Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ahmad Sukarno Alitufanya Tuwe Marafiki Chapa
09/02/2008

Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) iliweza katika kipindi takriban kirefu kuwa na sauti duniani. Lakini kwa bahati mbaya, leo hii nafasi ya NAM imefifia. Kwa hakika, waasisi wakuu wa Jumuiya hii walikuwa ni watu watatu au wanne hivi ambapo hayati Ahmad Sukarno ndiye aliyekuwa na nafasi kubwa zaidi.

Haitokuwa vibaya nikasimulia hapa kumbukumbu moja inayohusiana na yeye. Katika mwaka 1353 Hijria Shamsia (1974 Miladia), mimi pamoja na mtu mmoja au wawili hivi, tulifungwa kwenye seli moja ndogo sana (katika jela moja) ya Tehran. Urefu wa seli hiyo ulikuwa ni mita 2 na sentimita 20, na upana wake mita 1 na sentimita 80. Siku moja nilikuwa nikisali sala ya magharibi pale mfungwa mmoja mpya alipoletwa kwenye seli yetu. Mfungwa huyo mpya alikuwa ni katika wale Wakomunisti wakereketwa. Aliponiona mimi ninasali na kufahamu kwamba mimi ni mtu wa dini, kuanzia hapo hapo akaanza kunikunjia uso! Kila nilivyojaribu kuingiliana naye sikufanikiwa. Kila wakati alikuwa amekunja uso na wala hakuwa na uchangamfu na mimi. Hata hivyo nilikuja kumwambia maneno yaliyombadilisha kikamilifu. Nilimwambia kwamba Ahmad Sukarno alisema katika mkutano wa Bandung kuwa: "Kilichotuleta sote hapa si dini moja wala itikadi moja wala rangi moja, bali ni matakwa (mahitajio).

Aidha, nikaendelea kumwambia: "Mimi na wewe hapa tuna matakwa mamoja. Tunaishi kwenye seli moja, nyuma ya mlango tunalindwa na mlinzi mmoja, tunasailiwa na mtu mmoja, na tuna mtesaji mmoja anayetusubiri sote wawili - mimi na wewe. Itikadi zetu si moja lakini matakwa yetu ni mamoja." Nikaendelea kumwambia: "Ikiwa kuwa na umoja matakwa katika upeo wa ulimwengu mzima kunaweza kuwa na athari, basi ndani ya seli hii ndogo kunaweza kuwa na athari kubwa zaidi."

Baada ya mazungumzo hayo tukawa marafiki! Kwa hakika ni Ahmad Sukarno ndiye aliyetufanya tuwe marafiki! Leo hii pia hali ni vivyo hivyo. Nchi zetu zina matakwa ya pamoja. Leo hii nchi zote za Kiislamu bila kuacha hata moja ni walengwa wa tamaa na njama mbalimbali. Hii ni katika hali ambayo nchi hizo zina suhula nyingi sana.

 
Mbele >

^