Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Faharasa ya Uistikbari Chapa
14/09/2009

Mlango wa Kwanza: Mafuhumu ya Uistikbari

Mafuhumu ya Ki-Qur'ani ya Uistikari
Mafuhumu ya Uistikbari Katika Utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu
Madola ya Kiistikbari
Dhihirisho la Uistikbari
Msingi wa Uistikbari
Mantiki ya Uistikbari
Mpango wa Uistikbari

Vitendea Kazi vya Uistikbari

   Vyombo vya Habari na Propaganda
   Mpango wa Mazungumzo
   Kutia Fikra ya Kukatisha Tamaa na Shaka
   Kuzusha Hitilafu
   Mpango wa Mashariki ya Kati Kubwa
   Njama za Kitaalamu
   Kuwatumia viongozi wa kidini ndani ya utawala wa Kifalme
   Wenzo wa Kiutamaduni

Nukta Dhaifu za Uistikbari

Mlango wa Pili: Usharura wa Kupambana na Uistikbari

Usharura wa Kupambana na Uistikbari

Hoja za Kupambana na Uistibakri

    Hoja ya Kitaifa
    Hoja ya Kidini

Mapambano Makubwa dhidi ya Uistikbari
Maana ya Kuacha Mapambano dhidi ya Uistikbari
Nara za Mauti kwa Uistikbari Maana Yake ni Nini?
Udharura wa Kuhifadhi Nara na Shaari za Kupambana na Uistkbari

Njia za Kupambana na Uistikbari

   Kurejea Katika Uislamu
   Mafunzo na Malezi
   Umoja wa Kitaifa
   Mshikamano wa Kiislamu
   Himaya ya Serikali kwa Wananchi Wao

Sababu za Uadui wa Uistikbari

   Sababu ya Uistikbari Kuwa na Uadui na Uislamu
   Sababu ya Uistikbari Kuwa na Uadui na Taifa la Iran
   Sababu ya Uadui wa Uistikbari na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
   Sababu ya Uadui wa Uistikbari kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu

Lengo la Mwisho la Uistikbari

Faharasa ya Uistikbari


Mlango wa Kwanza: Mafuhumu ya Uistikbari

Mafuhumu ya Ki-Qur'ani ya Uistikari

Mafuhumu ya Uistikbari, ni mafuhumu ya Ki-Qur'ani na sio kitu ambacho hakina hoja ambacho kimekuja katika utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Mafuhumu ya Uistikbari inawataka na kuwalazimu Waislamu, waumini, mfumo na Mapinduzi ya Kiislamu kupambana na Uistikbari; tena mapambano yenyewe sio kwa ajili ya maslahi ya msimu na ya mbinu; bali mapambano haya yapo kwa sura ya daima na ya kudumu. Dhati ya Mapinduzi ni hii kwamba, madhali Mapinduzi yapo basi kitu kama hiki nacho kitakuwepo pia.

Hii ndio mafuhumu ya Uistikbari katika Qur'ani Tukufu nayo ni asili, mtu, mkusanyiko wa watu fulani au mrengo fulani kujivuna na kujiona kuwa, uko juu ya haki, kutoipigia magoti haki bali kuona nguvu zake kuwa ndicho kigezo cha haki! Muistikbari wa kwanza katika historia ambaye Qur'ani Tukufu inawabainishia wanadamu ni iblisi. Mwenyezi anasema: '' Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri'' al-Baqarah 2:34. Hivyo Iblisi alikuwa muistikbari na mtu wa kwanza kujivuna na kujiona.

Hata hivyo, Uistikbari una maana pana. Inavyoonekana Uistikbari sio ghururi na majivuno. Yamkin tukasema kwamba, akthari ya wakati ghururi huwa ni sifa ya kimoyo na kiroho. Yaani mwanadamu kujiona kuwa yuko juu ya wengine. Lakini Uistikari zaidi ni katika upande wa kivitendo wa ghururi. Yaani ni mtu kuonyesha ghururi na kujiona kuwa ni mbora na yuko juu ya watu wengine, katika muamala wake na watu pia, hufanya jambo kwa namna ambayo ghururi na majivuno hayo huonekana na kudhihiri katika vitendo vyake. Mtu huyo huwadunisha watu wengine, huwatusi na kuwavunjia heshima watu wengine, huingilia mambo ya watu wengine na hujitokeza na kuwa mtu anayewachukulia maamuzi watu wengine.

Juu ya ukurasa

Mafuhumu ya Uistikbari Katika Utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu

Katika utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Uistikbari umepewa jina hilo ule mjumuiko wa madola ambayo kwa kutumia nguvu zake za kisasa, kijeshi, kielimu na kiuchumi na kwa kuchukua ilhamu kutoka katika mtazamo wa kibaguzi kwa aina ya wanadamu, mkusanyiko wa mkubwa wa wanadamu-yaani mataifa, serikali na nchi-na kwa udhibiti wa kikatili na kwa kudhalilisha, hutaka kujipatia faida kwa kutumia mashinikizo na unyonyaji; huingilia kazi na mambo yao na hutia mkono katika utajiri wao; hutumia lugha za vitisho na mabavu dhidi ya serikali zao na huwafanyia dhulma wananchi wake na vile vile huzidharau na kuzivunjia heshima tamaduni na ada zao.

Juu ya ukurasa

Madola ya Kiistikbari

Madola ya Kiistikbari ni yale ambayo uongozi na uendeshaji wa sehemu kubwa ya dunia uko katika uwezo na nguvu zao; Mtandao wa Kimataifa wa Kizayuni, nguvu na mabavu ya Marekani, vyombo vya fedha ambavyo vinatoa himaya na uungaji mkono kwa mfumo huu wa kibeberu ulimwenguni, wote hao wanahesabiwa kuwa ni nguvu za madola ya Kiistikbari.

