Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kuteuliwa Katibu na Wajumbe wa Baraza Kuu, na Mudiri wa Hawza ya Kielimu ya Khorasan Chapa
08/03/2016
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameteua katibu na wajumbe wa Baraza Kuu pamoja na mudiri wa Hawza (Chuo Kikuu cha kidini) ya Khorasan.
Matini kamili ya hukumu ya uteuzi huo uliofanywa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

 

Bismillahir Rahmanir Rahim

Hawza ya kielimu ya Mash'had tukufu ni moja ya vituo vikongwe kabisa na vyenye thamani kubwa vya kielimu katika ulimwengu wa Kishia na ni sehemu muhimu ya kulea watu wenye majina makubwa katika fani tofauti za kielimu za kiakili na za kunukulu kwa karne nyingi sasa. Kuwepo katika mji huo Haram tukufu ya Imam Ridha (ziwe juu yake maelfu kwa maelfu ya rehema za Mwenyezi Mungu) kumeufanya mji huo kuwa kivutio cha maulamaa wakubwa kutoka Hawza za maeneo mengine na jambo hilo limeongeza thamani ya mji huo katika vipindi tofauti.

Hivi sasa Hawza hiyo yenye historia kubwa na ya kipekee ya kielimu, kihistoria na kisiasa, imepanuka zaidi kiidadi na kiubora baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini na sasa hivi ina uwezo mkubwa wa kulea maulamaa na wahakiki wakubwa wa Kiislamu katika fani za kila namna.

Ili uwezo huo uweze kuchanua na kunawiri unahitajia uongozi mkuu wa kusimamia vizuri pande zote kwa njia bora kabisa hivyo ninatumia fursa hii kuwateua Maayatullah na Mahujjatul Islam Alhaj Sayyid Hassan Mortazavi, Alhaj Sheikh Raj Ali Reza Zadeh, Alhaj Sheikh Mahdi Morvarid, mwakilishi wangu katika mkoa huo, mfawidhi wa Haram tukufu ya Imam Ridha AS, Alhaj Sheikh Muhammad Baqir Farzane na Alhaj Sayyid Misbah Amoli kuwa wajumbe wa Baraza Kuu la Hawza (ya Khorasan) na janabi Farzane kuwa katibu wa baraza hilo na janabi Amoli kuwa mudiri wa Hawza hiyo.

Kinachotarajiwa ni kwamba muundo huu wa watu wanaofaa kabisa na wachapa kazi na ambao umekamilika kila upande utafanya kazi zake kwa mpangilio mzuri na utaweza kuandaa uwanja wa kuimarika zaidi na kujitokeza makumi ya fikra za maana katika kila fani na kila uwanja unaohitajiwa na jamii ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na fani za fikihi, kalam, tafsiri, hadithi na kuzaa mamia ya watafiti na waandishi na watoa khutba na makadhi na watu wengine wa kushika masula ya kielimu na kijamii ya Kiislamu. Ni wajibu kwangu kuitumia fursa hii pia kumshukuru marhum Hujjatul Islam Walmuslimin Bw. Tabasi kwa kazi zake za maana alizozifanya wakati akiwa mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha AS nikimuomba Mwenyezi Mungu ampe radhi Zake na ampandishe daraja za juu Kwake.

Wassalaamu Alaykum Warahmatullah
Sayyid Ali Khamenei
18 Mwezi Isfand, 1394
(8 Machi, 2016).

 
< Nyuma   Mbele >

^