Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Maana ya Nauruzi Chapa
09/02/2008

Nauruzi (Nairuzi) maana yake ni siku mpya! Katika riwaya (mapokezi) yetu na hasa ile riwaya maarufu ya Mu'illi bin Khunais imezingatia zaidi nukta hii. Mu'illi bin Khunais ambaye ni mmoja wa wapokezi mashuhuri wa hadithi katika masahaba, na ambaye kwa mtazamo wetu sisi ni mtu wa kuaminika, ni mmoja wa shakhsia mashuhuri na mtu wa ndani katika nyumba ya watu wa Mtume. Yeye alipitisha maisha yake akiwa pamoja na Imam Jaafar Sadiq (sala na salamu zimshukie) na baadaye akauawa shahidi. Huyu Mu'illi bin Khunais akiwa na sifa hizi, siku moja alikwenda kwa Imam Sadiq, na kwa bahati ilisadifu na siku ya Nauruzi.
Imam akamwambia: "Unajua ni nini Nauruzi?" Baadhi ya watu wanadhani kwamba Imam alizungumzia masuala ya historia katika riwaya hii, kwamba katiku siku hiyo ndipo yalipojiri matukio ya kuteremshwa duniani Adam, safina ya Nuh, kutangazwa Wilaya (Ukhalifa) wa Amirul Muuminin Ali AS, n.k. Lakini mimi sikuifahamu hivyo riwaya hii.
Nilivyoelewa mimi ni kwamba hapa Imam anaelezea maana ya Nauruzi. Makusudio yake ni haya: Leo watu wameipa jina la "Nauruzi" kwa maana ya "siku mpya". Nini maana ya siku mpya? Siku zote za Mwenyezi Mungu zinafanana. Ni siku gani inaweza kuwa siku "mpya"? Kuna sharti. Nauruzi au siku mpya ni ile siku lilipojiri tukio kubwa. Ile siku ambayo wewe utaweza kufanya jambo kubwa, hiyo ni Nauruzi. Kisha Imam akatoa mifano kwa kusema: "Ile siku ambayo Nabii Adam na Bi Hawa walikanyaga ardhi ya dunia, ilikuwa Nauruzi. Ilikuwa ni siku mpya kwa wana wa Adam na kizazi chao. Ile siku ambapo baada ya tufani iliyogharikisha kila kitu safina ya Nuh ilivuka salama hadi ufukweni, ilikuwa siku mpya. Ni siku mpya ambapo ukurasa mpya ulifunguliwa katika maisha ya mwanadamu. Ile siku Qur'ani ilipoteremshwa kwa Bwana Mtume ilikuwa siku mpya kwa wanadamu. Hivi ndivyo ilivyo hakika ya suala hilo.
Siku ilipoteremshwa Qur'ani kwa wanadamu ilikuwa ni sehemu katika historia ambapo kwa wanadamu ilikuwa ni siku mpya. Siku hiyo ambapo Amirul Muuminin [Ali] alichaguliwa kuwa Imam ilikuwa ni siku mpya. Siku zote hizo ni Nauruzi. Iwe kwa majibu wa kalenda ya Shamsia (Jua) inaafikiana au haiafikiani na siku ya kwanza ya mwezi wa Kondoo (Hamal). Hilo silo alilokusudia kuzungumzia Imam kwamba matukio yote hayo yalijiri tarehe mosi ya mwezi wa Kondoo, yaani tarehe mosi Farvardin (21 Machi). Si hivyo! Suala ni kwamba siku yoyote ambayo ndani yake yatajiri matukio yenye sifa kama hizo ni siku mpya na ni Nauruzi. Iwe ni tarehe mosi Farvardin (21 Machi) au siku nyingine yoyote katika nyakati za mwaka.

 
< Nyuma   Mbele >

^