Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Fatima Zahra AS Kilele cha Ubinadamu Chapa
27/04/2008

Leo hii tunazungumza kwa jina la Uislamu na tunafahamu kuwa risala ya Uislamu ndio ujumbe bora kabisa. Kwa hakika tunajifakharisha kwa kuweko wanawake kama nyinyi. Linalofahamika ni kuwa, kila wakati ujumbe au madai yanapokaribia hatua ya utendaji na kutimia ndipo bila shaka thamani na malengo yake huonekana na kudhihiri zaidi. Hivyo basi, kuhusiana na masuala ya wanawake kwa upande mmoja, na masuala ya elimu na utaalamu, kwa upande mwingine, na vilevile huduma kwa wanadamu kwa upande mwingine, tuna madai kwa jina la Uislamu. Madai yetu yamo katika kalibu (fremu) ya mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu

Sisi tunaamini kwamba, katika kila jamii iliyo salama wanawake wanaweza kupata fursa na kila mmoja kwa nafasi yake akafanya hima na bidii kwa ajili ya maendeleo ya kielimu, kijamii , ujenzi na kuwa na nafasi za uongozi hapa duniani. Kwa utaratibu huo basi, hakuna tofauti yoyote iliyoko baina ya mwanamume na mwanamke. Lengo la ya kuumbwa kila binadamu, ni katika yaleyale malengo ya kuumbwa wanadamu wote, yaani afikie daraja ya saada na ukamilifu na kustafidi na fadhila na neema ambazo kama mwanadamu akijitahidi atafanikiwa kuzifikia na hivyo kuweza kustafidi nazo. Hivyo basi, katika hilo hakuna tofauti yoyote baina ya mwanamume na mwanamke. Mfano wake katika daraja ya kwanza kabisa ni Fatima Zahra (alayha 's-salaam) [binti wa Mtukufu Bwana Mtume Muhammad SAW], na katika daraya ya baadayena ni wanawake wakubwa katika historia.

Fatima Zahra AS yupo katika kilele cha ubinadamu na hakuna mwingine aliye juu zaidi kuliko yeye. Tunaona kwamba Mtukufu huyo anajulikana kuwa ni Mama wa Waislamu. Bibi Fatima amefanikiwa kufikia daraja hii ya juu ya utukufu kwa jitihada zake mwenyewe. Hivyo basi, mbele ya Mwenyezi Mungu na kwa mujibu wa mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu, hakuna tofauti yoyote ile baina ya mwanamume na mwanamke. Pengine ni kutokana na hilo ndio maana Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu anapotoa mfano wa waja wema na watu wabaya, hutoa mifano yote miwili hiyo kuhusiana na wanawake. Katika mfano mmoja anamtolea na kumzungumzia mke wa Firauni, na katika mfano mwingine anamzungumzia mke wa Nabii Nuh na Lut: "Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walioamini - mkewe Firauni...." (at-Tahriim, 66:11) Na mkabala wake, kuhusiana na mwanadamu mwenye matendo mabaya, aliyekengeuka na ana anayeelekea upande wa njia isiyo sahihi, Mwenyezi Mungu amewapigia mfano kwa mke wa Nabii Nuh na Lut.

Jibu la Uislamu kuhusiana na ufahamu mbaya na wa kuendelea katika historia ya mwanadamu kuhusiana na nafasi ya mwanamke linapatikana hapa. Swali la kuulizwa hapa ni lipi: Kwa nini Mwenyezi Mungu asingetoa mfano kwa mwanamke mmoja na mwanamume mmoja na badala yake akatoa mifano yote miwili hiyo kwa mwanamke tu hali mwanamume alikuwepo pia?. Katika Qur'ani kila mahala inaposema: "Mwenyezi Mungu amewapigia mfano wali amini..." au "Mwenyezi Mungu amewapigia mfano waliokufuru..." (66:10-12) katika mifano yote miwili inamuhusu mwanamke. Je hiyo haina maana kwamba sisi tunatakiwa kutoa majibu ya mtazamo mbaya na kwa bahati mbaya wenye kuendelea kuhusiana na nafasi ya mwanamke katika historia ya mwanadamu kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu? Hivyo basi Uislamu unataka kusahihisha fikra hizo mbovu na zisizo sahihi kuhusiana na nafasi ya mwanamke (ambazo zilikuwako katika kipindi chote cha historia).