Juu ya ukurasa

Dhihirisho la Uistikbari

Leo hii katika dunia dhihirisho la Uistikbari-kwa maana ile ile mbaya na ya kuchukiza- ni Marekani, la sivyo si suala la uadui la jamii fulani, taifa fulani na nchi fulani. Kadhia iko hivi, kila taifa lina izza, shakhsia na hadhi yake na haliko tayari izza yake kuchezewa na hivyo kufanywa mwanasesere na nguvu kutoka nje tena kwa kutumia mabavu na hadaa.

Adui yaani ni kile kile kituo cha Uistikbari na ubeberu duniani, ambacho leo dhihirisho lake kubwa la na kimsingi ni Marekani. Hata hivyo, wakati inaposemwa kwamba, Marekani, kinachokusudiwa hapa sio wananchi wa Marekani. Wananchi wa Marekani kama walivyo wananchi wengine duniani wana sifa zile zile na nukta zile zile hasi na chanya. Wananchi wa Iran hawana uadui na wananchi hao. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanauhutubu uongozi unaotawala nchini Marekani ambao nia ya kudhibiti ulimwengu ndio inayoainisha siasa zake. Lengo letu kuhusiana na marekebisho ya << Ubeberu wa Kimarekani >>, ni utawala wa Marekani.

Juu ya ukurasa

Msingi wa Uistikbari

Uistikbari umejengeka juu ya msingi wa dhulma, uonevu na uadui, na utawala wa Marekani ambao unahesabiwa kuwa kile cha Uistikbari, leo hii ndio utawala mbaya kabisa ulimwenguni kwa upande wa Uistikbari. Utawala huu umejenga jengo lake juu ya mantiki hii kwamba, utakabiliana na nchi au serikali yoyote ulimwenguni popote pale ilipo, endapo serikali au utawala huo utakuwa hauko tayari kudhamini maslahi ya Marekani. Je kuna mambo mabaya kama kufru na Uistikbari?! Kuna wakati mtu husema: << mimi katika nyuma yangu nina maslahi na ninalinda maslahi hayo, hivyo musikabilieni nami wala musipambane na mimi >>. Vizuri; haya ni maneno. Lakini hii haina maana kwamba, mtu fulani aje na kuingia katika nyumba ya mtu au aende katika nyumba yake na aanze kumletea usumbufu, amnyang'anye usalama wake na kisha baadaye kama mwenye nyumba atauliza kwa nini unaninyang'anya usalama wangu, amjibu kwa kusema: << wewe umeteketeza maslahi yangu, mimi nina faida na kazi hii na kwa kuwa wewe hukuzingatia faida na maslahi yangu, hivyo ninakabiliana na kupambana na wewe >>. Je kuna dhulma kubwa zaidi ya hii!? Kile ambacho kinashuhudiwa katika uga wa kimataifa kutoka kwa Marekani ni hiki.

Juu ya ukurasa

Mantiki ya Uistikbari

Mantiki ya Uistikbari ni mantiki ya kutumia mabavu, kuua na kutumiwa kusiko kwa kiadilifu nguvu iliyonayo; hivyo wenyewe Uistikbari ndio unaoeneza ugaidi. Leo hii Wamarekani wakitumia jina la vita dhidi ya ugaidi wamekuwa wakiingia katika nchi mbalimbali na hivi ndivyo ambavyo wamekuwa wakiyashinikiza mataifa mengine, huyashambulia kwa mabomu mataifa hayo, na kuwauwa watoto, wanawake, wazee na watu wasio na dhambi wala hatia, mantiki yao ni hii kwamba, tunataka kupambana na ugaidi! Ugaidi ni nini? Kwani ni ghairi ya hii kwamba, ugaidi maana yake ni kwa ajili ya kupeleka mbele malengo yake kwa kutumia mabavu na hatua zisizo za kisheria? Je kazi ambayo inafanywa na Marekani leo huko Iraq, Afghanistan na Pakistan ni ghairi ya hii.

Juu ya ukurasa

Mpango wa Uistikbari

Mipango ya Uistikbari wa ulimwengu dhidi ya taifa la Iran kwa mukhtasari inaishia katika sentensi tatu: Mosi, vita vya kisiokolojia, pili vita vya kiuchumi na tatu kukabiliana na maendeleo na nguvu za kielimu. Uadui wa Uistikbari dhidi ya taifa la Iran unaishia katika mambo haya matatu ya kimsingi.

Nini maana ya vita vya kisaiokolojia? Lengo la vita vya kisaikolojia ni kutisha. Nani anataka kututisha sisi? Taifa ambalo halitishiki; ni mjumuiko mkubwa wa wananchi ambao hautishiki. Wanataka kuwatisha viongozi, shakhsia wa kisiasa na kwa kauli maarufu '' wenye vipawa''. Watu ambao wanawaeza kuhadaika na kupotea, wanataka kuwahadaa na kuwapoteza; wanataka kudhoofisha irada ya wananchi; wabadilishe ufahamu na hali ya wananchi ya kudiriki uhakika wa jamii; hili ndilo lengo la vita vya kisaikolojia.

Vita vya kiuchumi ni vita vingine. Wanataka kulibana kiuchumi taifa la Iran. Wanatishia kwamba, tutakuwekeeni vikwazo. Vikwazo havizwezi kuwa na madhara wala kutoa pigo kwa taifa la Iran. Kwani hadi sasa si walikuwa wameiwekea vikwazo Iran? Taifa la Iran limefanikiwa kupata teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia, maendeleo makubwa ya kielimu na ujenzi mkubwa wa nchi katika kipindi ambacho lilikuwa limwekewa vikwazo. Vikwazo hata katika baadhi ya mazingira huwa ni kwa manufaa ya taifa la Iran; kwani hatua hiyo huwafanya Wairani kuwa na hima na juhudi zaidi.

