Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Uteuzi wa Dk Abdolali Ali Asgari kuwa Mkuu wa IRIB Chapa
11/05/2016
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa hukumu ya kukubali kujiuzulu Bw. Mohammad Sarafraz na kumshukuru kwa jitihada zake za kimapinduzi zenye thamani kubwa na kupitia hukumu hiyo hiyo amemteua Dk Abdolali Ali Asgari kuwa mkuu mpya wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB.
Matini kamili ya hukumu ya uteuzi huo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Janab Dk Abdolahi Ali Asgari (Mwenyezi Mungu azidi kukupa taufiki)
Kufuatia kujiuzulu Janab Bw. Mohammad Sarafraz na sambamba na kumshukuru kwa jitihada zake za kimapinduzi, zenye thamani kubwa na alizozifanya kwa dhati ya moyo wake, jambo ambalo kamwe halipaswi kusahauliwa; natumia fursa hii kukuteua kuwa mkuu mpya wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hasa kwa kuzingatia historia yako ya kimapinduzi na uzoefu wako wa uongozi katika shirika hilo la taifa la utangazaji.
Jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa ni maelezo yote yaliyomo katika hukumu ya kumteua Janab Bw. Sarafraz kushika wadhifa huo. Hivyo ninaagiza kwa kusisitiza kuwa, lazima izingatiwe na kupewa umuhimu mkubwa mipango mizuri, kuchungwe mikakati na stratijia kuu, kuvutia na kulinda na kulea nguvu kazi ya kimapinduzi na yenye faida na kuwemo kwa nguvu zote na kikwelikweli katika Intaneti na kwenye mwasiliano ya kompyuta. Na mtegemee na tawakali kwa Mwenyezi Mungu katika kazi zako.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu akupe taufiki Yake.
Sayydi Ali Khamenei
22 Ordibehesht 1395
(Jumatano, Mei 11, 2016)
 

Katika hukumu nyingine, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemteua Bw. Sarafraz kuwa mjumbe katika Baraza Kuu la Mawasiliano ya Kompyuta la Iran. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB, Bw. Sarafraz alikuwa ni mjumbe binafsi wa Baraza hilo Kuu la Mawasiliano ya Kompyuta.

 
< Nyuma   Mbele >

^