Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Vietnam Chapa
15/03/2016
VietnamAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni (Jumanne) ameonana na Rais Trương Tấn Sang wa Vietnam na huku akiashiria nyuga za kila namna za kiuchumi, kiutaalamu, kibiashara na kiutamaduni zinazopasa kufanyiwa kazi katika kuimarisha uhusiano wa nchi mbili za Iran na Vietnam amesema kuwa: Ushujaa na muqawama wa taifa la Vietnam na kuwa nchi hiyo na shakhsia wakubwa kama vile Ho Chi Minh na Jenerali Võ Nguyên Giáp katika kupambana na uistikbari wa mabeberu, umepelekea taifa la Vietnam kuheshimiwa na kupata itibari mbele ya taifa la Iran na kwamba heshima na mapenzi hayo ya taifa la Iran kwa taifa la Vietnam ni fursa nzuri sana ya kuweza kustawisha ushirikiano wa pande mbili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia njama za madola ya kibeberu duniani za kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kusema kuwa: Baadhi ya wakati uingiliaji huo wa madola ya kiistikbari hufanyika kupitia kuzusha vita vya kila namna kama vile vita vya Vietnam na wakati mwingine hufanyika kwa mbinu nyingine. Amesema: Njia ya kukabiliana na uingiliaji wa madola hayo ya kibeberu, ni nchi huru duniani kuzidi kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja.
Amesema siasa zisizotetereka za Jamhuri ya Kiislamu wa Iran ni kushirikiana na nchi za Asia ikiwemo Vietnam na kuongeza kuwa: Sisi tunatambua pia ushirikiano wenu katika taasisi za kimataifa na tunaamini kuwa inabidi ushirikiano baina yetu uimarishwe kwa kadiri inavyowezekana.
Katika mazungumzo hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Trương Tấn Sang wa Vietnam amemshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa matamshi yake ya kuenzi na kusifu mapambano ya wananchi wa Vietnam na viongozi wao waliosimama kidete kupambana na mabeberu na kusema: Wananchi wa Vietnam walisimama imara kupambana na mashambulizi kutoka nje kwa makumi ya miaka hadi walipoweza kujikomboa na kupata uhuru wao.
Bw. Trương Tấn Sang ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake kwa Vietnam katika taasisi za kimataifa na kusema kuwa: Vietnam nayo kwa upande wake inaunga mkono misimamo ya Iran katika taasisi za kimataifa na inaamini kuwa kutumia teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani ni haki isiyopingika ya Iran na katika siku za usoni pia itaendelea kuunga mkono misimamo ya Iran.
Rais wa Vietnam amesisitizia pia udharura wa kuongezwa ushirikiano wa pande mbili katika nyanja zote na kusema kuwa: Ni matumaini yetu Iran kwa kuzingatia siasa zake za kuzingatia nchi za mashariki mwa dunia, itaendelea kuihesabu Vietnam kuwa mshirika wake mkuu kama huko nyuma.
 
< Nyuma   Mbele >

^