Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Nyumbani kwa Baba wa Rais Chapa
20/02/2008

Katika kipindi changu cha Urais, haikuwahi kumpitikia mtu yeyote akilini mwake - si wao wala si mimi - kwamba labda kwa kuwa hivi sasa mimi nimeshakuwa Rais wa nchi basi ningeifanyia matengenezo nyumba ya marehemu wazazi wangu. Hata pale mmoja wa majirani zetu wa hapa alipopandisha ghorofa ya nyumba yake akawa sasa anaweza kuona mpaka ndani ya ua huu na hivyo kumfanya mama yangu awe hawezi kutembea uani bila kuwa na buibui, baadhi ya jamaa waliniambia: "Mwambie (jirani) asifanye hivyo." Mimi nilimpelekea ujumbe, lakini hakunisikiliza! Mimi sikuwa na njia ya kisheria ya kufanya - yaani hakukuwepo madai yenye nguvu ya kuweza kumbana jirani yetu huyo labda kwa kumwambia kwa mfano punguza urefu wa nyumba kwa mita moja. Katika nchi yetu na mfumo wetu wa utawala, haya ni miongoni mwa mambo yanayopendeza na kutupa faraja sote kwamba vyeo vya kidunia na suhula za kimaada haziwi sababu ya kuwafanya watu kuchanganya mambo yao ya kibinafsi na masuala ya umma na kudhani kwamba lazima wao wawe wanaishi katika hali bora zaidi.
(Aliyasema hayo tarehe 8 Agosti 1995 alipozuru nyumba ya marehemu baba yake huko Mashhad)

 
< Nyuma   Mbele >

^