Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Endapo Mtaziendea Nyoyo na Nafsi za Vijana kwa Kutumia Akhlaki na Lugha Nzuri Chapa
20/02/2008

Msikiti ambao mimi nilikuwa nikisali, wakati wa sala za magharibi na isha ulikuwa ukijaa sehemu ya ndani bila kubaki hata nafasi ya kutia mguu. Sehemu ya nje ya msikiti pia watu walikuwa wakisongamana. Asilimia themanini ya watu waliokuwa wakija msikitini humo walikuwa ni tabaka la vijana, kwa sababu tulikuwa tukiwahutubu wao zaidi. Katika miaka hiyo majaketi ya sufi ya ukosi ulioshonwa nje ndani yalikuwa ndiyo fasheni, na vijana wengi waliokuwa watu wa mambo hayo wakivaa nguo hizo. Siku moja, nikamwona kijana mmoja aliyekuwa amevaa nguo hiyo amekaa nyuma yangu katika safu ya kwanza. Mzee mmoja wa kuheshimika katika wafanya biashara aliyekuwa mtu mwenye busara na ambaye mimi binafsi nikifurahi kumwona amekaa katika safu ya mbele, alikuwa ameketi kando ya kijana huyo. Nikamwona amemwelekea kijana huyo na kumnong'oneza kitu sikio, kiasi kwamba kijana yule ghafla akaonyesha kutafirika. Nilimgeukia yule mzee na kumuuliza: "Umemwambia nini?" Lakini badala ya kujibu yeye alijibu yule kijana kwa kusema: "Si kitu." Nilifahamu kwamba yule mzee alimwambia kijana huyo kuwa haifai kukaa safu ya mbele ukiwa umevaa nguo hiyo. Mimi nikamwambia: "Hapana! Inafaa kabisa wewe kukaa hapa hapa wala usitikisike!" Nikamgeukia yule mzee na kumwambia: "Vipi mzee, kwa nini unasema kijana akakae nyuma? Wacha watu waelewe kwamba hata kijana anayevaa nguo ya fasheni ya jaketi la sufi la ukosi wa nje ndani naye pia anaweza kuja kusimama nyuma yetu na kusali sala ya jamaa."
Ndugu zanguni! Ikiwa hatuna fedha na suhula za kisanaa, ikiwa pia kwa sasa hatuna tarjuma ya Qur'ani kwa lugha ya [malenga] Saadi wa zama hizi, lakini tunayo uwezo wa kuwa na akhlaki njema. [Hadithi inasema kwamba:] "Miongoni mwa sifa za muumini ni kuonekana furaha yake katika uso wake, na kubaki huzuni katika moyo wake." Waendeeni vijana hawa na ziendeeni nyoyo zao na nafsi zao kwa akhlaki njema; hapo ndipo tablighi itakapofanyika kwa ufanisi.
(Imenukuliwa katika hotuba aliyotoa tarehe 16 Juni 1997 mbele ya maafisa wa Taasisi ya Tablighi za Kiislamu )

 
Mbele >

^