Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hija: Uwezo wa Kutatua Matatizo Muhimu ya Kisiasa Chapa
03/05/2009
Sehemu ya ujumbe wa Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran alioutoa kwa ajili ya Mahujaji tarehe 15/5/1994.

Kwa yakini haikuwa bure kwa Mtume Mtukufu SAW kuamua kuyachagua siku za Hija kwa ajili ya kutangaza kujibari na washirikina ambayo ni amali halisi ya kisiasa, na ambayo ilihusiana kikamilifu na sera kuu za mfumo na serikali (hiyo) ya kwanza ya Kiislamu, na hivyo akaitangaza amri ya Mwenyezi Mungu iliyokuja ndani ya Qur'ani ya kwamba: "Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume Wake hawana jukumu lolote kwa washirikina. Basi mkitubu itakuwa kheri kwenu, na mkigeuka basi jueni kuwa nyinyi hamumshindi Mwenyezi Mungu. Na wabashirie makafiri kuwa watapata adhabu chungu." (9:3).

Naam, Hija ni faradhi ambayo ina uwezo wa kutatua matatizo makubwa ya kisiasa ya Umma wa Kiislamu. Kwa maana hii kwamba Hija ni faradhi ya kisiasa, sifa ambayo inafahamika kwa uwazi kabisa kutokana na maumbile na sifa za ibada hiyo. Watu wanaopinga hilo na kufanya propaganda dhidi yake, hakika ni kwamba wanapinga kutatuliwa kwa matatizo hayo. Kwa ufupi, ni kwamba Hija ni faradhi ya umma, faradhi ya umoja, faradhi ya nguvu ya Waislamu, faradhi ya kumtengeneza mtu mmojammoja na umma mzima kwa jumla; na katika sentensi moja ni kwamba Hija ni faradhi (kwa ajili ya) dunia na akhera. Wale ambao hawataki kuikubali maana ya kisiasa ya Hija, hakika ni kwamba wanataka kuuweka Uislamu mbali na siasa, na kutenganisha siasa na dini; nara ya kutenganisha dini na siasa ndicho kitu wamekuwa wakikizungumzia kwa miaka kadhaa maadui wanaopinga Uislamu katika jamii za Kiislamu.

(Ujumbe kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. 15/5/1994).
 
< Nyuma   Mbele >

^