Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Zabol - Kitovu cha Dunia! Chapa
09/02/2008

Miezi michache kabla ya kuaga dunia Imam Khomeini (r.a), nilikuwa nikiulizwa mara kwa mara kwamba baada ya kumalizika kipindi changu cha Urais wa Jamhuri, ninakusudia kufanya nini. Mimi mwenyewe ninapenda sana kujishughulisha na kazi za kielimu. Hivyo, nilikuwa nikifikiria kwamba baada ya kumaliza kipindi changu cha Urais wa Jamhuri, nitakwenda kukaa pembeni nijishughulishe na kazi za kielimu. Nilipoulizwa swali kama hilo, nilijibu: "Endapo baada ya kumalizika kipindi changu cha Urais wa Jamhuri, Imam ataniambia niende Zabol na kuwa mkuu wa idara ya kisiasa na kiitikadi ya askari wa polisi wa huko, hata kama badala ya kikosi, nitapewa kituo tu, basi nitamchukua mke wangu na watoto wangu na kuelekea huko! Wallahi! Niliyasema hayo kwa udhati wa moyo wangu. Yaani kwangu mimi Zabol ingekuwa ni kitovu cha dunia na mimi ningekaa huko na kujishughulisha na kazi za kisiasa na kiitikadi. Kwa maoni yangu, inatakikana kuwa na moyo wa aina hiyo na kujituma na kufanya juhudi na hima. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu atakapotia baraka katika kazi na mambo yetu.
(Imenukuliwa katika hotuba aliyotoa tarehe 24 Februari 1992 kwa wakuu wa Taasisi ya Tablighi za Kiislamu)

 
< Nyuma

^