Kukabiliana na maendeleo ya kielimu: Moja kati ya mifano yake muhimu ni hili suala la teknolojia ya nishati ya nyuklia. Katika matamshi, katika mazungumzo ya kisiasa na yasiyokuwa ya kisiasa, wanasema, Madola ya Magharibi hayakubaliani na suala la Iran kuwa na nguvu ya nishati ya nyuklia; sawa wasikubali hilo. Kwani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeomba idhini kutoka kwa mtu ili iwe na nguvu ya nishati ya nyuklia? Kwani taifa la Iran limeingia katika uga huu kwa idhini ya watu wengine hata wafikie kusema, eti sisi hatukubaliana na hilo?, vizuri musiafiki. Taifa la Iran linaafiki suala hili na lina shauku na hamu ya kumiliki teknolojia hii ya nishati ya nyuklia. Leo hii, moja ya masuala nyeti ya ukoloni, Uistikbari, Marekani na Wazayuni wapangaji wa mikakati ya kueneza ufisadi ulimwenguni ni kwamba, wasiruhusu madola yenye mfumo wa kimapinduzi kuwa na maendeleo ya kielemu. Unyeti huu uko maradufu kwa nchi kama Iran; kwani unyeti na hali waliyonayo ya kuguswa kwao na Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu, hawakuwa na hali hiyo, hawana na hawatokuwa nayo kwa nchi yoyote ile kama ilivyo kwa Iran.

Juu ya ukurasap

Vitendea Kazi vya Uistikbari

Vyombo vya Habari na Propaganda

Vitendea kazi vya Uistikbari wa Ulimwengu ni vyombo vya habari pia. Vyombo vya habari ulimwenguni vina nguvu sana, na viko kwa ajili ya watu wanaovimiliki na vinafanya mambo makubwa mno. Vyombo muhimu vya habari ulimwenguni-iwe ni mashirika ya habari, au iwe ni redio au televisheni, iwe ni magazeti makubwa- ni mali ya matajiri; yaani wale wale watu ambao ni misingi asili ya Uistikbari wa dunia. Katika habari ambazo wanazitangaza duniani, kila kitu hupangwa kwa mujibu wa maslahi na manufaa yao. Mimi ninawakumbusha na kuwataka ndugu wote Waislamu ulimwenguni kwamba, wazipime propaganda za Uistikbari ulimwenguni zinazoendeshwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia mashirika ya habari, magazeti, redio na matamshi rasmi ya wanasiasa na mantiki na kanuni jumla na watambue kwamba, vyombo vyote vya kipropaganda za Uistikbari kinara wao akiwa Marekani, hii leo viko pamoja kwa ajili ya kuendesha propaganda dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mataifa ya Kiislamu na hivyo kuarifisha mambo yanayohusiana na Iran na mataifa ya Kiislamu mbele ya macho ya walimwengu kinyume kabisa na ukweli halisi wa mambo ulivyo. Suala hili lina umuhimu mno.

Juu ya ukurasa

Mpango wa Mazungumzo

Wanasema kuwa: (( Sisi tunataka kuwa na uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu)). Hata hivyo maneno haya ni urongo mtupu; yaani hawataki uhusiano salama; wanataka uhusiano pacha na wa kututwisha mambo; yaani wanataka uhusiano sambamba na Uistikbari; wanataka uhusiano wenye maana ya uhusiano wa Marekani na tawala zilizodidimia na kuporomoka na ambazo ni fisadi. Leo hii serikali ya Marekani haina budi kusema na kutoa matamshi haya. Wale watu wanaodhania kwamba, Jamhuri ya Kiislamu inapaswa kufanya mazungumzo na kinara wa Uistikbari yaani Marekani, imma wanafikra finyu au wanaogopa. Kabla ya Uistikbari kula mkate wake wa ''nguvu na uwezo'' wake, hula kwanza woga na ukaripiaji wake. Kimsingi Uistikbari uko hai kwa kukaripia, kiburi na kumtishia mtu huyu na yule.

Juu ya ukurasa

Kutia Fikra ya Kukatisha Tamaa na Shaka

Maadui wanafanya njama za kuuarifisha mustakabali mbele ya macho ya wananchi kuwa ni kiza na wenye kukatisha tamaa. Kama munaona wakati mwingine baadhi ya watu wanatoa matamshi ya kukatisha tamaa kuhusiana na hali ya kiuchumi na mustakabali wa nchi, fahamuni kwamba, maneno haya asili yake yanatoka kwa Uistikbari. Moja kati ya njama za kipropaganda za adui ni kuzitia shaka fikra na akili za watu kuhusiana na mustakabali. Inasikitisha kwamba, baadhi ya watu wenye roho nyepesi- ambapo huenda kukawa na watu wanaofuatilia mambo kwa ajili ya maslahi yao binafsi- pindi wanapoona nchi inaelekea upande wa ujenzi na ustawi, badala ya kusaidia, kutoa ushirikiano, kurahisisha mambo na kuweka wazi anga ya muonekano ya wananchi, huyaweka kila mambo katika hali ya utata na shaka; kwa dhana hii kwamba, wananchi waingiwe na shaka. Juhudi na uongozi wenye nguvu unapaswa kwenda sambamba na maendeleo. Kwa nini lazima wananchi watiwe shaka kuhusiana na maendeleo? Watu ambao wanazungumza na kutoa maoni, wanapaswa kujichunga wasije wakasema jambo fulani ambalo litakuwa ni kwa maslahi na matakwa ya adui na Uistikbari. Kwani hili ndilo analolitaka adui na ana shauku kuona wananchi wanaingiwa na shaka kuhusiana na juhudi na ujenzi wao wenyewe.

