Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Msistaajabu! Chapa
20/02/2008

Mmoja wa viongozi wa mataifa ya Afrika alikuwa ni Ahmad Seko Toure aliyekuwa Rais wa Guinea Conakry. Yeye aliwahi kuja Iran mara kadhaa wakati mimi nilipokuwa Rais. Safari moja alipokuja hapa ilikuwa ni wakati wa vita. Akasema: "Msistaajabishwe na hivi vita mlivyotwishwa navyo. Mojawapo ya mambo ya awali kabisa yanayofanywa dhidi ya taifa linalofanya mapinduzi yoyote yaliyo dhidi ya vyombo vya kikoloni na kibeberu na madola yenye sauti duniani, ni kuchonganishwa na moja ya majirani zake. Hali yenu nyinyi pia inaingia katika kanuni hii. Hivyo msistaajabu!" Kisha akaniambia: "Nyinyi wamekushambulieni kutokea upande mmoja wa mpaka, lakini mimi walinishambulia kutokea pande tano - nilishambuliwa na nchi tano." Kwa vile Guinea Conakry ni nchi ndogo na imepakana na nchi kadhaa, yeye pia kwa vile alikuwa ni mwanamapinduzi na aliingia madarakani kwa kufanya mapinduzi, naye pia alishambuliwa.
(Imenukuliwa kutoka kwenye hotuba aliyotoa tarehe 12 Mei 1998 mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tehran)

 
< Nyuma   Mbele >

^