Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mnasaba wa Kuzinduliwa Baraza la Tano la Wanavyuoni Wataalamu Chapa
24/05/2016
Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kuanza kazi za Baraza la Tano la Wanavyuoni Wataalamu linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu na sambamba na kuwapongeza wajumbe wa baraza hilo kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na wananchi amesisitiza kuwa: Umuhimu wa baraza hilo adhimu, unatokana na ukubwa wa jukumu ambalo linabebwa na wajumbe hao waliochaguliwa na wananchi wa baraza hilo na jukumu hilo ni kuulinda kwa umakini mkubwa na kwa pande zote, utambulisho wa Kiislamu na Kimapinduzi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuzielekeza taasisi zenye mfungamano mkubwa za mfumo huo upande wa kufanikisha malengo aali na makubwa ya Jamhuri ya Kiislamu.
Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambao umesomwa leo asubuhi na Hujjatul Islam Walmuslimin Mohammadi Golpeygani, mkuu wa ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Kuanza kazi za Baraza la Tano la Wanavyuoni Wataalamu katika siku za maadhimisho ya siku ya kuzaliwa walii mkuu wa Mwenyezi Mungu (Imam Mahdi AS) ni sadfa iliyojaa baraka ambayo inabidi ihesabiwe kuwa ni bishara njema yenye kuleta yakini ya kupata msaada na auni ya Mwenyezi Mungu pamoja na muawana na radhi za Imam Mahdi AS katika moyo wa muumini na kumfanya azidi kusadikisha ahadi za Mwenyezi Mungu, na kuzidi kuwa imara moyo wake. Aidha uzinduzi wa baraza hilo la tano umesadifiana na tarehe 3 Khordad ambayo ni nembo ya ushindi wa muqawama na kupeperushwa juu bendera ya ushindi na ya ukombozi wa Mwenyezi Mungu, (ukombozi wa mji wa Khorramshahr wa Iran kutoka mikononi mwa utawala wa wakati huo wa Iraq, mwaka 1982) na inabidi kujua thamani ya jambo hilo na kupata funzo katika sadfa hiyo ya kustaajabisha.
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Azizi na Mwingi wa hekima kwa moyo wangu wote kwa kulipa taifa la waumini, taifa shujaa na la watu waaminifu (la Iran) taufiki ya kuunda baraza kama hilo na kuufanya umma kwa mara nyingine tena kutoa bay'a na kutangaza utiifu na uungaji mkono wao kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Ninatoa pongezi zangu kwenu nyinyi mlioshinda katika uchaguzi kutokana na kuaminiwa na wananchi na kuamua kukupeni kura zao na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mjuzi na anayeona kila kitu, akupeni taufiki ya kuihudumia nchi na wananchi kwa njia bora kabisa.
Umuhimu wa baraza hilo adhimu unatokana na ukubwa na adhama ya jukumu ambalo liko mabegani mwa wajumbe wake waliochaguliwa na wananchi. Jukumu na mas'uliya hiyo tunaweza kusema katika maneno machache kuwa ni:
Kuulinda kwa umakini mkubwa na kwa pande zote utambulisho wa Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unaotawala nchini na kuzielekeza taasisi za mfumo huo zenye mfungamo wa karibu baina yao, kuelekea upande wa kufanikisha malengo yake aali na matukufu. Ufanikishaji wa jukumu hilo zito na gumu unahitaji kuwa na ustahiki ambao umeashiriwa pia na Katiba.
Kazi ya kuainisha kuwepo na kubakia kwake ustahiki huo ni ya baraza hilo adhimu na hilo lenyewe ni jukumu na ni mas'uliya kubwa kwa baraza hilo. Kutambua nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu katika dunia ya leo; kuuzingatia mfumo wenye mvuto mkubwa wa demokrasia ya kidini kutoka katikati ya kundi kubwa la mbinu za kila aina za utawala ambazo ndani yake imma umaanawi na dini au wananchi au yote mawili yamekuwa wahanga humo; kuzingatia nafasi isiyo na mbadala ya imani na itikadi zinazotokana na mafundisho ya Uislamu katika namna ya uteuzi wa wananchi; kuzingatia athari za taqwa ya mtu binafsi ya na kisiasa ya Kiongozi Muadhamu mwenyewe katika kulinda na kuhifadhi imani ya wananchi na usalama, uimara na kutotereka mfumo (wa Jamhuri ya Kiislamu)... yote hayo ni sehemu ya majukumu ya baraza hilo adhimu ambalo linaundwa na wanavyuoni wanaopendwa na wananchi na wenye taathira katika jamii. Ninatumia fursa hii kukumbushia umuhimu wa majukumu hayo na wajibu wa kutekelezwa kwa umakini unaotakiwa. Kila moja na mambo hayo lina ndani yake majukumu ambayo iwapo yatatekelezwa vizuri yatapelekea nchi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu uzidi kupata ustahiki na umakini wa hali ya juu na kumsaidia Kiongozi Muadhamu katika ufanikishaji wa jukumu lake kubwa ambalo halina kifani.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Manani akupeni nyote waheshimiwa taufiki ya kutekeleza vizuri majukumu yenu katika njia hii iliyobarikiwa ambayo ni njia ya Imam wetu mtukufu na ndilo lililokuwa lengo lake kuu na muhimu mno.
Sayyid Ali Khamenei,
1 Khordad 1395
(Mei 21, 2016).

 
< Nyuma   Mbele >

^