Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Risala ya Tanzia Kufuatia Kufariki Dunia Marhum Farajollah Salahshoor Chapa
27/02/2016
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, ametoa ujumbe wa tanzia kufuatia kufariki dunia mtengeneza filamu mkubwa na mashuhuri na msanii aliyeshikamana vizuri na dini, marhum Bw. Farajollah Salahshoor. Matini ya jumbe huo wa Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Ninaitumia fursa hii kutoa mkono wa pole kwa familia, jamaa na wafiwa wote wa marhum Bw. Farajollah Salahshoor; msanii mkubwa aliyeshikamana vizuri na dini. Athari na kazi kubwa na zitakazobakia daima za msanii huyu aliyekuwa na imani thabiti na ambazo zimevuuka mipaka ya nchi yetu, ni heshima na fakhari kubwa kwa tasnia ya filamu ya Iran na ni kazi zenye itibari kubwa mbele ya macho ya mataifa mengine. Bila ya shaka yoyote kazi zake hizo zitampa jazaa njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kulibakisha hai jina lake na wema wake mbele ya watu, Inshaallah.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu ammiminie rehema Zake na maghufira na amnyanyue daraja za juu Kwake; mja huyu mwema, na azipe subira nyoyo za wafiwa wote.
Sayyid Ali Khamenei,
8 Isfand, 1394 (Hijria Shamsia)
(27 Februari, 2016 Milaadia).
 
< Nyuma   Mbele >

^