Johann Schneider-Ammann wa Uswisi na huku akiashiria historia ndefu ya uhusiano wa nchi mbili na mwangwi chanya wa hatua na siasa za serikali ya Uswisi katika fikra za walio wengi nchini Iran amekaribisha juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kielimu baina ya pande mbili na kusema kuwa, kiwango cha mabadilisho ya kiuchumi baina ya Iran na Uswisi ni kidogo na hakiko katika daraja inayotakiwa. Ameongeza kuwa, iwapo wafanyabiashara na wawekezaji wa Uswisi watajua vizuri nafasi na uwezo mkubwa wa Iran katika nyuga mbali mbali, basi bila ya shaka yoyote wataweza kunyanyua vizuri kiwango hicho cha mabadilishano ya kibiashara.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kutokuwepo historia hasi ya kushiriki Uswisi kwenye mashinikizo na vikwazo vya baadhi ya tawala wa Magharibi dhidi ya Iran kuwa ni moja na nyuga nzuri za kiutamaduni za kunyanyua kiwango cha ushirikiano baina ya pande mbili na kuongeza kuwa: Sisi tangu zamani tulikuwa tunaijua Uswisi kuwa ni kituo cha amani na urafiki na ushirikiano, tab'an baadhi ya nchi za Ulaya haziko hivyo na zinadhani maslahi yao yatapatikana kupitia kuzusha vita na mifarakano katika mataifa mengine.
Vile vile amegusia uzoefu wa wananchi wa Iran kuhusiasa na siasa za kupenda vita za baadhi ya nchi za Ulaya kama vile siasa za nchi hizo za Ulaya za kuupa makombora na ndege za kivita utawala wa Saddam wakati wa vita vya kujihami kutakatifu ambavyo Iran ililazimishwa kupigana na kuongezwa kuwa: Vitendo vya nchi hizo vimeweka kumbukumbu hasi ndani ya akili za wananchi wetu kuhusiana na nchi hizo za Ulaya, lakini mawazo kama hayo hayapo nchini Iran kuhusiana na Uswisi.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia juu ya uungaji mkono kamili wa kiuchumi na dhamana ya kisheria inayotolewa na serikali ya Jamhuri ya Kiiaslamu kwa maafikiano ya pande mbili na kuongeza kuwa: Lililo muhimu ni kuhakikisha hatua za kivitendo zinachukuliwa kupitia kudumisha ushirikiano wa kweli, unaopewa uzito wa hali ya juu na ambao utaambatana na nia na azma isiyoyumba.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Johann Schneider-Ammann wa Uswisi ameelezea kufurahishwa kwake na kupata fursa ya kutembelea Iran na huku akigusia uhusiano wa muda mrefu wa kirafiki baina ya nchi mbili amesema kuwa: Ni fakhari kubwa kwetu kuona kuwa tuko Iran hivi sasa na tunashuhudia namna uhusiano wa nchi zetu mbili unavyozidi kuimarika.
Rais Johann Schneider-Ammann wa Uswisi ambaye ametembelea Iran akiongoza ujumbe wa aina mbili wa kielimu na kiuchumi wa nchi yake ameongeza kuwa: Katika ziara yetu hii tumepata fursa ya kujadiliana muongozo na ramani ya ushirikiano mpana na wa kila namna baina ya Iran na Uswisi na kwamba kwa kutiwa saini ramani hiyo ya njia kutawezesha kupanuliwa na kustawishwa zaidi na zaidi uhusiano wa pande hizi mbili.
Rais wa Uswisi ameashiria pia kuwepo changamoto nyingi kubwa duniani na kuongeza kuwa: Madhara ya ukosefu huo wa utulivu na changamoto nyingi zilizopo leo hii duniani zimeenea kote hadi barani Ulaya na katika maeneo ya karibu na Uswisi na kwamba tunahitajia kuwa na ushirikiano wa kweli kwa ajili ya kukabiliana vilivyo na changamoto zote hizo.
 
< Nyuma   Mbele >

^