Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mnaiogopa Marekani?! Chapa
20/02/2008

Mimi na Bwana Hashemi [Rafsanjani] pamoja na mtu mmoja mwengine ambaye sitaki kumtaja jina lake, tuliondoka Tehran na kuelekea Qum kuonana na Imam [Khomeini] ili kumuuliza tuwafanye nini hawa majasusi [wa Marekani] - waendelee kubaki au tusiwaweke tena; hasa kwa vile ndani ya Serikali ya Muda [ya Waziri Mkuu Mahdi Bazargani] yalikuwa yakipigwa makelele ya ajabu kwamba tuwafanye nini majasusi hao! Tulipofika kwa Imam na kumsimulia hali ya mambo ilivyo, ikiwa ni pamoja na kwamba redio mbalimbali zinasema hivi! Marekani nayo inasema vile! Viongozi wa serikali nao wanasema hivi! Imam alitaamali kwa muda kisha akauliza: "Mnaiogopa Marekani?" Tukajibu: "Hapana." Akasema: "Basi endeleeni kuwashikilia!"
Naam, hakika ulikuwa unahisi kwamba mtu huyu hana chembe ya khofu kwa sababu ya uwezo wa kimaada, satua, na nguvu za kidhahiri za kila kitu ilizokuwanazo Marekani. Kutokuwa na khofu kwake na kutoshughulishwa na nguvu za kimaada za adui kulitokana na uwezo na haiba yake binafsi na umakini aliokuwa nao. Kutokuwa na khofu kiumakini ni tofauti na kutokhofu kwa kutojali tu bila kuwa na umakini wala utambuzi wowote. Kwa mfano mtoto mdogo naye anaweza asimwogope mtu mwenye nguvu au mnyama wa hatari; lakini mtu mwenye nguvu naye pia huwa haogopi, isipokuwa tu watu na jamii hukosea katika kupima nguvu zao na nguvu ambazo hawazioni.
(Imenukuliwa katika hotuba yake aliyotoa tarehe 17 Aprili 1999 kwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu)

 
< Nyuma   Mbele >

^