Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mwanamke - Askari wa Mstari wa Mbele wa Mapinduzi Chapa
27/04/2008

Mapinduzi yetu haya yameondoa fikra potovu na dhan batili kuhusiana na masuala ya wanawake, na tumeona wazi ni jinsi wanawake walivyokuwa ni maaskari wa mstari wa mbele katika harakati za Mapinduzi - na hii ndio maana halisi ya neno. Huo ndio ukweli halisi wa mambo wala sitii chumvi. Tulishuhudia katika nchi yetu wakati wa harakati za Mapinduzi kwamba wanawake walikuwa maaskari wa mstari wa mbele katika Mapinduzi. Kama wanawake wasingelikubaliana na Mapinduzi na wasingekuwa na imani, nina uhakika kabisa kwamba Mapinduzi haya yasingelitokea na kupata ushindi. Mimi ninaitakidi na kuamini hivi. Kwanza, kama wanawake wasingelikuwepo, basi nusu ya wanapambano wa Mapinduzi wasingelikuwepo kabisa katika uwanja wa mapambano. Pili, kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja, wangewaathiri watoto wao, waume na kaka zao pamoja na mazingira ya nyumba - ambapo mwanamke ana taathira mno ya kiutamaduni katika mazingira ya nyumbani. Hivyo basi, ni kuweko kwao wanawake ndiko kulikopelekea kuvunjwa nguzo za maadui na kuyapeleka mbele mapambano - kwa maana halisi ya neno - hadi yakapata ushindi.

Kwa upande wa medani ya kisiasa pia, tumeona na tunaona wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kuzungumza kwa ufasaha, na wako tayari kukubali kuchukua majukumu katika mfumo wa Kiislamu. Hapana shaka harakati hizi zimo katika kupanuka, na linalopaswa ni kuchukuliwa hatua za kuziendeleza. Katika uwanja wa elimu, nyinyi wenyewe ni mfano wazi na kuna wanawake wengi mithili yenu ambao wamo katika taaluma na fani mbalimbali....


Katika jamii yetu ni jambo la lazima kwa kila mtu - ambaye ana uwezo - kujifunza elimu mbalimbali ambazo zina umuhimu katika kukidhi mahitaji ya jamii. Kwa hakika, leo ni wakati ambapo licha ya kutafuta na kujifunza elimu kuwa ni wajibu wa kidini, ni wajibu wa kijamii pia.

Kutafuta elimu si fursa peke yake kwa ajili ya mtu kutaka kupata kazi fulani yenye kipato kikubwa. Uhakika wa suala hili ni kwamba, watu wanaoweza kusoma na kutafuta elimu wana jukumu na wadhifa wa kufanya hivyo na kubobea katika taaluma fulani. Kusoma na kutafuta elimu na kutopea katika taaluma ya udaktari - kama zilivyo taaluma nyingine - kwa wanaume ni wajibu, lakini kwa wanawake ni wajibu zaidi, kwani wanawake ni wachache katika uwanja wa kazi hizo. Tukitazama madaktari tulionao katika jamii yetu, tunaona kwamba wanawake ni wachache ukiwalinganisha na wanaume katika uwanja huo. Kwa hivyo, kwa mtazamo wa Kiislamu, jambo hilo limeshapatiwa ufumbuzi, na jamii yetu inapaswa kulipeleka mbele suala hilo.

 
< Nyuma   Mbele >

^