Juu ya ukurasa

Kuzusha Hitilafu

Kila mahala ambapo baina ya waumini na waja wema wa Mwenyezi Mungu kuna umoja, basi hapo pia pana tawhidi na pia Mwenyezi Mungu yupo hapo. Kila mahala ambapo baina ya waumini na waja wema wa Allah pana hitilafu, bila shaka mahala hapo yupo shetani na adui wa Mwenyezi Mungu. Kila mahala ambapo nyinyi mutaona kuna hitilafu, basi chunguzeni, bila ya taabu mutampata shetani mahala hapo, imma shetani atakuwa ndani ya nafsi zetu ambaye ana jina la ''Nafs Ammarah'' yaani nafsi yenye kuamrisha maovu ambaye ni shetani hatari zaidi, basi mutampata. Ndio maana nyuma ya hitilafu zote, imma ni kiburi na kujiona, kutaka jaa na uongozi na kifo cha mwanadamu au ni mashetani wa nje yaani mikono ya adui, Uistikbari na madola dhalimu na ya kidikteta. Basi leo moto haupaswi kuchochewa. Kila mtu awe na itikadi yake na aithibitishe itikadi hiyo, wakati wasemaji wa madhehebu tofauti ya Kiislamu wanapopanda katika mimbari zao wasilete hoja na wasithibitishe madhehebu yao. Hapana, watoe hoja na wathibitishe madhehebu yao. Hata hivyo kuthibitisha itikadi ni mjadala, na kuleta uadui na upande mwingine na kuwa na sauti moja na Uistikbari wa ulimwengu na kutumia nguvu kwa ajili ya vita vya ndani baina ya Waislamu ni nao mjadala mwingine. Lakini katika mlango wa hitilafu za kimakundi baina ya Waislamu, matamshi yake mapya ni kwamba, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuenea fikra za Mapinduzi haya katika maeneo mbalimbali ya Kiislamu, moja kati ya njama za Uistikbari katika kukabiliana na wimbi hili ilikuwa ni kuyatambulisha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa ni harakati ya Kishia kwa maana ya kundi lake- na sio kwa maana ya Kiislamu kwa maana yote- na katika upande mwingine, maadui walifanya njama za kuleta mivutano, undumakuwili baina ya Waislamu wa madhehebu ya Kishia na Kisuni. Tangu awali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuzingatia hila na ujanja huu wa kishetani, daima ilikuwa ikisisitiza juu ya umoja baina ya makundi ya Kiislamu na ilifanya jitihada za kusambaratisha na kukabiliana na hali hii ya kuleta fitina.

Juu ya ukurasa

Mpango wa Mashariki ya Kati Kubwa

Mpango wa Kimarekani wa Mashariki ya Kati Kubwa una njama za kuyachukua mambo yote ambayo yana maslahi na manufaa katika eneo hili na kuyatia katika tumbo lisilojaa la kupenda kujitanua la Uistikbari wa Marekani.

Wao hawaridhishwi na wala hawatosheki na satua na ushawishi walio nao hivi sasa; wanataka udhibiti mutlaki; wanafuatilia kuwa na udhibiti mutlaki kwa dunia yote; likiwemo eneo hili la Mashriki ya Kati ambalo limejaa vyanzo vya utajiri na maliasili na nguvu kazi ya mwanadamu, na nukta nyeti na muhimu mno. Uistikabri wa dunia na madola ya kikoloni tangu awali hadi leo wamekuwa wakiutumia utawala ghasibu wa Israel kama wenzo wa mashinikizo kwa tawala za Kiarabu na kisha za Kiislamu katika eneo hili na wameuweka utawala huo kama jambia lenye sumu kwa ajili ya kupambana na Ulimwengu wa Kiislamu; na leo shetani mkubwa (Marekani) amemshika mkono huyu mbwa aliyepata mafunzo.

Hivyo basi, si jambo la kustaajabisha kwamba, ukiukaji wa mara kwa mara wa sheria za kimataifa, ukiukaji wa kuendelea wa haki za binadamu- tena kwa maafa makubwa kabisa- uvamizi wa mara kwa mara dhidi ya nchi jirani, operesheni za kigaidi na utekaji nyara wa wazi, kutayarisha silaha za atomiki kunakoongezeka na mfano wa hayo- ambapo kila mtu katika nchi yoyote ulimwenguni ambaye hatakuwa na uhusiano wa umiliki wa Raia au madola mengine makubwa, huhesabiwa kuwa tukio kubwa- awakubali Wazayuni na asiyakasirishe na wala asiwe tishio kubwa kwa kanali za Uistikbari wa dunia, husuasan shetani mkubwa (Marekani).

Juu ya ukurasa

Njama za Kitaalamu

Uistikbari wa dunia una wataalamu na wanafikra ambao hukaa na kuchunguza na kisha kuandaa mafaili kuhusiana na mataifa, fikra, na madhehebu tofauti na kisha mafaili yote hayo yaliyowekwa katika vituo vyao vya kiutafiti, kiutamaduni, kijasusi na kisiasa huyazungumzia katika hatua mbili na kuyafanyia kazi mpya ya utafiti. Hii kwamba, huko Israel kunafanyika semina yenye anuani isemayo (( Kuufahamu Uislamu na Ushia nchini Iran)) ni kwa maana hii na katika uwanja huu huu. Katika maeneo mengi duniani kumekuwa kukifanyika semina na vikao vya utafiti ambavyo vinaandaliwa na ulimwengu wa Magharibi, matajiri na Uistikbari na kutolewa fikra mbalimbali kwa ajili ya kuutazama upya Uislamu. Kwa ujudi wake wote Uistikbari hutumia fikra katika kujiendesha na hufanya harakati kwa fikra kamili na kuongoza matukio ya dunia ili usalimike; kwani unafahamu kwamba, kama hautokaa chini na kufikiria kuhusu mustakabali na kama hautakuwa na takwimu basi utapata pigo. Vyombo bora na vya hali ya juu kabisa vya kifikra vipo mikononi mwa Uistikbari.

