Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Imam: “Wananchi Wako Pamoja Nanyi” Chapa
20/02/2008

Wakati sisi tulipokwenda huko [katika nchi za kigeni], wananchi walitupokea vizuri, kwa sababu tulikuwa wawakilishi wa nchi hii. Si kwamba sisi twende huko na wananchi wa huko wawe hawana habari, kisha tuseme limetokea tukio kama hili. Hata hivi sasa pia hali iko vivyo hivyo. Wakati nyinyi mnapowasili kwa mara ya kwanza katika hizi nchi ambazo hatuna uwakilishi, na mkabahatika kufika kwenye mijumuiko ya wananchi waliokuwa wanakutazamieni - sizungumzii juu ya yale makundi yaliyo mbali na masuala haya - kama wanachuo, wanafikra na duru za watu wenye msimamo, uchungu na ikhlasi, mtaona kwamba ujumbe huu umeshafika huko kabla yenu. Mimi katika safari nilizofanya katika sehemu mbalimbali na katika vipindi tofauti, nilishuhudia hali hiyo katika nchi zote, ziwe za Kiislamu au zile zisizo na Kiislamu, bali hata kwenye nchi za kikomunisti. Katika kipindi cha Urais wa Jamhuri, nilipotaka kufanya safari katika nchi kadhaa, kabla ya hapo lilizuka tukio kuhusiana nasi ambalo lilienea habari zake duniani kote - tukio ambalo lilipigiwa upatu na propaganda za Kizayuni, Marekani na ustakabari (ubeberu) wa kimataifa. Nilikwenda kuonana na Imam [Khomeini] kwa ajili ya kumuaga na kupata nasaha na miongozo ambayo kwa kawaida alikuwa akinipa kila ninapokwenda safari. Nikamwambia: "Imesadifu kwamba wakati huu wa kukaribia safari yangu, ndio limejiri tukio hili, na serikali za nchi mbalimbali na maadui zetu wameonyesha kuguswa mno na suala hili." Imam akasema: "Ndiyo, lakini mataifa yako pamoja na nyinyi." Kwa kweli hilo nililishuhudia kwa uwazi kabisa kuthibiti maneno hayo katika safari hiyohiyo, kwa namna ambayo isingeweza kuthibitika kwangu hata kama ningetolewa chungu ya hoja.

(Imenukuliwa katika hotuba aliyotoa tarehe 23 Aprili 1991 kwenye kikao na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu pamoja na wawakilishi wa Vitengo vya Kiutamaduni vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nchi za nje)

 
< Nyuma   Mbele >

^