Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Siku ya Quds Chapa
07/09/2009

 Udharura wa Kuadhimishwa Siku ya Quds

Maadhimisho ya Siku ya Quds

Athari na Faida za Siku ya Quds

Upinzani dhidi ya Siku ya Quds

Jukumu la Umma wa Kiislamu katika Siku ya Quds

Ulimwengu wa Kiislamu Usighafilike

Siku ya Quds

Udharura wa Kuadhimishwa Siku ya Quds

Inapowadia Siku ya Kimataifa ya Quds kwa mara nyingine huzidi kuwasisitizia na kuwatilia mkazo Waislamu wenye ghera na uchungu na dini yao duniani kuhusu jukumu lao muhimu la kuliunga mkono na kulilinda taifa madhlumu la Palestina.

Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) aliitangaza siku hiyo ili kuamsha hisia za walimwengu kuhusiana na kadhia ya Palestina na ili upinzani na malalamiko yote yaelekezwe upande wa utawala wa Kizayuni. Hii ni kusema kuwa kila mwaka tunashuhudia kuongezeka kwa kiwango kikubwa idadi ya Waislamu wanaodhimisha siku hiyo.

Watu ambao wanapambana vilivyo na Wazayuni ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina licha ya kukabiliwa na matatizo mengi - ambapo wao ndio matumaini pekee ya kuweza kuikomboa Palestina na kufuta utawala ghasibu unaozikalia kwa mabavu ardhi hizo – inabidi wahisi na wajue kuwa wana uungaji mkono mkubwa wa Waislamu wa pembe mbalimbali duniani. Inabidi maandamano kama hayo ya wananchi katika ulimwengu wa Kiislamu yaimarishwe kama tunataka kweli kuwapa moyo na kuwafanya wanamapambano hao wa ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu wahisi kuwa mataifa ya Kiislamu yako pamoja nao. Ubunifu huo wa kuainisha Siku ya Quds uliofanywa na Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) umetokana na fikra na lengo hilo hilo kwani ni jambo lililo wazi kwamba wakati watu wanapojitokeza katika barabara za Tehran kwa mfano kuadhimisha Siku ya Quds haina maana kuwa wakati huo wanakabiliana kwa silaha na Israel.

Juu ya ukurasa

Maadhimisho ya Siku ya Quds

Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuipa umuhimu mkubwa Siku ya Quds. Makundi ya wananchi Waislamu yasiruhusu baadhi ya tawala zao vibaraka kuiangamiza pole pole na hatua kwa hatua Palestina katika anga ya utulivu na ndani ya ukimya bandia ziliojiandalia kwa nia ya kulisahaulisha suala hilo la Palestina. Usaliti wa tawala ambazo zinawakumbatia Wazayuni kwa kuwafanya wahanga Wapalestina inabidi usisahauliwe. Kadhia hiyo si ndogo hata kidogo.

Iadhimisheni Siku ya Quds na ihesabuni kuwa ni siku muhimu na kubwa kwenu. Tunajua vyema kuwa propaganda za kimataifa haziiakisi; ni sawa tu hata kama haziiakisi; lakini kumbukeni kwamba Wapalestina walioko katika jela za Wazayuni zinapowafikia habari za maadhimisho ya siku hiyo wanatwambia kuwa misimamo yenu, kujitokeza kwenu makundi kwa makundi – jambo ambalo linaonyesha nia yenu njema – kunazidi kutupa moyo na kutufanya imara katika mapambano yetu. Watu walioko ndani ya kuta za jela za Wazayuni inabidi wajue kwamba hawako peke yao na hivyo wasichoke kupambana. Wale wanawake na wanaume ambao wanashambuliwa na magenge ya Wazayuni wahuni katika chochoro na mitaa ya Baytul Muqaddas, Ukanda wa Ghaza na katika miji mingine ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu inabidi wahisi na watambue kuwa nyinyi mko pamoja nao ili kwa njia hiyo wazidi kuwa imara katika istikama yao. Tab'an tawala za nchi mbalimbali nazo zina jukumu lake katika jambo hilo.