Kwa hakika mimi ninastaajabu mno - isipokuwa katika baadhi ya mambo - kwa nini hali iko hivi ilivyo? Kwa nini daima mwanadamu alikuwa na mtazamo mbaya na usio sahihi kuhusiana na suala la mwanamke na mwanamume na anataka kusimama kupigania kile kinachojulikana kama haki sawa baina ya viumbe wawili hawa? Ukiacha mafundisho ya Manabii, katika mitazamo na uoni mwingine na uchambuzi pamoja na fikra za mwanadamu utapata kuwa, kuna mtazamo mbaya na uoni finyu kuhusiana na nafasi ya mwanamke na mwanaume. Hata katika tamaduni na staarabu kongwe na zilizokuwa na misingi ya muda mrefu (kwa mfano utamaduni wa Kirumi na Kiirani) tunapata kuwa, kuna mitazamo isiyo sahihi kuhusiana na masuala ya wanawake, ambayo hapa mimi sitaki kuyazungumzia kwa urefu, bali nyinyi wenyewe mnapaswa kufanya uhakiki kuhusiana na suala hilo. Inasikitisha kuona kwamba, hii leo pia hali ya dunia iko hivyo hivyo kuhusiana na masuala ya wanawake. Leo hii pia licha ya makelele, madai na nara zote hizi zinazopigwa kuhusiana na kumtetea mwanamke, inasikitisha kuona kwamba hayo yote yanasemwa lakini ufahamu wa kimakosa na fikra potofu kuhusu madai haya ndio mambo yenye nafasi kubwa katika dunia na walimwengu wa leo. Kwa kuwa madola ya Ulaya yamechelewa kuingia katika medani na maudhui hii ukilinganisha na nchi za Kiislamu na mataifa yasiyokuwa ya Ulaya, hivyo, mataifa hayo yamechelewa pia kuzinduka kuhusiana na masuala ya wanawake pamoja na haki zao. Kama mnavyojua, hadi katika miongo ya pili ya karne hii, hakuna mwanamke katika sehemu yoyote ile Ulaya aliyekuwa na haki ya kupiga kura (kutoa maoni). Katika maeneo hayo, kile kinachoelezwa kuwa ni demokrasia kilikuweko katika nchi hizo, lakini mwanamke hakuwa hata na haki ya kutumia mali yake kwa uhuru na matakwa yake kikamilifu. Lakini kuanzia muongo wa pili - yaani mwaka wa 1916 au 18 na kuendeleam - taratibu mataifa ya Ulaya yakakata shauri na kuchukua uamuzi kwamba yampatie mwanamke haki ya kutoa maoni na kutumia mali yake kwa uhuru wake kamili na vilevile kumpatia haki zingine za kijamii kama ilivyo kwa mwanaume. Hivyo basi kwa msingi huo, tunafahamu wazi kwamba mataifa ya Ulaya yamechelewa sana kuamka kutoka usingizini na vilevile yamechelewa mno kufahamu na kutambua kikamifu masuala ya haki za wanawake. Leo hii sasa [Wamagharibi] wanataka kufidia kubaki kwao nyuma kuhusiana na masuala hayo kupitia njia ya propaganda na uwongo. Lakini hata hivyo katika historia ya Ulaya kuna wanawake waliokuwa wakiwa malkia au walioheshimika na kutukuzwa katika jamii. Hata hivyo hilo lilitokea kwa baadhi ya wanawake na kwa baadhi ya familia tu. Kwa hakika ubaguzi huo ulikuweko zama zote. Walikuwepo wanawake walioshika vyeo vikubwa; kwa mfano, walikuwepo wanamke waliokuwa malkia wa nchi fulani. Hata hivyo walifanikiwa kupata cheo hicho kupitia njia ya urithi wa familia zake. Kinyume na hivyo mwanamke hakuwa na haki yoyote katika jamii. Tofauti na mitazamo ya dini za mbinguni na hasa dini ya Kiislamu ambapo mwanamke amepewa haki zake zote kulingana na maumbile yake.