Juu ya ukurasa

Kuwatumia viongozi wa kidini ndani ya utawala wa Kifalme

Katika jamii ambazo kutokomeza hali ya usafi na utakasifu ya viongozi wa dini lilikuwa ni jambo lisilowezekana, wahusika walikuwa wakifanya jitihada ili tabakala hili liwe na mfungamano na nguvu na tawala chafu na za dhulma. Viongozi wa kidini wanaofungamana na tawala ambao katika matamshi yote haya ya Imam mpendwa ambapo anawataja kwa ubaya na kwa chuki, kwa hakika wameufanyia khiyana na usaliti sana Uislamu. Imam Sajjad AS alimwambia mmoja wa watu mashuhuri katika zama zake kwamba: (( Ninaona umeiandaa shingo yako na kuifanya mhimili wa madhalimu, ili wao kwa kukutumia wewe wawafanyie dhulma watu)). Yule alimu ambaye anatumiwa na vyombo vya ufisadi kuhalilisha dhulma yao ni hatari kuliko vyombo hivyo. Kiongozi wa dini ambaye atafanya mambo kwa ajili ya malengo ya Uistikabri ni mtu mbaya kabisa; kwani mtu huyo kidhahiri huonekana mtu wa haki lakini katika batini yake ni mwenye kuneza batili.

Juu ya ukurasa

Wenzo wa Kiutamaduni

Hivi sasa kuna mapambano ya kifikra, kiutamaduni na kisiasa. Kila mtu ambaye ataweza kuwa na udhibiti katika medani hiyo ya vita na mapambano, azifahamu na kuzielewa habari, awe na udhibiti wa kifikra na kutupia jicho medani, kwake yeye kutakuwa hakuna shaka kwamba, sasa adui analeta mashinikizo zaidi kupitia masuala ya kiutamduni.

Mashinikizo hayo nayo si madogo, maadui wamekuwa wakiwanunua na kuwapa fedha waandishi, wanautamaduni wa dini na nyoyo zenye dhamira mbovu ambazo zimeathirika na ufisadi wa Uistikbari-iwe wengi wao wako nje ya nchi au hawa wachache walioko hapa ndani- ambao hufanya mambo kwa ajili ya malengo ya Kiistikbari, na hivyo hutumia kalamu zao kuandika, hutunga tungo za mashairi, hufanya kazi na kufanya kazi kwa ajili ya kupeleka mbele malengo ya Kiistikbari.

Juu ya ukurasa

Nukta Dhaifu za Uistikbari

Leo hii duniani kuna mambo yanayokinzana. Kwa mtazamo wa mataifa ya Kiislamu, mataifa ya Mashariki ya Kati-mataifa ya Asia, mataifa ya Afrika, Mataifa ya Amerika ya Latini na mataifa ya Mashariki ya Kati-kuhusiana na taifa la Iran ni kuwa, Iran ni taifa shujaa, linalotetea haki na uadilifu na ambalo limesimama kukabiliana na utumiaji mabavu wa madola ya kbeberu na Kiistikbari; mataifa hayo, yanalitambua taifa la Iran namna hii na kwa sifa hizi. Mataifa hayo, yanalisifu na kulipongeza taifa la Iran kwa misimamo yake hii. Lakini taifa hili hili la Iran na mfumo huu huu wa Jamhuri ya Kiislamu ambao unasifiwa kwa sifa kemkemu na kupongezwa kiasi hiki na mataifa hayo, kwa mtazamo wa madola yenye nguvu na yanayotumia mabavu, taifa hili linatuhumiwa kwamba, linakiuka haki za binadamu, madola hayo yanalituhumu taifa hili kwamba, linahatarisha na kuondoa amani na usalama wa dunia, linatuhumiwa kwamba, linaunga mkono ugaidi! Hii ni hali ya ukinzani na mgongano; ni mgongano baina ya mtazamo wa mataifa na matakwa ya madola ya kibeberu ulimwenguni.

Mgongano huu, unatishia mfumo wa kibeberu duniani. Madola haya yanazidi kuwa mbali na mataifa mengine siku baada ya siku; jambo hili limeleta tundu na upenyo mbaya katika jengo la demokrasia ya kiliberali ya Magharibi na tundu na upenyo huu utazidi kuongezeka siku baada ya siku. Hatimaye propaganda za Kiistikbari zitaweza kwa muda fulani kuficha uhakika wa mambo; lakini ukweli wa mambo ni kuwa haiwezi kuficha haki milele. Mataifa yamekuwa yakiamka na kuwa na mwamko siku baada ya siku; Rais wa Iran anasafiri na kuelekea katika nchi mbalimbali barani Asia, Afrika na katika nchi za Amerika ya Kusini, mataifa hayo hupiga nara za kumpongeza, huandamana kumuunga mkono, huonyesha kuwa wanamuunga mkono; kwa upande wake naye Rais wa Marekani husafiri na kuelekea katika nchi za Amerika ya Kusini- yaani ua uliowazi wa Marekani- lakini wananchi wa nchi hizo huchoma moto bendera ya Mrekani kwa mnasaba wa safari ya Rais wa Marekani katika nchi hizo; hii ina maana ya kulegalega kwa misingi ya demokrasia ya kiliberali ambayo leo ulimwengu wa Magharibi ukiongozwa na Marekani unadai kubeba bendera yake. Mgongano katika matakwa yao, shauku ya wananchi na mambo wanayoyashuhudia wananchi yamekuwa yakiongezeka siku baada ya siku. Wanapiga debe kuhusu demokrasia, haki za binadamu, usalama wa dunia na mapambano dhidi ya ugaidi, lakini batini yao ya ushari na uadui inaonyesha juu ya kupenda kwao vita; inaonyesha juu ya kukiuka na kukanyaga haki za mataifa; inaonyesha juu ya hamu, shauku na malengo yao ya siri kuhusiana na vyanzo vya nishati ulimwenguni; mataifa yanaona mambo haya.

