Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mwambie Imam (Mwanangu) ni Muhanga kwa Ajili Yake! Chapa
20/02/2008

Mama wa mateka mmoja wa vita aliniambia: "Mwanangu alikuwa mateka, na leo imekuja habari kuwa amekufa shahidi. Nenda ukamwambie Imam [Khomeini] kuwa (mwanangu) ‘Ni muhanga kwa ajili yake, wala mimi sihuzuniki.'" Nilipokwenda kwa Imam, nilisahau kumweleza hilo kwanza, baadaye nilipotoka nje nikakumbuka, nikamweleza mmoja wa watu waliokuwepo hapo kwamba mwambieni Imam kuwa kuna kitu kimoja kimebaki cha kumweleza. Imam alikuja hadi nyuma ya mlango wa ua wa ndani wa nyumbani kwake, nami nikaenda kumwona. Wakati nilipomwambia maneno ya yule mama, uso wa Imam ulibadilika na kuonyesha hali ya huzuni huku akitokwa na machozi, kiasi kwamba nilijuta kwa nini nilimweleza maneno yale. Kwa kweli ni jambo la kustaajabisha mno! Sisi tumepoteza roho za mashahidi wote hawa, kwani hili si jambo la mchezo? Wenzi sabini na mbili wa Mapinduzi waliuawa shahidi lakini Imam alisimama imara mithili ya mlima kana kwamba asilani hakikutokea chochote, lakini hivi sasa kutokana na kuuliwa mateka mmoja uso wake umejawa na huzuni huku machozi yakimtoka. Hii imetokana na nini? Kwa kweli sielewi. Kwa kweli mtu anashindwa kabisa kuielezea shakhsia na haiba ya mtu huyu.
(Imenukuliwa katika hotuba aliyotoa tarehe 22 Mei 1990 wakati alipokutana na Kamati ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kutawafu Imam Khomeini)

 
< Nyuma   Mbele >

^