Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hija: Mjumuiko wa Fursa Chapa
03/05/2009
Sehemu ya ujumbe wa Hija alioutoa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Udhma Khamenei kwa ajili ya mahujaji wa Nyumba tukufu ya Allah tarehe 10/4/1997.

Katika siku hizi kwa mara nyingine Nyumba ya Mwenyezi Mungu ni mwenyeji wa umma mkubwa wa mamilioni ya watu walio na nyoyo zenye hamu na shauku ambao wametoka kila pembe ya dunia na kujumuika pamoja kwenye Kaaba ya matumaini; watu ambao wakiwa wamekusanyika pamoja chini ya kivuli cha ibada ya ikhlasi kwa ajili ya Mola Mpweke, wanajihisi kuwa wao ni umma mmoja. Macho yanayobubujika machozi hupata maliwazokwenye Haram ya Mtume adhimu wa shani SAW, Mawalii wa Mwenyezi Mungu AS na mujahidina wa Uislamu ; (huwa ni marejeo) ya nyoyo zinazoangaziwa na nuru katika anga ya kimaanawi ya Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu na Haram Tukufu ya Mtume Mtukufu (maelfu ya sala na salamu ziwe juu yake na ali zake); mikono (ya watu) iliyoinuliwa juu kwa dua wanaoshtakia shida na haja zao mbele ya Mola Mkwasi; watu walio na maumivu ambao wamesimama mbele ya mlango wa nyumba ya tabibu kutafuta dawa ya kutibu magonjwa sugu yaliyoupata ulimwengu wa Kiislamu, ambao hukutana pamoja nao hapo wenzao walio na maumivu kama yao wa rangi na lugha mbalimbali kutoka kila pembe ya ulimwengu; wale ambao ni madhaifu na walio wapweke hujihisi hapo kuwa ni wenye nguvu na adhama. Siku hizi kwa mara nyingine umma mkubwa wa Kiislamu unaonyesha dhihirisho la haiba na adhama yake mbele ya macho ya watu waliokuwa wameghafilika na adhama hiyo. Dhihirisho hilo huwapa matumaini marafiki na kuwatia khofu na kiwewe maadui.

Mvua za hekima na rehma huwamiminikia wenye kiu na kuzifanya nyoyo zilizokunyaa zinawiri na akili zilizodumaa kupevuka na kutafakari.

Naam! Siku hizi ni siku za sikukuu na siku za makutano kwa ulimwengu wa Kiislamu na Umma wa Kiislamu, na ni mahala pake kwa Waislamu katika kila pembe ya dunia na hasa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kuzitumia saa na lahadha za siku hizo kwa ajili ya ibada na kutafakari, na kwa wale ambao wamepata fursa yenye thamani kubwa ya kwenda Hija na kuzuru warejee katika nchi zao na baraka tele za hekima na rehma za Mwenyezi Mungu na azma na irada mpya kwa ajili ya mustakabali wao na wa Umma wa Kiislamu.

Kati ya faradhi mbalimbali za dini, Hija ndiyo faradhi kubwa kabisa ambayo ndani yake yamejumuishwa pamoja kwa uwazi kabisa mambo yanayomhusu mtu binafsi na jamii kwa jumla.

Kwa upande wa mtu binafsi, lengo ni kujitakasa na kufikia kwenye nuru na utakasifu na kujiweka mbali na mapambo yasiyo na maana ya kimaada, na kukaa katika faragha kwa ajili ya kujijenga kimaanawi na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na kumdhukuru, kunyenyekea na kufanya tawasuli Kwake ili mja aweze kufikia daraja halisi ya kuabudu ambayo - ni kuishika njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyooka kwa ajili ya kuelekea kwenye ukamilifu.

Katika sehemu hii, kuna anuwai za fursa na majaribu kwa kiasi ambacho kila pale mtu atakapoamua kuipita njia hiyo kwa mazingatio, hapana shaka kuwa atapata matunda yenye thamani kubwa; fursa ya ihramu na talbiya (kusema Labeka) , fursa ya kutufu na kusali, fursa ya kwenda (sa'i) na kukazana (harwala) baina ya Safa na Marwa, fursa ya kisimamo cha Arafa na Mash'ari, fursa ya kutupa mawe, kuchinja na fursa ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu - yote hayo ni mithili ya anga iliyojaa roho na uhai ambayo inashuhudiwa katika hali hizo zote.

Mjumuiko wa fursa hizo unaweza kuwa ni kipindi cha mafunzo ya muda mfupi ya kuipa mgongo dunia kunakoruhusiwa katika sheria za kidini, zuhudi, upole, amani na baadhi ya hulka nyingine nzuri.

Kwa upande wa kijamii, kati ya faradhi zote za Kiislamu, Hija haina mfano wake, kwani ni dhihirisho la nguvu, utukufu na umoja wa Umma wa Kiislamu. Hakuna faradhi nyingine yoyote inayowapa Waislamu wote kwa ujumla wao kwa kiwango hiki funzo na mazingatio juu ya masuala ya Umma wa Kiislamu na ulimwengu wa kiislamu, na kuwafanya wakaribie zaidi kiroho na kihakika kwenye ile hali ya kuwa na nguvu, utukufu na umoja baina yao. Kuifuta sehemu hii ya Hija ni sawa na kuwazuilia Waislamu chemchemu ya kheri ambayo haiwezi kupatikana kwa namna nyingine yoyote.

(Ujumbe kwa mnasaba wa kufanyika ibada ya Hija.10/4/1997)
 
< Nyuma   Mbele >

^