Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mitazamo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Kuhusu Siasa Chapa
13/07/2008
Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

Dondoo
Baadhi ya juhudi za wanaadamu huhusiana na wao binafsi ambapo hiyo ni sehemu ndogo sana ya kazi za mwanaadamu kama vile maisha, umaanawi, hisia na mfungamano binafsi wa mambo hayo yenyewe kwa yenyewe. Amma sehemu kubwa ya kazi za mwanaadamu hutendwa ndani ya jamii na huwashirikisha wote. Kazi hizo ndizo zinazoitwa siasa. Siasa za uchumi, siasa za jamii, siasa za kijeshi, siasa za kiutamaduni, siasa kuhusu wananchi na siasa za kimataifa. Mambo hayo ndiyo yanayochukua sehemu kubwa ya kazi za mwanaadamu katika maisha. Kwa nini tunasema ndiyo yanayochukua sehemu kubwa? Ni kwa sababu siasa hizo humfanya mwanaadamu kuelekea upande maalumu katika kazi zake binafsi. Sehemu kubwa ya idili na jitihada za mwanaadamu ni zile kazi kuu ambazo pia huzipa mwelekeo maalumu shughuli binafsi za watu. Dini huhusika katika nyuga zote mbili, yaani katika uchanjaa wa juhudi za mtu binafsi na uga wa siasa ambao ni mpana na wenye uwanda mkubwa katika maisha ya mwanaadamu.

Hatua ya kwanza iliyochukuliwa na Bwana Mtume Muhammad SAW baada ya Hijra ni kuunda serikali na idara ya kisiasa ya jamii, na kuna dalili na ushahidi mwingi wa kuonyesha mfungamano wa dini na siasa. Mtazamo wa Uislamu asili wa Mtume Muhammad ni kuwa siasa ni sehemu katika dini na haitenganishiki. Uislamu unawataka Waislamu wote kudiriki na kujishughulisha na siasa. Si Uislamu pekee bali dini zote za Mwenyezi Mungu zina siasa, elimu, maisha na masuala ya kijamii katika matini zake. Dini ni mwongozo wa maisha ya mwanaadamu katika nyuga zote ukiwemo uwanda wa siasa.

Fikra ya ukoloni ambayo imezitumbukiza makumi ya nchi na mamilioni ya watu katika mtihani mgumu na shadidi sana kwa miaka mingi, ni miongoni mwa vitu ambavyo vilitokea barani Ulaya baada ya kutenganishwa elimu na umaanawi, siasa na umaanawi na serikali na maadili mema. Vita viwili Vikuu vya Dunia, ukomunisti, kuangamia mfumo bora wa familia, kukithiri uasherati na ufuska wa kijinsia na kufurika ubepari wa kufurutu mipaka yote hayo ni matunda ya kutenganishwa dini na siasa. Hivi tunavyosema kwamba siasa yetu ndiyo hiyo dini yetu na dini yetu ndiyo hiyo siasa yetu - ambapo maneno ya almarhum Mudarris kuhusu suala hilo yalikuwa sawa kabisa na Imam aliyaunga mkono - ni maneno ambayo yako wazi, lakini tujue kwamba sura yake nyingine ni kuwa siasa yetu lazima iwe ya kuweka mbele dini na kujiepusha na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya watu wanaiangalia siasa kwa jicho tu la kama kazi ya kisiasa isiyo na mielekeo yoyote ya kidini. Lengo lao ni kutaka kazi ya kisiasa iende kisiasa. Hayo ni makosa, kwani kazi ya siasa lazima iende kidini. Vitu vyote vilivyoharamishwa na sheria lazima vitiliwe maanani katika shughuli za siasa na viheshimiwe. Tab-an kuna hatari mbili zinaitishia siasa: mojawapo ni ya kutaka kuiweka mbali siasa na maadili bora na kuitoa katika umaanawi na hali ya kiroho yaani kutawalisha ufirauni na ushetani ndani ya siasa, kufanya vishawishi vya nafsi za watu viteke siasa, manufaa ya tabaka la mabwanyenye na mabeberu katika jamii yaitie mikononi siasa na kuiyumbisha huku na huko. Kama maafa hayo yataikumba siasa, basi nyanja zote za jamii ya mwanaadamu nazo hazitasalimika. Hatari nyingine ni siasa kudhibitiwa na watu wenye mitazamo finyu, dhaifu na wenye fikra za kitoto na lijamu ya siasa kutoka mikononi mwa watu madhubuti na kuingia mikononi wa wasiostahiki.


 
< Nyuma

^