Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kana kwamba Hawakuwa Kundi la Wanamapinduzi Chapa
20/02/2008

....Nikaona kuwa kama tulivyotarajia - kwani zaidi ya hilo mtu hawezi kabisa kutarajia - kwamba kundi moja lenye fikra za mrengo wa kushoto wa Kikomunisti limefanya mapinduzi ya kijeshi, au mapambano ya kijeshi msituni au ya kudumu, kisha likatwaa madaraka, hivyo badala ya wale waliokuwa wakiwatawala, wao wenyewe sasa ndio waliokuja madarakani! Kasri ambayo kabla yake alikuwa akiishi humo mtawala wa Kireno aliyekuwa akitawala Msumbiji, ndimo humohumo ambamo Samora Machel, kiongozi mwanamapinduzi wa Msumbiji - ambaye baadaye aliuawa - aliishi! Yeye alinikaribishia na kuniandalia dhifa kwenye kasri hiyohiyo. Nikahisi kwamba hali ya wakati huo haikuwa tofauti na ya kabla yake! Ndani ya kasri mlikuwemo na zulia ambalo nilishughulika kulitizama. [Samora] Akaniambia: "Haya ni katika yale mazulia yaliyosalia tokea enzi za Wareno." Niliona kwamba sio tu alikuwa akiishi ndani ya kasri hiyo kwa taadhima hiyohiyo, lakini pia alikuwa akiishi kwa namna ileile aliyokuwa akiishi mkoloni wa Kireno. Utadhani kana kwamba hawakuwa kundi la wanamapinduzi na lililotokana na wananchi. Na kwa kweli halikuwa la wananchi wala wananchi hawakuwa na sauti kabisa!

Tulipotaka kuingia kwenye ukumbi wa karamu nikaona watu wawili wamesimama kando ya mlango mkubwa unaounganisha ukumbi huo na ukumbi wa kupokelea wageni. Walisimama kama watumwa katika majumba ya kisultani ambapo mtawala wa Kireno alikuwa akiishi. Kwa hakika watu wawili hao wa zama hizo za wakoloni wa Kireno walikuwa watumwa weusi! Lakini hawa wa sasa walikuwa watu weusi tu, hawakuwa watumwa tena, kwa sababu tu mtawala wao alitokana na wao wenyewe! Watu hao wawili ambao walikuwa wamevalia sare maalumu walikuwa wamesimama kama watumwa kwenye kingo mbili za mlango; na walichokuwa wakitakiwa kufanya ni kwamba wakati pale mfalme, yaani huyo kiongozi mwanamapinduzi, na mgeni wake ambaye nilikuwa ni mimi, watakapofika mlangoni wafungue shata mbili hizo za mlango kwa wakati mmoja huku wakionyesha hali maalumu ya unyenyekevu. Hivyo ndivyo walivyofanya. Mimi nilitabasamu huku nikiangalia mandhari hiyo. Kisha huku nikiwa nimeandamana naye [Samora Machel] ambaye alikuwa akionyesha mikogo sawa na ile ya mtawala wa Kireno, tukaingia kwenye ukumbi wa karamu.

(Imenukuliwa katika hotuba aliyotoa tarehe 28 Mei 1990 alipokutana na maimamu wa sala ya Ijumaa wa nchini kote)

 
< Nyuma   Mbele >

^