Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu Kufuatia Kushiriki kwa wingi Wananchi katika Uchaguzi Chapa
28/02/2016
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametoa ujumbe maalumu wa kulishukuru taifa lenye mwamko na lenye msimamo imara la Iran kwa kuitia labeka mwito wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kushiriki kwa wingi mno, kwa nia thabiti, kwa shauku, kwa nishati ya kupigiwa mfano katika uchaguzi wa hivi karibuni na kuwaonesha walimwengu kwa njia bora kabisa maana halisi ya demokrasia ya kidini. Amewaambia viongozi nchini kwamba wana jukumu la kuwashukuru kivitendo wananchi kwa kuwatumikia inavyopasa. Vile vile amesisititizia wajibu wa kufanya jitihada za pande zote za maendeleo ya kujizalisha kujiimarisha kutokea ndani ya nchi, likiwani ndilo lengo kuu la taifa na kuongeza kuwa: Bunge lijalo litakuwa na jukumu kubwa na ni matumaini yetu kuwa, kiwango cha kutekeleza vizuri majukumu mbele ya Allah na mbele ya watu kitashuhudiwa kikipanda kwa viongozi wote.
Matini kamili ya risala na ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo
:
 

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mjuzi wa kila kitu Ambaye amelipa ushindi taifa lililo macho na lenye misimamo isiyotetereka la Iran katika mtihani mwingine muhimu na mkubwa na kuwawezesha wananchi wa Iran kushiriki kwenye uchaguzi wa nchi nzima kwa mara ya 36 tangu yalipopata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu na wameshiriki kwenye uchaguzi huo kwa nia ya kweli, kwa shauku na uchangamfu wa hali ya juu na kujiuamulia mustakbali wa nchi yao wakati huu, na kuchaguwa wawakilishi wao kwa ajili ya mabaraza mawili yenye nguvu na umuhimu mkubwa na kwa mara nyingine kuwaonesha walimwengu demokrsia ya kweli ya kidini yenye sura inayong'ara na nguvu za kuaminika.
Iran ya Kiislamu inajivunia wananchi wake na inatembea kichwa juu kwa umadhubuti wa sheria ambazo zimeleta fursa hii muhimu kwa ajili ya kunyanyua heshima yake na kulitia nguvu upya taifa.
Ni wajibu wangu kushukuru kwa namna wananchi wetu wote walivyoitikia labeika mwito huu wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kumuomba Mwenyezi Mungu awalipe malipo bora kabisa na awaongoe wananchi hawa ambao waliunda Ijumaa iliyojaa kazi na iliyojaa hadhi na heshima.
Viongozi wote nchini, iwe ni wale waliochaguliwa katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na Baraza la Wanavyuoni Wataalamu au wale wenye vyeo na nafasi za utendaji katika mihimili mingine mikuu wa dola au viongozi wengine katika taasisi na asasi nyingine, napenda kuwakumbusha kuwa, wana jukumu la kutoa shukrani za kweli za kuwahudumia kwa ikhlasi wananchi na nchi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu; na ninawasisitizia wote kujipamba kwa sifa za maisha ya mepesi na chini, usafi wa kimaadili, kuwepo wakati wote katika eneo la kutekeleza majukumu, kustahabu na kufadhilisha manufaa ya taifa mbele ya manufaa binafsi na ya mirengo, kusimama imara kishujaa mbele ya uingiliaji wa mabeberu, kuonesha radiamali ya kimapinduzi mbele ya njama za wanaolitakia mabaya taifa na wasaliti, na kujipamba kwa sifa za kijihadi katika fikra na vitendo kwa muhtasari: Kufanya kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika njia ya kuwatumikia waja wa Mwenyezi Mungu, iwe ndiyo ratiba yao ya daima katika kipindi chote cha kutekeleza majukumu yao na wasilidharau suala hilo kwa thamani yoyote ile.
Kipindi hiki nyeti mno, kinawawajibisha watu wote na hususan nyinyi viongozi kuwa makini zaidi na kuwa na hisia kali zaidi pamoja na nia isiyoteterekea, katika kulilinda taifa. Maendeleo ya nchi yetu ndilo lengo kuu. Maendeleo ya juu juu yasiyo na uhuru wala heshima ya taifa, hayakubaliki. Maendeleo hayana maana ya kukubali kumeng'enywa ndani ya mmeng'enyo wa madola ya kibeberu duniani. Kulindwa heshima na utambulisho huu wa kitaifa hakutawezekana kama hakutapatikana maendeleo ya pande zote ya kujizalisha na kujiimarisha ndani kwa ndani. Bunge lijalo lina jukumu zito na kubwa la kufanikisha mikakati hiyo muhimu na ni matumaini yangu kwamba kiwango cha kubeba majukumu mbele ya Allah na mbele ya wananchi, kitaonekana kikipanda kwa watu wote.
Ni wajibu wangu kuwashukuru kwa dhati wahusika wote waliofanikisha uchaguzi huu uliofana sana, kuanzia maafisa watendaji na wasimamiaji, walinda usalama, shirika la habari la taifa na asasi nyingine zote pamoja na kila aliyechangia kufanikisha uchaguzi huo.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu akupeni nyote taufiki katika mambo yenu.
Sayyid Ali Khamenei
9/Mwezi Isfand/1394
(28/Februari/2016).

 
< Nyuma   Mbele >

^