Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Kazakhztan Chapa
11/04/2016
Meeting with Kazakhstan presidentAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni (Jumatatu) ameonana na Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan na huku akigusia udharura wa kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa nchi mbili katika nyuga tofauti za kisiasa, kiuchumi, kimataifa na katika vita dhidi ya ugaidi amesema kuwa: Baadhi ya madola hususan Marekani si wakweli katika madai yao ya kupambana na ugaidi, lakini nchi za Kiislamu zinaweza kupambana vilivyo na vitisho vyote vinavyoukabili ulimwengu wa Kiislamu kwa kuwa na ushirikiano wa kweli baina yao.
Ayatullah Udhma Khamenei ameitaja misaada ya Wamarekani kwa kundi la Daesh huko Iraq kuwa ni mfano wa wazi wa kutokuwa wakweli miungano mbali mbali inayodai kupambana na ugaidi na kuongeza kuwa: Madola hayo yanafanya njama za kuhalalisha vitendo vyao hivyo vya kindumilakuwili kwa kuugawanya ugaidi katika aina mbili; ugaidi mzuri na ugaidi mbaya.
Kiongozi Muadhamu wa Maipnduzi ya Kiislamu ameashiria namna watu wenye uraia wa nchi za Ulaya wanavyofanya mashambulio ya kigaidi barani humo na vile vile kuweko kwa wingi watu watokao Ulaya katika makundi ya kigaidi yanayofanya mauaji na jinai nchini Iraq na Syria na kuongeza kuwa: Uhakika huo unathibitisha kuwa kwamba hakuna nia ya kweli kwa nchi za Magharibi hususan Marekani katika suala zima la kupambana na ugaidi.
Amesema dunia ya leo ni dunia iliyozongana na kuongeza kuwa: Nchi za Kiislamu leo hii kwa upande mmoja zinakabiliwa na makundi ya kigaidi ambayo yanatumia jina la Uislamu kutenda maovu dhidi ya Waislamu kwani kwa hakika makundi hayo yako dhidi ya Uislamu na Waislamu na kwa upande mwingine zinakabiliwa na vitimbi na ubeberu wa baadhi ya madola ya Magharibi ambayo hayapendi kuziona nchi za Waislamu zinaungana na kuwa kitu kimoja.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kupambana na hatari ya ugaidi na miamala ya kindumilakuwili ya madola ya kibeberu kuwa linahitajia ushirikiano wa nchi za Kiislamu chini ya msingi wa siasa za kimantiki na zinazoingilika akilini na kuongeza kuwa: Sisi tunazihesabu nchi zote za Waislamu kuwa ni ndugu zetu na kwamba misimamo ya Iran na Kazakhstan nayo ni ya aina moja katika masuala mengine ya kimataifa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia ushirikiano wa Kazakhstan na Iran katika jumuiya za kimataifa na kusisitiza kuwa: Pamoja na mataifa haya mawili kuwa ni dini, historia na utamaduni wa aina moja pamoja na fursa na nyuga nyingi za ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili, lakini kiwango cha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi wa nchi hizo mbili hakionekani kupanda na sisi tunakaribisha kuongezwa kiwango cha ushirikiano wa nchi hizi mbili katika masuala tofauti ya kisiasa, kiuchumi, kibiashara, usafiri na uchukuzi pamoja na ushirikiano katika masuala ya mfumo wa kisheria wa eneo la bahari ya pamoja.
Katika mazungumzo hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan amesema kuwa, Iran ni jirani yetu mkubwa na mwenye nguvu, anayeaminika na anayefaa kutegemewa na kuongeza kuwa: Nchi hizi mbili zina fursa na nyuga nyingi za kustawisha uhusiano wao na sisi katika ziara yetu hii tumefikia makubaliano mazuri sana katika upande wa masuala ya kiuchumi na kibiashara na ni matumaini yetu kupitia mikataba hiyo kutakuwa na ongezeko zuri la ushirikiano baina ya nchi mbili.
Rais wa Kazakhstan ameongeza kuwa, ugaidi ni tishio kubwa na huku akigusia matukio ya kigaidi yanayotokea katika nchi za Magharibi na njama za Wamagharibi za kujaribu kuuhusisha Uislamu na vitendo hivyo vya kigaidi na kusema kuwa: Ugaidi na wimbi la wakimbizi kwa hakika ni vitu vinavyotokana na vitendo vya madola ya Magharibi kukabiliana na tawala halali katika eneo hili, kwani wakati serikali kuu inapokosa utulivu na kushindwa kudhibiti masuala ya nchi, nafasi yake huchukuliwa na ugaidi.
Rais Nazarbayev amezungumzia pia uwezo na nguvu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ushawishi wa kimaanawi alio nao Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika nchi za Kiislamu na kumwambia Ayatullah Udhma Khamenei kwamba: Mimi ninaafikiana kikamilifu na nadharia zako kuhusu umoja wa ulimwengu wa Kiislamu na tunapaswa tuuoneshe ulimwengu mzima kuwa Uislamu ni dini ya maendeleo, ya umoja na ni dini inayopiga vita kikamilifu vitendo vyote vya kigaidi.
 
< Nyuma   Mbele >

^