Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kuhusu Demokrasia ya Kidini Chapa
13/07/2008
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

Dondoo
Leo hii suala la demokrasia ya kidini ambalo tumeliarifisha na tunalitekeleza humu nchini ni jambo jipya na si kwa sababu tunaonyesha tawi jingine la demokrasia, hapana. Mimi kwa hakika nina mashaka na demokrasia iliyoko duniani leo, kwa sababu chaguzi na uteuzi uliopo unaathiriwa na propaganda ambazo zinadhibitiwa kikamilifu na muki na mabepari.

Msingi wa demokrasia ya kidini unatofautiana na demokrasia ya Magharibi. Demokrasia ya kidini - ambao ndio msingi wa chaguzi zetu uliosimama juu ya haki na takilifu ya mwanaadamu mbele ya Mwenyezi Mungu - si mkataba tu. Watu wote wana haki ya kuchagua na kuainisha mustakbali (wao). Demokrasia ya kweli ni demokrasia ya kidini ambayo hutanguliwa na imani na kuheshimu majukumu ya kidini.

Katika utamaduni wa Kiislamu watu bora zaidi ni wale wanaowanufaisha akthari wenzao. Tofauti na demokrasia za kujilabu na kudanganya watu, demokrasia ya kidini ni mfumo wa kutoa huduma kiikhlasi na ususuani bila masimango na masimbulio na kutekeleza vyema majukumu kwa usafi na unyofu.

Tofauti na propaganda wa mabeberu wa dunia wa "Demokrasia Huria", ni Mfumo wa Kiislamu ulio chini ya bendera ya tauhidi na dini ndio unaoweza kuwatunuku walimwengu demokrasia ya kweli kwa sura ya wazi na kwa lugha nyepesi. Wanachotaka kusema (mabeberu) ni kwamba demokrasia ni yao wao tu. Wanashindwa kuhimili ukweli kwamba Mfumo wa Kiislamu na kidini uliojaa matukufu aali unaweza kutoa misingi madhubuti ya demokrasia. Kigezo chetu sisi hatukukichukua kutoka tawala za Mashariki wala za Magharibi, bali kimetoka ndani ya Uislamu, na kutokana na kuuelewa Uislamu, wananchi wetu wameuchagua Mfumo wa Kiislamu (kuwaongoza).

 
< Nyuma

^