Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Makamanda wa Ngazi za Juu wa Vikosi vya Ulinzi Chapa
10/04/2016
Leader meets with high ranking generals of Army and IRGCAmirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo (Jumapili) ameonana na makamanda waandamizi wa vikosi vya ulinzi vya Iran na kusema kuwa kielelezo cha "utambulisho wa pamoja" wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa, kwa wakati mmoja vina uwezo wa kufanya opereseheni za kijeshi na wakati huo huo vina misukumo na misimamo ya kimaanawi na kidini.
Ayatullah Udhma Khamenei aidha amesema: Katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, jukumu kuu la vikosi vya ulinzi ni kulinda mipaka na usalama wa taifa, hivyo kuna wajibu wa kuongezwa nguvu na uwezo wa kufanya operesheni za kijeshi na misukumo ya kimaanawi ya vikosi hivyo kadiri inavyowezekana.
Amesema "utambulisho wa pamoja" wa vikosi vya ulinzi vya Iran ni kuwa, kwa wakati mmoja vikosi hivyo vina "uwezo wa operesheni za kijeshi" na wakati huo huo vina "misukumo na misimamo ya kimaanawi na kidini."
Amesisitiza kuwa, kuna wajibu sifa hiyo ya kipekee ya vikosi vya ulinzi vya Iran itiwe nguvu na ilindwe wakati wote na kuongeza kuwa: Vikosi vya ulinzi vya Iran si mali ya mtu binafsi au chama na mrengo fulani, bali ni mali ya taifa na nchi nzima na vinapaswa kuwa ngao ya ulinzi na usalama pamoja walinzi wa taifa na wananchi wote.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia kuweko vikosi vya aina mbili vya ulinzi vyenye utambulisho maalumu katika nchi nyingi duniani na kuongeza kuwa: Katika baadhi ya nchi duniani, kuna jeshi na polisi wa kimaonesho, kimapambo na kidhahiri tu bila ya kuwa na uwezo wa kufanya operesheni za kijeshi bali kazi kubwa ya vikosi hivyo ni kulinda serikali na usalama wa watawala tu.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Katika eneo letu hili (la Mashariki ya Kati) viko pia vikosi vya namna hiyo ambavyo baadhi yake kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja sasa vinatumia nguvu zao zote kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya Yemen na wananchi wake, na pamoja na hayo hadi leo hii vimeshindwa kufanikisha chochote cha maana.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kuna vikosi vingine vya kijeshi ambavyo kijuu juu vinaonekana kuwa na nguvu kubwa za kufanya opereseheni za kijeshi lakini vinapoingia kwenye medani ya operesheni vinaonesha mabavu ya kijeshi tu na vinafanya mambo yasiyoingilika akilini na yasiyo na chembe ya huruma; na mfano wa wazi wa jambo hilo ni vitendo vya jeshi la Marekani katika nchi za Iraq na Afghanistan, na wakati vikosi kama hivyo vya ulinzi vinaposhindwa katika medani ya mapambano, havisiti hata chembe kutumia vikosi vya watu waliokubuhu katika kutenda jinai kama vile vikosi vya Black Water.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema amesisitiza kuwa, vikosi vya ulinzi vya Iran ndivyo vikosi pekee duniani ambavyo vimesimama juu ya msingi wa chuo cha kidini na misukumo ya kimaanawi na wakati huo huo vinafanya kazi zake kwa umakini na uwezo wa hali ya juu tena katika nchi ya Iran ambayo ina uhuru kamili wa kisiasa.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesisitiza kuwa: Kazi za kijeshi ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si kazi za kimaonesho na kimapambo tu na pia si kazi za kufanya operesheni zisizodhibitiwa au zisizoingilika akili au zisizojali na kuzingatia pande zote kabla ya kuchukua hatua.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kuongezwa uwezo wa opereseheni za vikosi vya ulinzi ambavyo ni majimui ya kitaasisi, ya vifaa, ya mafunzo na ya kuimarisha nguvu sambamba na kupandisha juu uwezo wa kimaanawi kuna maana ya kutenda mambo yake kwa zaidi ya utekelezaji wa faradhi na suna za kidini na inabidi ndani kabisa ya nyoyo za maafisa wa vikosi vya ulinzi mambo hayo yawe na nafasi kubwa na ni hapo ndipo vikosi vya ulinzi vitaweza kuhisi kuwa na nguvu za kweli.
Kabla ya hotuba ya Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran, Meja Jenerali Hassan Firouzabadi, Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran ametoa ripoti fupi kuhusu kazi na mipango ya baadaye ya vikosi hivyo na kusema: Vikosi vya ulinzi vya Iran vinajua vyema kwamba, kuongeza uwezo wake wa kijeshi na kujilinda hususan katika upande wa kuimarisha akiba yake ya makombora ya balestiki na kupanua kambi zake za makombora ndiko kunakodhamini uwezo wa vikosi hivyo wa kuulinda Uislamu wa kweli na usalama wa taifa pamoja na mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni kwa msingi huo ndio maana tunaamini kuwa, hivi sasa kufanyika mazoezi ya kijeshi ni jambo la dharura na mazoezi hayo yataendelea.
Kabla ya mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Khamenei amewasalisha hadhirina Sala za Adhuhuri na Laasiri.
 
< Nyuma   Mbele >

^