Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Makamanda wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Iran Chapa
27/11/2016
Navy commanders and forces met with Ayatollah KhameneiAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo (Jumapili) ameonana na makamanda na maafisa wa kikosi cha majini cha jeshi la Iran na kuyataja maendeleo na uwezo mkubwa wa kikosi hicho katika nyuga tofauti kama za nguvu kazi za watu, uongozi, ufundi na teknolojia kuwa ni nguzo muhimu inayopasa kuzingatiwa kuhusiana na kikosi hicho na kuongeza kuwa: Jambo la lazima katika kuondoa mapungufu yaliyopo ni hima ya hali ya juu na kutosalimu amri mbele ya vizuizi na changamoto mbali mbali zinazojitokeza.
Katika mkutano huo ulioitishwa kwa mnasaba wa maadhimisho ya tarehe 7 Azar (Novemba 27), siku ya kikosi cha majini cha jeshi nchini Iran, Ayatullah Udhma Khamenei amegusia umuhimu wa utaalamu wa kiufundi katika harakati za baharini za baadhi ya nchi na kuongeza kuwa: Nchi yetu ina mipaka mikubwa na mipana ya majini na vile vile ina historia kongwe na ndefu ya ubaharia na harakati za baharini, hivyo nguvu na uwezo wa jeshi la majini la Jamhuri ya Kiislamu unapaswa kuwa katika hadhi na kiwango cha Jamhuri ya Kiislamu na historia ya nchi hii.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kuweko nguvu za jeshi la majini la Iran katika maji huru kuwa kuna maana ya kuongezeka nguvu na uwezo wa Iran na kusisitiza kuwa: Inabidi kikosi cha majini cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kiimarishe zaidi uwepo wake katika maji huru kote ulimwenguni.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelionya Baraza la Congress la Marekani akisisitiza kuwa, hatua yoyote ya kuvirudisha vikwazo ambavyo muda wake umeisha ni uwekaji wa vikwazo vipya na ni uvunjaji wa makubaliano.
Aidha amegusia mazungumzo ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1 yaliyomalizika kwa kufikiwa makubaliano ya JCPOA na kuonya kuhusu mpango wa Baraza la Congress la Marekani wa kurefusha vikwazo dhidi ya Iran huku likidai kuwa hivyo si vikwazo vipya bali ni kurefusha tu vikwazo. Amesema, hakuna tofauti yoyote baina ya kuweka vikwazo vipya na kuendeleza vikwazo ambavyo muda wake umeisha, na kwamba hatua hiyo ya kurefusha muda wa vikwazo ni uvunjaji wa makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa baina ya Iran na kundi hilo la 5+1.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Admeri Habibullah Sayyari, Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa ripoti fupi kuhusiana na kazi na hatua zilizochukuliwa na kikosi hicho na kuema: Kikosi cha Majini cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kinaendeleza uwezo wake katika maji huru kwa nguvu zake zote na hivi sasa kimepanua wigo wa uwepo wake katika maeneo ya nje ya eneo hili.
Katika mkutano huo, hadhirina wamesalishwa Sala za Adhuhuri na Laasiri na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei.
 
< Nyuma   Mbele >

^