Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hija: Neema kwa ajili ya Kujenga na Kutengeneza Dini na Dunia Chapa
03/05/2009
Sehemu ya ujumbe wa Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mahujaji alioutoa tarehe 15/5/1994.

Hii hapa tena Hija, neema kubwa itokayo kwa Mwenyezi Mung. Waislamu kwa ujumla na umma mzima wa Kiislamu unapaswa kutumia fursa hiyo ili kufaidika na Hija, na kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu ameifanya Kaaba - hii Nyumba Tukufu - kuwa tengenezo la (maisha ya) watu." (5:97) Wafaidike watu na Hija kwa ajili ya kujenga na kutengeneza dini na dunia yao. Leo hii dini ya Waislamu inakabiliwa na hatari kutokana na hujuma za kiutamaduni za adui na uenezaji wa ufuska, uchafu wa kimaadili, dhulma na mambo ya kuwatoa watu imani ya dini katika jamii za Kiislamu ambayo aghalabu yao hupangwa na kuratibiwa na madola yanayoupiga vita Uislamu na kwa msaada wa vyombo vyao na vinginevyo vya habari. (Aidha) dunia yao pia inakabiliwa na hatari kutokana na kuongezeka siku baada ya siku udhibiti wa ustakabari (ubeberu) kwa masuala ya nchi za Kiislamu pamoja na kuzidishwa maradufu mbinyo na mashinikizo ya adui kwa kila kundi la watu au serikali ambayo inataka kuzielekeza fikra za Waislamu kwenye suala la kuwa na utawala wa kweli wa Kiislamu na kuwafanya Waislamu wawe huru na wenye nguvu. Tabaan, aliyeko mstari wa mbele katika hujuma hizi za kila upande dhidi ya Uislamu ni Shetani Mkubwa yaani serikali ya Marekani. Kila anayeangalia kwa makini anaweza kuona jinsi serikali hiyo iliyo dhidi ya Uislamu inavyotia mkono wake au ushawishi wake kwa nyuma ya pazia katika masaibu mbalimbali yanayowapata Waislamu.

(Ujumbe kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. 15/5/1994).
 
< Nyuma   Mbele >

^