Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hija: Msimu wa Kuchomoza na Kujitokeza Roho ya Maisha ya Kitawhidi Chapa
03/05/2009
Ifuatayo ni sehemu ya ujumbe wa Hija alioutoa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Udhma Khamenei kwa Mahujaji tarehe 4/5/1995.

Kama ulivyo msimu wa machipuo ambao kila pale unapowadia wakati wake wa kila mwaka, huandamana na uchangamfu wa maisha, msimu wa Hija nao ni machipuo ya roho na nyoyo na msimu wa kuchipua na kujitokeza roho ya maisha ya kitawhidi ndani ya moyo wa kila Mwislamu aliyeelekea kwenye makutano (hayo ya Hija) ambapo kila mwaka pale unapowadia msimu huo maalumu ulioainishwa na Mwenyezi Mungu hujaji hurejea kutoka kwenye makutano hayo ambayo ni mithili ya chemchemu kadhaa zenye baraka zinazomwagikia kwenye ardhi ya ulimwengu mzima wa Kiislamu kuupa maisha ya saada ya Kiislamu, na kwa wale ambao wamepata taufiki ya kujikosha kwenye chemchemu hiyo yenye baraka, husafika na kutakasika na vumbi la kinyongo cha madhambi, shirki, kupenda mambo ya kimaada na kuvutiwa na mambo maovu na machafu; na kama watakuwa watu wa kukumbuka na kuzingatia, matunda hayo huwa sababu ya kufuzu na kutengenekewa mtu katika uhai wake wote uliosalia.

Hivi sasa zaidi ya karne kumi nne na ushei zimepita tangu wito wa Ibrahim Khalilullah AS kupitia kinywani mwa Muhammad Mustafa SAW, umekuwa kila mwaka ukitoa mwito kwa kuwaalika wageni wa Nyumba (ya Kaaba) katika msimu huu kwa ajili ya kukutanika kwenye kitovu cha umaanawi na umoja, ili kutufu kwenye kitovu hicho cha Tawhidi pamoja na ule mkondo wa 'uruji ya milele' na kusimama kwa ajili ya sala kwenye Maqam Ibrahim na kuelekea Kaaba ya Kimuhammadi SAW kutekeleza sai ya milele kati ya Safa na Marwa ambayo ni chimbuko la utakasifu wa muumini. Mtu hujitambua jinsi alivyo dhalili na kuelewa adhama na utukufu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu huko Arafa, na kumdhukuru, kuonyesha mapenzi, na kunong'ona Naye Mola asiye na mshirika na kujifunza jinsi ya kuangaziwa na nuru Yake Mola ndani ya jangwa la giza la ndani ya nafsi yake huko Mash'ari na kumlenga kwa mawe shetani mkubwa pamoja na mashetani mengine huko Mina na kuchinja kama ishara ya kudhabihu na kukata hawaa na matamanio yenye kupotosha - na yote hayo yanafanyika katika hali ya ihramu ambayo ni mipaka ya moyo na nafsi ya hujaji mkabala wa matunda yaliyokatazwa ya pepo hiyo (ya Hija), na huyafanya hayo pia kwa kusimama pamoja na Waislamu wengine wa kutoka kila mahala, kila rangi, na wa kila daraja la uwezo wa kimaada na daraja ya kimaanawi, walio na lugha na utamaduni mbalimbali. Kisha baada ya hapo katika hali ya kuashiria kusafika na kila aina ya nongo na uchafu aliopata katika anga iliyochafuka ya maisha ya kimaada na kuathiri roho na moyo wake, hunyoa na kupunguza nywele, na kisha kwa mara nyingine hurejea tena kwenye Nyumba ya Mwenyezi Mungu katika hali ya uchangamfu iliyotokana na kusafika na madhambi na kudhihiri hali ya utambuzi na mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mara hii kutufu, sala na kusai (kwenda baina ya Safa na Marwa) hufanyika katika hali ya upeo na uoni mpana zaidi ya hapo kabla na kutokana na kujipatia akiba ya hazina kubwa ya Tawhidi na umaanawi na hali ya utakasifu, pamoja na azma thabiti ya kupambana na mashetani na nguvu ya kuishinda na kuidhibiti nafsi, huwa tayari sasa kwa ajli ya kurejea katika nchi zao ili kueneza marashi ya Hija katika kila pembe ya dunia.

(Ujumbe kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. 4/5/1995)
 
< Nyuma   Mbele >

^