Maswali Yaliyofutuliwa |
Mlinganisho wa Fatwa |
Sherhe ya Hadithi |
Kabla ya Mapinduzi |
Baada ya Mapinduzi |
Ayatullah Khamenei |
Imam Khomeini |
Risala ya Tanzia Kufuatia Kufariki Dunia Ayatullah Vaez Tabasi |
![]() |
04/03/2016 | |
Bismillahir Rahmanir Rahim Nimeipokea kwa masikitiko na majonzi makubwa habari ya kufariki dunia alimu mujahid na mfuasi wa kweli wa Mapinduzi ya Kiislamu, Janab Hujjatul Islam Walmuslimin Alhaj Sheikh Abbas Vaez Tabasi, (rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Sheikh Tabasi alikuwa ni kaka mwenye huruma kwangu na mwenye maelewano mazuri, na alikuwa mtu mwaminifu wa Imam (Khomeini – quddisa sirruh) na alikuwa mtumishi mwenye misimamo isiyotetereka na mchapakazi mzuri wa Mapinduzi ya Kiislamu. Tangu zilipotokeza cheche za awali kabisa za mapambano ya mwamko wa Kiislamu katika mji mtakatifu wa Mash’had, muda wote tulimuona mwanachuoni huyu akijitokeza mbele kwa ushujaa na kwa athari kubwa katika nyuga zilizojaa hatari na kujitolea kubeba mambo mazito na magumu na kwmba uwepo wake huo wa wazi na wa kweli tuliuona hadi katika siku za mwisho za mapambano hayo ya mwamko wa Kiislamu ya taifa la Iran. Baada ya kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia, imani ya Imam wetu mtukufu kwake ilimfanya apate fakhari ya kuwa mfawidhi na mtumishi mkuu wa Haram tukufu ya Imam Ridha AS, na amefanya mambo mengi makubwa na mazuri na kwa ikhlasi kubwa katika haram hiyo. Misimamo yake ya kimapinduzi na utiifu wake kwa malengo matukufu ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na jitihada zake kubwa katika njia hiyo ambazo sehemu yake kubwa alizifanya bila ya watu kujua, zenyewe ni ukurasa unaojitegemea katika kurasa za maisha ya mwanachuoni huyu mkubwa. Hivi sasa na baada ya kututoka mwanachuoni huyu, ninahisi nimepoteza kaka mwenye huruma, mwenzangu wa karibu katika kipindi kigumu cha misukosuko mingi cha kabla ya ushindi wa Mainduzi ya Kiislamu na mtumishi mwenzangu mwenye jitihada kubwa wakati wa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema amlipe malipo mema anayostahiki na maghufira na radhi Zake. Aidha ninatoa mkono wa pole kwa udhati wa moyo wangu kwa wafiwa hususan mkewe mwenye subira na fikra njema na wanawe wapendwa nikimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azijaze subira nyoyo zao. Sayyid Ali Khamenei 14 Mwezi Isfand, 1394 (4 Machi, 2016). |
< Nyuma | Mbele > |
---|