Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hukumu za Taklidi - Namna Tatu: Ihtiyati, Ijtihadi, Taklidi Chapa
20/02/2008

Swali 1: Je, taklidi ni suala la kiakili tu au lina ushahidi pia wa kisheria?

Jibu 1: Taklidi ina ushahidi wa kisheria na akili inahukumu kwamba mtu asiye na elimu ya hukumu za dini inampasa amfuate mujtahidi mwenye kutimiza sifa (mujtahid jami'u ‘sh-shara'it).

S2: Kwa mtazamo wako, Mheshimiwa, kufanya ihtiyati ni bora au taklidi?

J2: Kwa vile kufanya ihtiyati kunamlazimisha mtu kujua mambo na namna ya ihtiyati, na inamlazimu kutumia wakati zaidi, hivyo, ni vyema kwa mukalafu (mtu aliye na akili na aliyebaleghe) kumkalidi mujtahidi aliyetimiza sifa katika hukumu zake.

S3: Upana wa ihtiyati katika hukumu za dini baina ya fatwa za mafakihi una ukubwa gani? Je, inabidi kuzingatia pia rai za mafakihi waliotangulia?

J3: Makusudio ya ihtiyati katika mambo yanayohusiana nayo ni kuzingatia kila uwezekano wa kifikihi kiasi kwamba mukalafu apate yakini kuwa ametekeleza ipasavyo wajibu wake.

S4: Karibuni hivi binti yangu atatimiza umri wa kuwajibika kisheria na itampasa ajichagulie marjaa taklidi wake, lakini ni vigumu kwake kuelewa suala la taklidi. Tunapaswa kufanya nini kwa ajili yake?

J4: Kama peke yake anashindwa kutambua wajibu wake wa kisheria kuhusu jambo hilo, jukumu lenu ni kumwongoza na kumuelimisha.

S5: Ni jambo maarufu miongoni mwa mafakihi kwamba kuainisha maudhui za hukumu ni jukumu la mukalafu mwenyewe, na jukumu la mujtahidi ni kuainisha hukumu; lakini kwa wakati huohuo kuna mambo mengi ambayo mujtahidi hutoa rai zao katika kuainisha maudhui za hukumu. Je, ni wajibu kufuata rai za mujtahidi katika maudhui pia?

J5: Kuainisha maudhui ni kazi ya mukalafu mwenyewe na si wajibu kumfuata mujtahidi katika kuainisha maudhui, isipokuwa kama atapata yakini katika uaninishaji huo au maudhui yenyewe iwe ni miongoni mwa maudhui ambazo kuzianisha kwake kunahitajia kutolewa hukumu (istinbat).

S6: Je, mtu anayezembea kujifunza hukumu za dini kwa kiwango anachohitaji ni mtenda dhambi?

J6: Kama kutojifunza huko kutamfanya aache wajibu au afanye la haramu, atakuwa ni mtenda dhambi.

S7: Baadhi ya wakati wanapoulizwa watu wenye elimu ndogo ya masuala ya kidini kuhusu marjaa taklidi wao, husema hatujui au husema tunamfuata mujtahidi fulani, lakini hawafanyi juhudi za kusoma Risala (kitabu cha hukumu na fatwa) yake wala hawazifuati fatwa zake. Je, amali za watu kama hao zina hukumu gani?

J7: Kama amali zao zitaafikiana na ihtiyati, au kutabikiana na ukweli (wa mambo) au rai za mujtahidi ambaye wana wajibu wa kumkalidi, basi amali zao ni sahihi.

S8: Kwa vile katika yale masuala ambayo mujtahidi mjuzi zaidi amesema ni ihtiyati wajibu tunaweza kumfuata mujtahidi mjuzi zaidi (mujtahid aalam) wa kabla yake, je tunaweza kumfuata mujtahidi mjuzi zaidi wa kabla ya (huyu wa pili) katika masuala ambayo naye amesema ni ihtiyati wajibu? Na kama fatwa ya mujtahidi wa tatu itakuwa hivyo hivyo je inawezekana kumfuata mjuzi zaidi wa kabla yake? Na hivyo hivyo... Tafadhali tufafanulie suala hilo.

J8: Katika masuala ambayo mujtahidi mjuzi zaidi hajayatolea fatwa, hakuna matatizo kumfuata mujtahidi yeyote katika mas'ala ambayo hakufanya ihtiyati na ameitolea fatwa ya wazi, tab'an inabidi kuchunga utaratibu wa "mjuzi zaidi bora". (al alam fal alam).

 

^