Ndio maana tunaona leo, jinsi ustaarabu wa Magharibi unavyotaka kufidia kubaki kwake nyuma huko kunakolaumiwa kuhusiana na kadhia ya mwanamke na haki anazostahiki kupatiwa mwanamke. Mtazamo wangu katika hili ni kuwa, [Wamagharibi] wamelifanya suala la upande wa kibinadamu kuhusiana na mwanamke katika masuala ya propaganda, siasa na kiuchumi kama ambavyo huko nyuma pia barani Ulaya hali ilikuwa hivyo hivyo. Kwani hata pale mwanamke alipopatiwa haki zake huko, aghalabu alipewa kwa mtazamo huo na msingi huohuo usio sahihi. Wakati ninapozama medani ya kifikra ya ulimwengu na mtazamo wa Uislamu, ninaona kwa uwazi kabisa kwamba jamii ya mwanadamu itaweza kuifahamu kadhia ya mwanamke na uhusiano baina ya mwanamke na mwanamume pale tu itakapoweza kufahamu na kudiriki kikamilifu mtazamo wa Uislamu kuhusiana na suala hilo bila ya kupunguza au kuzidisha, na bila kuonyesha ukali au ubaridi. Kwa hakika, hayo ndio madai yetu kuhusiana na kadhia ya mwanamke ulimwenguni. Sisi hatukubaliani na kile kilichopo na kinachotekelezwa katika staarabu za kimaada za leo, na hatukihesabu wala kukikubali kuwa ni kitu chenye maslahi na manufaa kwa mwanamke na jamii kwa ujumla.

Kwa hakika dini ya Kiislamu inataka kumkuza mwanamke kifikra, kielimu, kijamii na kisiasa - na juu ya yote - kumfikisha katika daraja za juu za kimaanawi; na uwepo wa wanawake katika jamii na familia ya mwanadamu - wakiwa kama kitu kimoja - uwe na faida na matunda mazuri. Mafundisho yote ya Uislamu, likiwemo suala la hijabu, yamesimama juu ya msingi huo. Suala la hijabu halina maana ya kumtenga mwanamke. Endapo mtu atakuwa na mtazamo na ufahamu huo, basi atakuwa amekosea na kuwa na mtazamo potovu na usio sahihi. Masuala ya hijabu kwa mwanamke yanamaanisha kwamba pawepo na kinga ya kuzuia mchanganyiko na maingiliano ya kuchupa mipaka katika jamii baina ya wanawake na wanaume, mchanganyiko ambao unaweza kuwa na madhara kwa jamii, mwanamke na mwanaume - na hasa kwa mwanamke.

Vazi la hijabu si kizuizi wala kikwazo kwa mwanamke kujihusisha na harakati za kisiasa, kijamii na kielimu; na mfano wa wazi ni nyinyi hapa. Pengine baadhi ya watu walikuwa wakistaajabu na hadi sasa wangali wanashangaa kwamba, katika taaluma kuna mwanamke mwenye kiwango cha juu cha elimu, mwanamke ambaye ameheshimu na kutii pamoja na kufuata kikamilifu mafundisho ya Kiislamu likiwemo suala la hijabu na kujistiri. Baadhi ya watu hawakuamini jambo hilo wala hawakuweza kufikiria hilo.

Katika zama za utawala wa kitaghuti walikuwepo watu ambao walikuwa wakilikejeli vazi la hijabu. Katika zama hizo, walikuwepo wanawake wachache na mabinti katika vyuo vikuu ambao walikuwa wakijistiri kwa vazi la hijabu, lakini walikuwa wakitaniwa na kukejeliwa.....

 
< Nyuma   Mbele >

^