Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hija: Hidaya Isiyomalizika na Chemchemu Isiyobubujika Daima Chapa
03/05/2009
(5/7/1989) 
Ifuatayo ni sehemu ya ujumbe wa Hija alioutoa Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mahujaji tarehe 5/7/1989.
 
Mwezi mtukufu wa Dhil Hijja na hazina yake ya milele kwa ajili ya Umma wa Kiislamu umeingia. Hamdi zote ni za Mwenyezi Mungu kutokana na hidaya hii isiyomalizika na chemchemu isiyokauka ambayo kwa kadiri ya hima na utambuzi watakaokuwa nao Waislamu ulimwenguni wanaweza kufaidika nazo (hidaya na chemchemu hiyo) kila mwaka na kujichotea zawadi za kuchukua. Ukubwa na mchanganyiko wa anuai za maslahi na manufaa ambayo Mwenyezi Mungu amejaalia kwa elimu na hekima Yake viwemo kwenye faradhi ya Hija, ni wa kadiri ambayo hakuna faradhi nyingine yoyote katika Uislamu inayoweza kulinganishwa na faradhi hiyo. Kuanzia kwenye dhikri, na uhudhuriaji wa kimaanawi, kujitambua yeye mwenyewe Mwislamu anapokuwa katika faragha yeye na Mola wake, utakasaji wa moyo na kutu za dhambi na mghafala mpaka zile hisia anazopata mtu kwa kujumuika na wenzake, na kuhisi hali ya umoja kati ya Mwislamu mmoja mmoja na umma mzima wa Kiislamu pamoja na kuhizi utukufu wa nafsi kutokana na adhama ya mjumuiko mkubwa wa Waislamu. Aidha kuanzia juhudi zinazofanywa na kila mmoja kwa ajili ya kupata tiba na dawa ya majeraha na magonjwa ya kimaanawi yaani madhambi, mpaka hamu na udadisi pamoja na jitihada za kutaka kuyajua na kuyatibu machungu na majeraha makubwa uliyopata Umma wa Kiislamu, na vilevile kuwa pamoja kihisia na Waislamu wa mataifa mengine kwa taabu na shida zao, Waislamu ambao ni viungo katika mwili mzima wa umma huu mkubwa wa Kiislamu, yote hayo yamejumuishwa kwenye Hija na katika amali na matendo mbalimbali ya faradhi hiyo. Qur'ani imezitaja amali za Hija kuwa ni shaari [nembo na alama]. Hii ina maana kwamba hizo si amali za kuishia kufanywa na mtu binafsi tu kwa ajili ya kutekeleza wajibu wake, bali ni ishara ya kuamsha na kutoa msukumo kwa hisia na utambuzi wa mtu kwa kitu ambacho, amali za Hija ni alama ya kukifikia kitu hicho; kwani nyuma ya alama hizo kuna Tawhidi, yaani kukana nguvu zote ambazo kwa namna moja au nyingine huidhibiti roho na mwili wa mwanadamu na kuviweka chini ya satua yake, na badala yake kukiri utawala na mamlaka mutlaki ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wote; au kwa maelezo ya uwazi zaidi ni kwamba kutawala kwa mfumo wa Kiislamu na sheria za Kiislamu katika maisha ya mtu binafsi na jamii nzima ya Waislamu.

(Ujumbe kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. 5/7/1989)
 
< Nyuma   Mbele >

^