Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kuishi Pamoja na Wala Watu! Chapa
20/02/2008

....Walikwenda kuwatanasarisha watu ili ukoloni uweze kuingia huko na kufanya kazi yake. Mapadri nao walikuwa wakijua kwamba wanahudumu kwa ajili ya kitu gain - si kwamba walikuwa hawajui - lakini angalia jinsi walivyostahamili na kuvumilia masaibu mbalimbali kwa ajili ya lengo hilo. Masaibu ambayo hayawezi asilani kufidiwa kwa pesa. Kwa mfano, mtu awe tayari kwenda kuishi kwa muda wa miaka saba jirani na sehemu wanayoishi wala watu! Mambo hayo mtu anayasoma kwenye vitabu, anayaona katika baadhi ya ripoti, na yako pia hata kwenye baadhi ya filamu na vitabu vya riwaya. Mimi ninazo habari za masuala hayo na ninajua nini kimetokea katika miaka ya ukoloni.

Hata katika nchi yetu hii alitumwa padri mmoja kutoka nchi moja ya Ulaya akaenda Isfahan na Tehran na maeneo mengine ya nchi. Mhubiri mmoja wa Kikristo aliamua kuja kuishi hapa kwa muda wa miaka mingi na kuvumilia taabu na shida za kuweko mbali na nchi yake huku akitazamwa na watu kwa jicho baya kwamba huyu ni kafiri na najisi. Watu hao walikuja na kuishi hapa kwetu katika kipindi hicho ambapo mambo hayo yalikuwa nyeti mno baina ya watu, katika kipindi cha taasubu na kipindi ambapo watu walikuwa wameshikana barabara na itikadi za kidini. Walikuja na kuishi hapa wakiwa na matumaini kwamba wataweza kuwatanasarisha japo watu wanne; kama walivyokuwa wakifanya huko Afrika walidhani kwa mawazo yao batilifu kuwa wataweza kufanya hapa kwetu pia. Ingawa hawakuweza, lakini waliendelea kubaki kwa miaka na miaka.

Isomeni historia ya [wafalme wa] Qajari. Alikuwepo mtaalamu mmoja wa mambo ya nchi za Mashariki (orientalist) ambaye aliishi hapa Iran kwa miaka mingi na kuandika kitabu cha juzuu mbili kiitwacho Historia ya Iran. Aliishi hapa kwa muda mrefu katika eneo la kusini mwa Khorasan, Birjand na Zabol na maeneo ya hapa pia na kuandika kitabu chake hicho. Someni muone aliyoyanukuu kutoka kwa mapadri wao wenyewe ambao walikuweko hapa.

(Imenukuliwa katika hotuba aliyotoa tarehe 19 Novemba 1991 mbele ya maulamaa wa ofisi ya mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika Masuala ya Ahli Sunna wa [Mkoa wa] Sistan na Baluchistan)

 
< Nyuma   Mbele >

^