Siku baada ya siku, heshima ya demokrasia ya kiliberali, na heshima ya Marekani-ambayo ni kinara wa demokrasia ya kiliberali- kwa mtazamo wa mataifa ulimwenguni hadhi na heshima imekuwa ikipungua na inazidi kupungua zaidi. Mkabala na hilo, hadhi na heshima ya Iran ya Kiislamu imekuwa ikiongezeka kila siku.

Kuna siku viongozi wa Uistikbari ulimwenguni walikuwa wakidhani kwamba, hakuna kitu kilichobaki katika Uislamu. Kwa maji machafu yenye kueneza hawaa na matamanio ya nafsi ambayo walikuwa wameyamwaga duniani walikuwa wakidhani kwamba, hakutabaki kitu baina ya Waislamu kuanzia mafundisho ya Kiislamu, moyo wa Kiislamu, ghera ya Kiislamu, usafi wa Kiislamu hadi hamu na shauku ya Kiislamu; lakini baadaye wakafahamu kwamba, wamekosea. Kwanza, kunyanyuliwa na kutundikwa kwa bendera yenye nguvu ya Kiislamu katika taifa kubwa la Iran na baina ya taifa hili lenye hadhi na sharafu na lenye fakhari; na pili ni kujitokeza mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu wote wa Kiislamu, ni mambo ambayo yaliwafanya wazinduke kutoka katika mghafala na kufahamu kwamba, Uislamu ni hakika yenye kung'ara, yenye nguvu na imara. Hivyo wanapambana nao. Leo ulimwengu wa Kiislamu na mataifa ya Kiislamu yamediriki hakika hii. Ndio maana nyinyi munaona taarifa ambazo wao wanazo zinawaambia na kuwaeleza kwamba, Marekani, Uzayuni, Uistikbari na viongozi wake wanachukiwa katika nchi za Kiislamu.

Juu ya ukurasa

Mlango wa Pili: Usharura wa Kupambana na Uistikbari

 

Usharura wa Kupambana na Uistikbari

Mapambano dhidi ya Uistikbari- ambapo leo pia dhihirisho la Uistikbari ni serikali na utawala wa Marekani- ni sehemu ya dhati ya Mapinduzi haya na ni sehemu ya kazi na matakwa ya asili na ya kimsingi ya taifa hili. Endapo taifa hili litaacha kuendesha mapambano dhidi ya Uistikbari maana yake ni hii kwamba, watakuwa wamekubali kuingiliwa katika mambo yao na wageni, kukubali kudhalilishwa na kuruhusu hali mbaya ya vitisho iliyokuwako hapa nchini kabla ya Mapinduzi! Wananchi wote wa Iran wana hisia hii na wana udiriki huu kuhusiana na suala la kupambana na Uistikbari.

Juu ya ukurasa

Hoja za Kupambana na Uistibakri

Hoja ya Kitaifa

Kwa nini wananchi wa Iran walisimama kupambana na Uistikbari na kwa nini Uistikbari ni mbaya? Munapaswa kuzingatia kwamba, hisia ya kwanza ambayo taifa fulani linakuwa nayo mkabala na roho na ada ya Kiistikbari, sio hisia ya kidini; bali ni hisia ya ghera ya kitaifa; hisia ya utambulisho na hisia ya uwepo; kwani Uistikbari umeingia katika nchi na kuwa na udhibiti kwa nchi hiyo na umekuwa ukikana utambulisho wa taifa hilo. Unapora vyanzo vya utajiri vya taifa hilo, unaingilia mambo ya kisiasa au nchi hiyo; lakini yote hayo ni sehemu tu ya kukana kwao utambulisho wa taifa hilo. Uistikbari awali unapoingia hausemi kwamba, tunakuja ili tuje tukane utambulisho wenu wa kitaifa; hawaji kwa namna hii; bali huingia katika nchi nyingine kwa visingizio tofauti. Wanapokuwa tayari sasa wamekwishaingia, kile kitu ambacho wanakilenga na kukifanya kuwa ni shabaha yao ni utambulisho wa kitaifa. Yaani utamaduni, itikadi, dini, irada, kujitawala, utawala, uchumi na kuchukua vitu vyote kutoka kwa taifa lile na kuvishikilia mkononi mwake; yaani kitu kile kile ambacho kilitokea nchini Iran kabla ya Mapinduzi. Hii ni hisia ambayo mataifa huwa nayo mkabala na Uistikbari; hivyo basi mataifa ambayo hata hayana dini, hata sio mataifa ya Waislamu, leo hii- sio siku ile; wakati ule mtu alikuwa hathubutu hata kidogo kusimama mkabala na Marekani; taifa la Iran ndilo lililofungua njia hii- kwa kadiri yanavyoweza yanasimama na kukabiliana na Marekani.

