Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mitazamo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kuhusu Dini Chapa
13/07/2008
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
Dondoo
Kabla ya jambo lolote, dini ni welewa na uono mpana. Mjumuiko wa utambuzi kuhusu dunia hii, kuhusu mwanaadamu na kuhusu njia na malengo ndio msingi wa dini. Dini inamuhesabu mwanaadamu kuwa ni mhimili wa dunia. Akiwa hana mithili yake, mwanaadamu anaweza kutumia vyema akili yake na kutwaa maeneo yasiyowahi kufikwa.

Dunia ni medani kuu ya kutekelezea majukumu, dhima na risala ya dini. Dini imekuja ili kuufanya uga huu adhimu na uwanda huu wa anuwai za rangi kuwa uchanjaa wa kumuongoza na kufanya juhudi zake mwanaadamu. Dini na dunia ni vitu visivyotenganishika kwa taabiri na maana hiyo ya dunia. Dini ikikosa dunia, haiwezi kupata sehemu nyingine yoyote ya kufikishia na kutekelezea ujumbe wake. Dunia nayo bila ya muhandisi dini na mkono maadili na mjenzi dini huwa dunia bila umaanawi, bila uhakika, bila nyonda na bila roho. Dunia - yaani eneo aishilo mwanaadamu - inapokosa dini hubadilika kuwa uwanja wa sheria za msituni, mazingira ya porini na maisha ya mwituni. Katika uga huo mkubwa, mwanaadamu hana budi kuhisi kuwa na usalma na utulivu ndani yake ili aweze kufungua medani ya kuelekea kwenye ujalili na ukamilifu wake wa kimaanawi.

Kutenganisha dini na dunia kuna maana ya kuyavua umaanawi maisha ya kisiasa na kiuchumi na kuna maana ya kuangamiza uadilifu na umaanawi. Dunia kwa maana ya fursa za maisha ya mwanaadamu, kwa maana ya neema hizi na zile katika uwanda huu mkubwa, kwa maana ya ujamali, matamu, machungu na misiba, ni chombo cha kumpevusha mwanaadamu na kumfikisha kwenye ukamilifu wake. Mambo hayo pia kwa mtazamo wa dini ni nyenzo za kumrahisishia njia binaadamu kuelekea kwenye utukufu na utimilifu, na kudhihiri vipawa ambavyo Mwenyezi Mungu amemzawadia. Dunia yenye maana hiyo haikong'oleki na dini... Hata hivyo dunia ina na maana nyingine. Katika matini za Kiislamu, dunia inatambulishwa pia kwa maana ya ubinafsi na unyimivu na kuwa mateka wa hawaa na matamanio ya kinafsi na kuwafanya wengine kuwa ngawira za tasliti na tamaa binafsi... Katika ndimi za riwaya zetu, dunia ni duni na haiwezi kukaa pamoja na dini.

Nionavyo ni kwamba wanaadamu ndio asili ya mambo yote. Kwa mtazamo wa Kiislamu, hakuna mkinzano baina ya fikra mbili za "Kiini ni Mwenyezi Mungu" na "Kiini ni Mwanaadamu." Kila moja ya fikra hizo inapanda juu ya nyingine. Mojawapo ni kwamba madhali watu hawakushikamana na dini na kuwa na imani nayo, kamwe haiwezekani kutawala serikali ya Kiislamu katika nchi ya watu hao na jamii ya kidini haiwezi kuundika ndani yake. Hivyo kuweko kwa serikali ya dini katika nchi kuna maana ya wakazi wake kuwa watu wa dini, yaani wananchi wameitaka serikali kama hiyo na imetawala.

Lengo la utawala wa dini ya Mwenyezi Mungu ni kufuatilia hali za wanaodhulumiwa na kutekeleza faradhi, hukumu na ada ya Mwenyezi Mungu. Kwani ufanisi umo katika kutekeleza hukumu za dini, ni kwa kuwa uadilifu unategemea kutimilizwa hukumu za dini na ni kwa sababu uhuru na ukombozi wa mwanaadamu umo ndani ya utekelezaji wa hukumu za Mwenyezi Mungu. Wanataka ukombozi na uhuru waupatie wapi? Uko chini ya mwavuli wa hukumu za dini sehemu ambayo inadhamini mahitaji yote ya mwanaadamu.

Mwanaadamu wa leo hatofautiani na mwanaadamu wa miaka elfu au elfu kumi iliyopita katika upande wa mahitaji yake ya kimsingi. Mahitaji ya kimsingi ya mwanaadamu ni kwamba anataka amani na usalama, uhuru, maarifa, maisha yasiyo na tabu, na hapendi kubaguliwa na kudhulumiwa. Mahitaji hayo yanaweza kupatikana tu chini ya baraka na kivuli cha dini.

Mtume msharafu wa Uislamu ametuletea dini tukufu na hivyo kutuwekea mwongozo wa kutekelezea hayo. Alijiegemeza kwenye umaanawi, lakini muda baada ya muda akawapatia watu nyezo za kimaada. Katika baadhi ya sehemu, mwenyewe aliwaelimisha watu moja kwa moja, yaani aliwapa elimu ya maisha na elimu ya kuongoza masuala ya maisha yao. Katika baadhi ya sehemu palipohitajika utaalamu wa mtaalamu wa kitu fulani, aliwaamrisha waende huko kujifunza akiwaambia "enendeni mkatafute elimu, enendeni mkaone vitu vingine."

Karne za kati zilikuwa ni karne za kiza totoro kwa Wazungu lakini kwetu sisi Waislamu zilikuwa karne za nuru, ustaarabu na elimu. Wazungu wanaficha ukweli huo na wanahistoria wa Kimagharibi hawalizungumzii jambo hilo, nasi tumelizoea na kulikubali.

Karne ya 19 ambayo ni ya kunawiri utafiti wa kielimu katika ulimwengu wa Magharibi, inahesabiwa kuwa ni karne ya kujitenga na dini na kuitupa nje ya uchanjaa wa maisha. Fikra hiyo imeacha athari mbaya pia nchini mwetu na msingi mkuu wa Vyuo vyetu Vikuu ukajengwa nje ya dini. Maulamaa wakatoka katika Vyuo Vikuu, na Vyuo Vikuu navyo vikajiweka mbali na maulamaa na vyuo vya kidini.

Wale wanaojidhulisha na kujionyesha kutetea dini wanasema "dini haipaswi kuingilia mambo ya siasa," lakini wamesahau kuwa huo ni ujanja mpya wa propaganda za mabeberu na wakoloni dhidi ya utawala wa Uislamu ambao hawataki kuona dini hiyo ya Allah inapata uhai mpya. Tab-an suala hili la kutenganisha dini na siasa limekuwa likizungumziwa kwa karne nyingi sasa. Awali fikra hiyo ilitoka mikononi mwa madikteta, yaani majabari walioongoza kiimla masuala ya jamii ambao walitaka kuwa na uhuru wa kutenda lolote walilopenda dhidi ya taifa na nchi na ni wazi kwamba hawakupenda kuona sheria za Kiislamu zinatawala na walinganiaji wa sheria za Kiislamu wanaingilia tawala zao. Ndio maana watawala na wafalme wakandamizaji ndio walioukuwa wa mwanzo kuongoza fikra potofu ya kutenganisha dini na siasa.

 

 
< Nyuma   Mbele >

^