Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mitazamo ya Kiongozi Mudhamu Kuhusiana na Mageuzi Chapa
27/07/2008

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu


Kila mfumo unahitaji mageuzi na mabadiliko; marekebisho ni kitu kinachohitajiwa zaidi na kila jamii; sisi pia tunahitajia mabadiliko. Mageuzi maana yake ni kuorodhesha nukta zote hasi na chanya, na kuzibadilisha nukta hasi kuwa chanya. Hayo ndiyo mabadiliko ya kimapinduzi; mabadiliko ya Kiislamu. Bila shaka maadui wa Mfumo na Mapinduzi haya, wanaleta kutokee mageuzi katika muundo wa asili wa mfumo, na mabadiliko kwa mtazamo wa maadui ni kuleta mageuzi ya mfumo na kuutoa katika sura yake ya Jamhuri ya Kiislamu na kuwa mfumo unaotegemea mataifa ya kibeberu. Maana halisi ya mabadiliko, inajumuisha vyombo vyote vya nchi. Hakuna chombo chochote kinachopaswa kujivua na kukosolewa au kudhani hakina doa. Vyombo vyote vya dola vinapaswa kukosolewa kiadilifu na wote wanapaswa kurekebisha nyendo zao kwa kalibu ya kufikia malengo ya Mfumo.
Mabadiliko ni jambo la dharura na la lazima, na inabidi litekelezwe nchini mwetu. Mabadiliko katika nchi yetu hayatokani na kwamba kiongozi fulani ilazimike kufanya marekebisho na kutia viraka hapa na pale kukidhi mahitaji magumu; hapana, mabadiliko ni sehemu ya dhati ya utambulisho wa kimapinduzi na kidini katika Mfumo wetu. Iwapo mabadiliko hayatafanyika katika sura ya kisasa, Mfumo utakuwa mbovu na utakwenda kombo. Mageuzi ni jambo la faradhi.
Mabadiliko, au tuseme mageuzi ya kimapinduzi, Kiislamu na kiimani yanakubaliwa na viongozi, wananchi waumini, na wasomi wote; lakini mabadiliko ya Kimarekani yanapingwa na viongozi wote, wananchi na waumini wa matabaka mbalimbali ya wananchi walio macho. Mabadiliko na mageuzi wanayoyataka Wamerekani yatokee nchini Iran, ni sawa na ufisadi. Mageuzi kwa mtazamo wa Wamarekani yana maana ya kuusambaratisha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kila kinachofuatiliwa na madola hayo ya kibeberu, huwa kwa maslahi yao. Kama wanatoa kaulimbiu za kuunga mkono mageuzi ni uwongo; hao hawajali maana ya uhakika ya neno mabadiliko. Wanapinga maana halisi ya mabadiliko yanayoshuhudiwa humu nchini.
Msingi wa mabadiliko ni kupambana na umasikini na ubaguzi. Mabadiliko ya aina yoyote ile - iwapo kweli ni mabadiliko - basi huzunguka katika mhimili huo. Ufisadi mkubwa katika jamii, ni kuongezeka umasikini na kuwepo ufa mkubwa kati ya masikini na tajiri. Ufisadi mkubwa katika jamii ni ule wa watu kukumbwa na ubadhirifu katika masuala ya kifedha na kiuchumi na kisha hutumia Baitul Maal ya wananchi kwa maslahi yao binafsi na kujaza mali hizo ndani ya mifuko yake. Ufisadi mkubwa ni kuweko ubaguzi katika utekelezaji wa sheria katika jamii na kutojaliwa ustahiki, sifa bora na ustahili wa watu. Ni mambo hayo ya umaskini, ufisadi na ubaguzi ndiyo ambayo nimekuwa nikiyazungumzia mara kwa mara.
Hatua ya kwanza ya mabadiliko, ni kufanyika mageuzi ndani yetu sisi wenyewe; yaani vinogozi wote wa Mfumo wanapaswa kujiosafisha na kujiweka mbali na mienendo, huluka na silika hizo zisizo za Kiislamu. Iwapo hilo litatendwa, hapo ndipo itawezekana kupata maendeleo katika kazi zetu.
Iwapo mabadiliko, ustawi na ubunifu hautafanyika kwa misingi ya matukufu ya Mapinduzi, jamii itakwama. Hiyo ndiyo misingi mikuu. Zingatieni matukufu; na msipotoshwe ubaguzi ili tuweze kusonga mbele kwa nguvu zote katika kalibu hiyo.
Inabidi kutolewe maana halisi ya neno mabadiliko. Kwanza, inabidi maana hiyo iweko wazi kwetu sisi wenyewe tunaotaka mabadiliko na ijulikane wazi tunataka kufanya nini. Pili, maana hiyo wafahamishwe wananchi na tuwaeleze lengo letu ni nini kuhusu mabadiliko, tuondoe mwanya wa kila mtu kuelezea maana ya neno hilo kwa utashi wake tu. Iwapo neno mabadiliko halitapatiwa maana yake sahihi, kuna hatari ya kutawaliwa na vigezo vya kupandikizwa.
Maongozi ya mageuzi yanapaswa kuwa mikononi mwa chombo chenye nguvu na makini. Yaani iwapo kazi tunayoweza kuifanya kwa uzuri na mafanikio katika kipindi cha miaka kumi, tutaka kuifanya kwa kipindi cha miaka miwili tu, tutapata hasara kubwa isiyolipizika.
(Suala jingine) ni kuzingatia na kuchunga muundo wa katiba katika mabadiliko. Tab-an msingi mkuu wa Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ni Uislamu ambao ndio chimbuko la sheria na miundo mbalimbali ya utawala. Muundo wa katiba unapaswa kuchungwa kwa umakini mkubwa. Katiba ni uthibitisho na nguzo yetu kubwa ya kitaifa, kidini na kimapinduzi.
Katika baadhi ya sekta mabadiliko huwa tata na magumu. Kwa mfano katika sekta ya uchumi, kugawa kiuadilifu mapato ya nchi na mithili ya hayo; ni kazi ngumu mno, kuuondoa umasikini na kutoa huduma kwa maeneo yaliyobaki nyuma, kuleta mabadiliko katika muundo wa kiidara yote hayo ni katika mageuzi.

 
< Nyuma   Mbele >

^