Juu ya ukurasa

Hoja ya Kidini

Hatua ya taifa la Iran ya kukabiliana na Uistikbari ina msingi na chimbuko la dini. Neno Uistikbari, kujiona na kujikweza ni mkabala na kudhoofika na mustadhaafu katika Qur'ani. Wakati taifa la Iran liliposimama likiwa na roho na moyo huu mkabala na Marekani na vyombo vya ufisadi vinavyofungamana na Marekani, lilikuwa na kinga na himaya kubwa ya itikadi na imani ya kidini nyuma yake na ndio maana likafanikiwa na kusonga mbele katika uwanja huu. Hii leo bendera ya mapambano dhidi ya maadui wa Uislamu iko mikononi mwa wafuasi wa Ahl al-Bayt AS; iko mikononi mwa taifa hili shujaa ambalo haliogopi nguvu yoyote ile isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu. Hii leo taifa la Iran liko hivi. Hii leo haya mambo ambayo ni nguvu muhimu ya Uistikbari na nguvu ambazo leo duniani ni kama kiumbe anayetisha kwa tawala, shakhsia, wanafikra, wanautamaduni, kwa taifa la Iran ni mambo ambayo hayana thamani wala umuhimu wowote.

Juu ya ukurasa

Mapambano Makubwa dhidi ya Uistikbari

Mapambano makubwa kabisa dhidi ya Uistikbati na mashetani ni mtu kutosalimu amri mbele ya matakwa yao. Leo taifa la Iran linayo haya mapambano makubwa na hii njia ambayo iko mbele yetu ametufungulia Imam Khomeini (Quddisa Sirruh) na taifa la Iran limesonga mbele katika njia hii na limefanya harakati na Alhamdulilahi limefikia katika izza na heshima; na leo pia linaendelea mbele na njia ile ile kwa nguvu na uimara kamili.

Juu ya ukurasa

Maana ya Kuacha Mapambano dhidi ya Uistikbari

Mapambano dhidi ya Uistikbari- ambapo leo pia dhihirisho la Uistikbari ni serikali na utawala wa Marekani- ni sehemu ya dhati ya Mapinduzi haya na ni sehemu ya kazi na matakwa ya asili nay a kimsingi ya taifa hili. Endapo taifa hili litaacha kuendesha mapambano dhidi ya Uistikbari maana yake ni hii kwamba, wananchi wa taifa hili watakuwa wamekubali kuingiliwa katika mambo yao na wageni, kukubali kudhalilisha na hivyo kuruhusu hali mbaya ya vitisho iliyokuwako hapa nchini kabla ya Mapinduzi! Wananchi wote wa Iran wana hisia hii na wana udiriki huu kuhusiana na suala la kupambana na Uistikbari.

Juu ya ukurasa

Nara za Mauti kwa Uistikbari Maana Yake ni Nini?

Pindi taifa la Iran linaposema (( Mauti kwa Uistikbari)) watu wasije wakadhani kwamba, maana yake ni hii kwamba, taifa la Iran limesimama kidete ili liuangushe kila utawala wa kila nchi ambao sio wa Kiislamu au nchi ambayo ni ya Kiislamu lakiini Iran haikubali Uislamu wake na ipigane nayo vita. La hasha! Hali halisi ya mambo haiko hivi! Kile ambacho ni muhimu kwa ajili ya Uislamu na utawala wa Kiislamu ni kupambana na dhulma na kukabiliana na madhalimu na uadui: Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwamba: '' Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.'' Al-Mumtahinah 60:09, kimsingi kadhia iko hivi. Watu ambao wanasimama kupinga hakika na uadilifu na wanakubaliana na dhulma na uonevu, ni hapo ambapo hali ya dhulma hujitokeza na pia kujitokeza hali ya kumili upande wa haki- kwa kiwango kile kile ambacho kinamili upande wa haki- na kupingana na hali hiyo ya dhulma na uonevu.

Juu ya ukurasa

Udharura wa Kuhifadhi Nara na Shaari za Kupambana na Uistkbari

Taifa la Iran linapaswa kuhifadhi nara na shaari za kupambana na Uistikbari kama bendera na mwenge. Kwa nini? Kwani kama bendera hii iliyotundikwa haitohifadhiwa, na hii nara na shaari kupotea, taifa pia litapotea njia. Kwa sababu uadui wa yule adui uko wazi na haujajificha kwa watu wa basari na adui kwa uwazi pia licha ya kuwa uadui wake uko wazi, lakini angali anatumia mbinu kwa ajili ya kuhadaa. Aghalabu ya mataifa yamehadaika na tawala ambazo zilifanya makosa, walikosea hapa kwamba, hawakuzitambua vizuri mbinu na mikakati ya adui. Kama mbinu na mikakati ya adui haitofahamika na kutambuliwa na mapambano dhidi ya uadui ambao unataka kuliangamiza taifa fulani la kimapinduzi utasahauliwa, ni jambo lililo wazi kwamba, taifa hilo litakwenda ile njia ambayo adui anaipenda na kuitaka; yaani njia ya kuangamia, njia ya kubomoka na njia ya ufisadi.

Juu ya ukurasa

Njia za Kupambana na Uistikbari

Kurejea Katika Uislamu

Ufumbuzi na tiba ya machungu yote na kushindwa kote mataifa ya Kiislamu ni kurejea katika Uislamu na maisha katika mfumo wa Kiislamu na chini ya kivuli cha sheria na hukumu za Kiislamu. Hiki ndicho kile ambacho kitawarejeshea Waislamu izza na nguvu na kuwafanya wawe na neema kubwa ya usalama na ustawi na ndio kitu ambacho kitabadilisha mustakabali mchungu na wa madhila ambao wapangaji wa Uistikbari wameuandalia umma wa Kiislamu.

