Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Sherehe za Kuingia kwenye Baleghe Wanafunzi wa Shule za Msingi Zilizohudhuriwa na Kiongozi Muadhamu Chapa
13/12/2016
Sherehe zilizojaa umaanawi za kubaleghe na kuanza kubeba majukumu ya kidini wanafunzi elfu mbili wa kiume wa shule za msingi za mkoa wa Tehran zimefanyika leo usiku (Jumanne) katika Husainia ya Imam Khomeini (quddisa sirruh) na kuhudhuriwa na Ayatullah Udma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika sherehe hizo zilizofanyika katika anga iliyojaa mapenzi, hamasa na shauku kubwa kwa mnasaba wa kuingia wanafunzi hao katika umri wa baleghe na kubeba majukumu ya kidini, Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Katika hatua mbali mbali za maisha yake, mwanadamu hupitia katika matukio mengi na tajiriba chungu nzima ambazo inabidi akabiliane nazo kishujaa ili aweze kufanikiwa duniani na Akhera.
Katika sehemu moja na miongozo yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, moja ya malengo makuu ya adui ni kujipenyeza kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni nchini Iran na anawalenga zaidi vijana na mabarobaro wa taifa hili la Kiislamu.

Ayatullah Udhma Khamenei amesema, mabarobaro ambao ni watoto wa taifa la Iran leo hii, kesho watakuwa watu wazima na viongozi wa nchi, hivyo wana jukumu la kushiriki vilivyo katika minasaba na mijumuiko mbalimbali ili kujiwekea kinga ya njama kama hizo za adui.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesema, kipindi cha kubaleghe mtu ni wakati muhimu sana ambao inabidi utumiwe vizuri kumfanya kijana abaleghe kimaanawi na kuongeza kuwa, siri ya maendeleo ya mtu binafsi na ya kijamii ni kulindwa uhusiano baina ya mtu huyo na Mwenyezi Mungu na kwamba kosa kubwa linalofanywa na ustaarabu wa Magharibi ambao hivi sasa unazidi kutoweka na kusambaratika, ni kujiweka kwake mbali na Mwenyezi Mungu.
Aidha, Ayatullah Udhma Khamenei amewataka vijana na mabarobaro kuwafanya mashahidi wa njia ya haki kuwa ruwaza na kigezo chao na kuwakumbusha kwa kuwaambia: Vijana wetu wengi azizi waliouawa kwenye njia ya kulinda uhuru wa taifa lao na maslahi ya nchi yao kwa lengo la kuondoa shari ya maadui, walijitolea kitu azizi na chenye thamani kubwa zaidi kwao, yaani nafsi na roho zao katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Amesema, njia bora kabisa ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu ni kushikamana na Sala na kusoma Quráni na kuongeza kuwa, kwa kutilia maanani kwamba mtu huwa anazungumza moja kwa moja na Mwenyezi Mungu Mtukufu na Muweza wakati wa Sala, ibada hiyo humtunukia mja nguvu za kutawakali kwa Allah, ushujaa na kujiamini, hivyo dumisheni Sala ya mwanzo wa wakati wake na itekelezeni ibada hiyo kwa mazingatio na shikamaneni na kusoma Quráni na kuzingatia maana na uongofu uliomo ndani yake ili mzidi kuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

 
< Nyuma   Mbele >

^