Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kumbukumbu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kuhusiana na Baba Yake Chapa
09/02/2008

Miongoni mwa sifa ambazo alikuwa nazo marehemu baba yangu na vilevile marehemu mama yangu na ambazo kwa kweli ni vitu vya ajabu ambavyo kila ninapofikiria nahisi ni watu wachache niliowaona kuwa na sifa hizo, ni kule kutojali na kutovutiwa na vitamanishavyo na mali za dunia. Kwa kweli kuna haja kwetu sote kujizoesha kuwa na sifa hii.
Mwaka 1972 marehemu Shahid Qadhi Tabatabai, Imam wa Ijumaa wa Tabriz alikuja hapa (Mashhad). Akaniambia: "Miaka arobaini iliyopita mimi na baba yangu tuliondoka Tabriz na kuja Mashhad na tukaamua kumpitia Mzee (Sayyid Jawad). Siku hiyo miaka arobaini iliyopita, Mzee alikaa mahala palepale ambapo ameketi leo, na mimi nimekaa palepale alipokuwa ameketi baba yangu miaka arobaini iliyopita; chumba hiki na nyumba hii iko vilevile haijabadilika hata chembe."
Kizazi kimoja kizima kilikuwa kimepita, lakini yeye alikuwa kama alivyokuwa miaka arobaini iliyopita. Wakati kaka yangu - Sayyid Hasan - alipotaka kuoa, kwa vile hatukuwa na pa kumweka, tulikibomoa chumba kile na kujenga vyumba viwili vidogovidogo. Kile kijichumba kidogo cha chini ya ardhi kilikuwa na mlango. Hivyo chumba hicho kikageuzwa hamamu (bafu) na nyumba yetu ikawa nyumba yenye hamamu. Lakini wakati huo mimi nilikuwa siko tena huko. Hivyo chumba kikubwa kikawa chumba cha wageni.

 
< Nyuma

^