Juu ya ukurasa

Athari na Faida za Siku ya Quds

Kama ulimwengu wa Kiislamu utaipa Siku ya Kimataifa ya Quds umuhimu wake unaotakiwa na kama watayatumia vyema malalamiko yanayotolewa dhidi ya Wazayuni maghasibu basi Inshaallah wataweza kumshinda adui kwa kiasi kikubwa na kumlazimisha arudi nyuma. Kama kawaida taifa la Iran litajitokeza vilivyo katika Siku ya Kimataifa ya Quds na kuonyesha nini maana ya kuitumia vyema siku hiyo sambamba na kutangaza msimamo wao kuhusu kadhia ya Palestina. Wapalestina wanaokabiliwa na dhuma kubwa wanachojua ni kwamba kuna watu katika pembe mbalimbali za dunia wanaguswa sana na kadhia yao. Inabidi hisia za kuguswa huko zionyeshwe waziwazi. Inabidi mashinikizo dhidi ya Israel yaongezeke. Inabidi Wapalestina walipe uzito wa hali ya juu jukumu la kuibakisha hai kadhia ya Palestina na wapambane vilivyo katika kulifanikisha hilo. Ijapokuwa kuendesha mapambano ni jambo zito, lakini uzito na tabu za kukaa chini ya mashinikizo ya Wazayuni ni kubwa mno kuliko ule wa kuendesha mapambana na kusimama kidete. Iwapo Wapalestina wataendelea kupambana basi watakuwa na mustakbali mzuri, lakini kama watakubali kuishi chini ya mashaka na matatizo ya mashinikizo ya Wazayuni, hakuna siku watakuwa huru na kamwe hawataweza kuwa na maisha mazuri. Ni sawa kwamba hivi sasa Taifa la Waislamu limeamka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, lakini pamoja na hayo mapambano ndani ya ardhi za Palestina inabidi yawe makubwa, yawe ya watu wote, yawe ya kuendelea na yawe yanatoka ndani ya nyoyo za uma wa Kiislamu, na kwamba mataifa mbalimbali ya Kiislamu kote ulimwenguni inabidi yasaidie katika hilo.

Juu ya ukurasa

Upinzani dhidi ya Siku ya Quds

Upinzani dhidi ya Siku ya Kimataifa ya Quds unaoonyeshwa na waungaji mkono rasmi wa Israel na waitifaki wao – ambao ni waungaji mkono wasio rasmi wa Israel – ni upinzani wa ajabu. Wameibunia Siku ya Kimataifa ya Quds mpinzani na wanajaribu kuisahaulisha siku hii iliyotangazwa na Imam Khomeini (MA). Hatujawahi kuona katika ulimwengu wa Kiislamu sehemu yoyote ile ambayo madola makubwa duniani yanaruhusu serikali za kieneo za mataifa hayo ziwashajiishe wananchi wafanye maandamano. Jambo la kusikitisha ni kuwa siasa za madola makubwa ya kibeberu dunia ni kuwa na ushawishi mkubwa katika nchi nyingi za Kiislamu. Hilo ni miongoni mwa bahati mbaya walizopata Waislamu na ulimwengu wa Kiislamu kiujumla. Kwa nini katika Siku ya Quds, tawala za nchi za Kiislamu zisiwahamasishe na kuwashajiisha watu wajitokeze katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds? Kwani kujitokeza wananchi hao kutaziletea madhara gani tawala hizo? Kama kweli tawala hizo zinaguswa na kadhia ya Palestina na zina uchungu nayo, kwa nini basi zinazuia maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina?

Juu ya ukurasa

Jukumu la Umma wa Kiislamu katika Siku ya Quds

Katika madhehebu yote mashuhuri ya Kiislamu, hakuna hitilafu zozote juu ya suala la kukomboa ardhi za Waislamu. Fiqhi zote zinakubaliana juu ya suala hili kwamba wakati kipande cha ardhi ya Kiislamu kinapotekwa na maadui wa Uislamu na maadui hao wa Uislamu wakachukua madaraka ndani yake, watu wote wana jukumu la kupigana jihadi na kufanya juhudi za kukikomboa kipande hicho cha ardhi ya Waislamu kilichotekwa. Hivyo mataifa ya Waislamu popote yalipo duniani yanajua kuwa ni jukumu lao kukomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Tab'an wengi wao hawawezi kufanya lolote, lakini yeyote anayeweza anapaswa kuchukua hatua na kwa hakika Waislamu wanachukua hatua mbalimbali kuhusiana na suala la Palestina. Na ni kwa sababu hiyo hiyo ndio maana Waislamu katika pembe zote za dunia wameipokea vizuri Siku ya Quds ambayo Imam Khomeini aliitangaza kuwa ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka.

Siku ya Quds haiihusu Iran tu bali ni siku ya ulimwengu mzima wa Kiislamu na ndio maana katika kona zote za ulimwengu wa Kiislamu, Waislamu wanajitokeza kuwatetea ndugu zao Wapalestina kwenye siku hiyo. Waislamu katika Siku ya Kimataifa ya Quds huonyesha azma yao thabiti katika kukabiliana na njama na chokochoko za Marekani na Israel katika Palestina madhlumu ambayo mara kwa mara inashuhudia umwagaji mkubwa wa damu.

Juu ya ukurasa

Ulimwengu wa Kiislamu Usighafilike

Wazayuni na mabeberu duniani ndio walioitia Palestina jeraha kongwe lisilopoa na hadi hivi sasa mikono ya wastakbari duniani inazidi kuingia katika mwili wa mfumo wa jamii ya Kiislamu na wa ulimwengu wa Kiislamu siku baada ya siku. Ulimwengu wa Kiislamu haupaswi kujipweteka na kukumbwa na mghafala kuhusu kadhia ya Palestina. Mataifa ya Kiislamu yasilisahau suala la Palestina na yanapaswa kulifanya suala hilo liwe hai daima. Kumbukeni kwamba Marekani, mabeberu na waungaji mkono wengine wakuu wa Wazayuni wanataka kuwalazimisha Waislamu wasiguswe na suala la Palestina na waisahau kadhia hiyo.

Juu ya ukurasa

 
< Nyuma   Mbele >

^