Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Makamanda wa Kituo cha Anga cha Jeshi ya Khatamul Ambiya SAW Chapa
28/08/2016
Commanders & officials of the army's Khatam Al-Anbia Air Defense Base met with LeaderAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo mchana (Jumapili) ameonana na makamanda na maafisa wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na huku akisisitizia umuhimu wa ulinzi huo ukiwa ni mstari wa mbele katika kukabiliana na mashambulizi yoyote yale amesema kuwa, kambi inayokabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ni kambi ya watu makhabithi, malaghai na wapinzani wa uhuru wa taifa la Iran. Aidha amesema: Inabidi kuviimarisha vilivyo vikosi vyetu vya ulinzi kwa kadiri kwamba adui hatokuwa hata na fikra ya kuishambulia nchi yetu, katika kukabiliana na adui wa namna hii ambaye lengo lake ni kudhoofisha uwezo na nguvu za kiulinzi cha nchi yetu.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amesema ulinzi wa anga ni mstari wa mbele katika kukabiliana na mashambulizi ya aina yoyote ile.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, vikosi vya ulinzi nchini vinapaswa kujiimarisha kwa kila namna kwa ajili ya kukabiliana na adui huyu ambaye lengo lake kuu ni kutaka kudhoofisha uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu, na vijiimarisha kiasi kwamba ifike mahala adui asiweze hata kufikiria kuivamia Iran.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa, azma, nia na uwezo wa nguvu kazi ni mambo muhimu ya kuweza kuondoa vizuizi na mapungufu yanayojitokeza na kuongeza kwamba: Kambi ya Ulinzi wa Anga ni moja ya mistari mikuu ya mbele vitani na inabidi thamani ya nafasi hiyo itunzwe na kufanyike jitihada za kila upande kwa kutumia azma, nia ya kweli na kutotetereka ili kudhoofisha nia ya adui ya kuishambulia Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, uadui dhidi ya taifa la Iran na dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni mkubwa zaidi ikilinganishwa na uadui unaojulikana leo duniani baina ya nchi na mataifa mbalimbali. Ameongeza kuwa, kambi inayokabiliana na Iran kama vile kambi ya mabeberu au Uzayuni wa kimataifa ni kambi ya watu makhabithi, malaghai na wenye fikra za kidhulma ambayo uadui wao ni dhidi ya asili ya itikadi za kidini, uhuru na kutokubali kuburuzwa taifa la Iran.
Amesema uadui wa kambi hiyo unadhihirishwa kwa sura tofauti na kuongeza kuwa: Uadui huo utaona siku moja unadhihirika kwa sura ya Marekani na siku nyingine kwa sura ya tawala za kidhalimu kama za Saddam, amma lililo muhimu ni kuwa, Iran inapaswa kuchukua misimamo na maamuzi sahihi na kuyafanyia kazi kivitendo kwa kutumia suhula na uwezo wake mwingi ilio nao pamoja na kuelewa vizuri zama zilizopo na mipango ya adui.
Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, kuzuka makelele mengi kuhusu mfumo wa kujilinda kwa mokombora wa S-300 au taasisi kama ya Fordow ni miongoni mwa mifano ya wazi ya ukhabithi wa adui wa taifa la Iran. Ameongeza kuwa: Mfumo wa kujilinda kwa makombora wa S-300 ni mfumo wa kujilinda na kujihami; si mfumo wa kushambulia, lakini pamoja na hayo Wamarekani wanafanya njama zao zote kuzuia Iran isifaidike na mfumo huo ambao hauna madhara kwa nchi yoyote ile.
Amesema: Sisi tunakabiliwa na adui ambaye hataki hata tufaidike na haki yetu ya kujilinda ili wakati wowote wanapotaka kuishambulia nchi yetu waweze kufanya hivi bila ya upinzani wowote.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran vile vile amehimiza watu kuwa macho, kuchukua hatua kwa wakati unaofaa na kutumia mbinu za kila namna pamoja na silaha za kisasa za ulinzi wa anga na kusisitiza kuwa: Adui anapaswa kuelewa kuwa kama atatushambulia basi atapata pigo kubwa na kwamba kujihami kwetu huko kutaambatana na majibu pia.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Farzad Ismaili, kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Ambiya SAW ametoa hotuba fupi na sambamba na kuenzi maadhimisho ya mwaka wa nane wa kuanzishwa kituo hicho ametoa ripoti fupi kuhusiana na hatua muhimu zaidi zilizochukuliwa na kituo hicho hadi hivi sasa.
 
< Nyuma   Mbele >

^