Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kusali Wasisali Lakini Mapanga Wacha Wajipige! Chapa
20/02/2008

Mtu mmoja aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya Urusi ya zamani na eneo la Jamhuri ya Azarbaijan ambalo wakaazi wake ni Mashia, alisimulia haya: "Katika enzi zile ambapo Wakomunisti walikuwa wamelidhibiti eneo la Azarbaijan, walifuta athari zote za Kiislamu katika eneo hilo. Kwa mfano misikiti waliigeuza kuwa maghala, kumbi za mikutano ya kidini na Husainia walizibadilisha ili zitumike kwa mambo mengine, hivyo kutobakisha athari yoyote ya Uislamu, dini au Ushia. Kitu kimoja tu walichokiruhusu kiendelee kuwepo ni kujipiga mapanga wakati wa maombolezo ya Muharram! Amri iliyotolewa na viongozi wa Kikomunisti kwa maafisa walio chini yao ni kwamba Waislamu hawana haki ya kusali, kusali sala za jamaa, kusoma Qur'ani, kufanya maombolezo na shughuli nyingine zozote za kidini, lakini waruhusuni wajipige mapanga!" Kwa nini? Kwa sababu kujipiga mapanga ni kitu ambacho waliweza kukitumia kama wenzo wa propaganda dhidi ya Uislamu kwa ujumla na hasa dhidi ya Ushia! Hivyo baadhi ya wakati maadui hutumia baadhi ya vitu kama hivi dhidi ya dini. Kila pale yanapofanywa mambo ya upuuzi (katika dini) basi jina la dini halisi huharibika pia.

(Imenukuliwa katika hotuba aliyotoa tarehe 21 Machi 1997 katika hadhara ya wananchi wa Mashhad)

 
< Nyuma   Mbele >

^