Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Muungano wa Mashia wa Iraq Chapa
11/12/2016
Sayyed Ammar Al-Hakim and Ayatollah KhameneiAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumapili) ameonana na Hujjatul Islam Ammar Hakim, mkuu wa Muungano wa Kitaifa wa Mashia wa Iraq na wajumbe wakuu wa muungano huo na sambamba na kuelezea kufurahishwa kwake na kuundwa muungano huo baina ya makundi ya Mashia wa Iraq amelitaja jambo hilo kuwa ni hatua muhimu na wakati huo huo ametilia mkazo ulazima wa kulindwa na kutiwa nguvu umoja huo na kuiangalia mirengo, kaumu na watu wa madhehebu yote nchini Iraq kwa jicho la baba.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na mjukuu wake Imam Jafar al Sadiq AS na vile vile ushindi wa mtawalia linaopata taifa la Iraq huko Mosul na kusema kuwa jukumu la mkuu na wajumbe wakuu pamoja na mirengo yote ya ndani na nje ya Iraq ya muungano wa kitaifa wa Mashia ni kubwa mno na kwamba uamuzi na hatua yao yoyote ile ya muungano huo inaathiri matukio ya Iraq, ya eneo la Mashariki ya Kati na ya ulimwengu mzima wa Kiislamu. Ameongeza kuwa, ili kuweza kufikia malengo yenye thamani ya muungano wa kitaifa hakuna njia nyingine isipokuwa kuwa na umoja na mshikamano na inabidi kuwa macho wakati wote kwa ajili ya kuliendeleza jambo hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei ametaja moja ya majukumu muhimu ya muungano huo wa kitaifa kuwa ni kuzilinda serikali zinazoingia madarakani nchini Iraq na sambamba na kuelezea kufurahishwa kwake na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Waziri Mkuu wa Iraq, Haydar al Abadi, hususan kushirikiana vilivyo na vikosi vya kujitolea vya wananchi vya al Hashdu al Shaabi amesisitiza kuwa: Al Hashdu al Shaabi ni utajiri adhimu na ni akiba kubwa kwa ajili ya leo na kesho ya Iraq kutokana na kuwa ni vikosi vilivyoundwa na wananchi wenyewe wa nchi hiyo na inabidi ilindwe na kuungwa mkono.
Aidha amelitaja suala la kutiliwa nguvu elimu na utafiti kwa ajili ya maendeleo na nguvu za kielimu za Iraq kuwa ni jambo muhimu mno na kusema: Kuvitia nguvu vyuo vikuu na kuimarisha misingi ya kielimu na kiutafiti ya Iraq ni majukumu ambayo lazima yapewe uzito mkubwa hususan kwa kuzingatia kuwa Wamarekani na maadui wengine wa taifa la Iraq wameua wataalamu wengi sana wa nchi hiyo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa nasaha nyingine muhimu kwa Muungano wa Mashia wa Iraq akiwaambia: "Musiwaamini hata kidogo Wamarekani"
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Wamarekani wanapinga suala la kuwa na nguvu nchi za Kiislamu ikiwemo Iraq na kusisitiza kuwa: Haipasi kupumbazwa na kulaghaiwa hata kidogo na dhahiri yao na tabasamu zao za mdomoni.
Amesisitiza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu siku zote yanatufundisha kuwa tusiiamini Marekani. Sisi katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kila tulipochunga nasaha hizo tumeshinda na kila tulipozidharau tumepata madhara.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kwamba, tofauti na wanavyodai Wamarekani, lengo lao kamwe si kuwamaliza magaidi wakufurishaji bali wanafanya kila njia kuwahifadhi magaidi hao kwa ajili ya malengo yao ya siku za usoni.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Hivi sasa Wamarekani hawapendi kabisa kuona magaidi wanaangamizwa kikamilifu huko Mosul Iraq na nchini Syria.
Vile vile amegusia namna genge la Daesh lilivyokuwa likipora na kuuza mafuta ya Iraq na kusema: Wakati magaidi wa Daesh walipokuwa wanapora mafuta ya Iraq, Wamarekani walikuwa wanaangalia kwa macho tu jinsi milolongo mirefu ya malori ya mafuta hayo yalivyokuwa yanapelekwa nje ya Iraq, hivyo haifai kabisa kuwaamini Wamarekani.
Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, mustakbali wa Iraq unang'ara, na kwamba maendeleo ya Iraq ni kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuimarishwa ushirikiano baina ya nchi hizi mbili kwa kadiri inayowezekana ni kwa manufaa ya pande zote mbili.
Katika sehemu ya mwisho ya matamshi yake, Ayatullah Udhma Khamenei ameyashukuru matabaka yote ya wananchi wa Iraq na viongozi wa nchi hiyo kwa kupokea mamilioni ya wageni wa Imam Husain AS wakati wa Arubaini ya mtukufu huyo na kusema kuwa, Arubaini ya Imam Husain AS ni tukio lisilo na mfano wake.
Mwanzoni mwa mazungumzo hayo, Hujjatul Islam Ammar Hakim, mkuu wa Muungano wa Mashia wa Iraq sambamba na kumshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa miongozo yake iliyojaa busara na hekima na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu kwa taifa la Iraq ametoa ripoti kuhusu mchakato wa kuundwa muungano huo wa kitaifa na hatua zilizochukuliwa hadi hivi sasa. Vile vile ametoa pongezi zake kwa ushindi mkubwa uliopatikana dhidi ya magaidi katika nchi za Iraq, Syria na Yemen na kusema kuwa: Moja na matunda ya Muungano wa Kitaifa wa Mashia wa Iraq ni kupasishwa sheria ya kuvitambua rasmi vikosi vya kujitolea vya wananchi yaani al Hashdu al Shaabi ambapo mbali na kuungwa mkono na muungano huo, wabunge wa mirengo na makundi mengine nao waliliunga mkono suala hilo.
 
< Nyuma   Mbele >

^