Uistikbari na kanali za kipropaganda zinazofungamana nazo, wana matarajio kwamba, matumaini ya Waislamu na kuwa kwao na mtazamo mzuri yatafifia na kubadilika na kisha kuwa na hali ya kukata tamaa na mtazamo mbaya na katika hilo hakuna kitu kitakachokuwa bora na chenye taathira kwa ajili ya malengo haya ghairi ya kuyaonyesha Mapinduzi ya Kiislamu kuwa yako katika mkwamo na kwamba, wananchi wa Iran wako njia panda na wameshindwa kufikia malengo yao na hivyo kuonyesha kwamba, Iran ya Kiislamu inakabailiwa na matatizo na hivyo imelazimika kuiacha njia ya Uislamu halisi wa Bwana Mtume Muhammad SAW na njia ya wazi ya Imam Khomeini (Quddisa Sirruh) mwanzilishi na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Juu ya ukurasa

Mafunzo na Malezi

Suala la utamaduni, mafunzo na malezi ni jambo la kwanza katika Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika muda mrefu hakuna kitu chenye umuhimu kama mafunzo na malezi. Nafasi ya mwalimu na mlezi katika jamii ya Kiirani ni nafasi ya kwanza kabisa. Kwa hakika ngome ya mapambano na kufru, dhulma na Uistikbari wa ulimwengu na mabavu ya mashetani wa kisiasa ulimwenguni ni hii madrasa, mafunzo, malezi na utamaduni. Wanafunzi wadogo ambao wapo katika vyombo vya utamaduni vya nchi, ni mtaji bora kabisa na akiba yenye thamani kwa mustakabali wa nchi. Tambueni thamani ya mafunzo, malezi, mwalimu na ngome ya utamaduni. Vijana na vijana wadogo wanaoinukia wanapaswa kutambua thamani ya masomo, kujifunza na kujitengeneza.

Juu ya ukurasa

Umoja wa Kitaifa

Yule mtu ambaye anataka kusimama kwa ajili ya kupambana na Uistikbari na kutoa pigo kwa adui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hivyo kuleta furaha katika nyoyo za waja wa Mwenyezi Mungu na kuzisononesha nyoyo za maadui, anapaswa kufanya jitihada ili mfungamano, mapenzi, huruma na hali ya kuamianiana baina ya wananchi na viongozi wa nchi iongezeke na kuwa imara na madhubuti siku baada ya siku. Kila mtu ambaye atafanya kinyume cha hili, atakuwa amefanya jambo katika fremu ya malengo ya Uistikbari.

Juu ya ukurasa

Mshikamano wa Kiislamu

Ni katika pembe gani ya ulimwengu ambapo Waislamu hawajadhurika kwa namna fulani na ubaya wa Uistikbari wa dunia na vyombo vya ubeberu ulimwenguni na hata kuwekewa mashinikizo?! Tiba ni nini ghairi ya Waislamu wenyewe kusimama kidete; tiba ni nini ghairi ya Waislamu wenyewe kuwa na mshikamano baina yao; tiba ni nini ghairi ya kuweko umoja baina ya Waislamu; ufumbuzi ni upi isipokuwa jamii za Kiislamu kuwa na mwamko na kutumia nguvu kazi kubwa ya Uisalamu iliyoko katika pembe tofauti ulimwenguni?

Juu ya ukurasa

Himaya ya Serikali kwa Wananchi Wao

Nguvu kubwa ambayo iko mikononi mwa Marais wa nchi za Kiislamu; na nguvu hiyo ni wananchi wa mataifa ya Kiislamu. Kwa kujikinga na nguvu hii isiyoshindwa, nchi za Kiislamu zinaweza kusimama mkabala na Marekani ambayo leo inaongoza kambi iliyo dhidi ya Uislamu yaani ''Kambi ya Uistikbari'' na hivyo kutetea haki za wananchi wake na za wananchi wa mataifa ya Kiislamu yaliyodhulumiwa. Uislamu ni dhamana bora kabisa kwa ajili ya taifa fulani kuendesha maisha na katika kivuli hicho, wananchi wanaweza kudhuku na kuonja ladha ya uhuru, kuwa na mamlaka ya kujitawala kikamilifu na kunufaika na hayo, na vile vile imani ya wananchi wa nchi zenye Waislamu, ndio kinga bora kabisa kwa ajili ya kufikia malengo haya. Matarajio ya watu kutoka kwa nchi za Kiislamu ni kuwa badala ya kuwa na uoga usio na maana kwa Uislamu –ambapo Marekani na viongozi wengine wa Uistikbari wanafanya njama kubwa kulionyesha hilo baina ya viongozi wa Kiislamu- watazame kioo hiki cha Mwenyezi Mungu kwa jicho la uongofu kwa ajili ya mataifa yao na kuuchukulia kuwa ni mfungamano baina ya mataifa ya Kiislamu, yaani na wautumie Uislamu kwa ajili ya kujiandalia uwanja wa nguvu, izza na heshima. Huu wenyewe ni wenzo wenye nguvu mno kwa ajili ya kupata himaya ya wananchi na serikali ambayo itakuwa na uungaji mkono wa wananchi haiwezi kuogopa chochote.

Juu ya ukurasa

Sababu za Uadui wa Uistikbari

Sababu ya Uistikbari Kuwa na Uadui na Uislamu

Mvutano uliopo leo baina ya Uistikbari na Uislamu ni juu ya nini? Hii leo Uistikbari unakabiliana na Uislamu; kwani ni wenyewe ambao umelisema hilo wazi pasina kificho. Rais wa Marekani ndiye aliyeleta jina la (( Vita vya Msalaba)). Wahubiri na watangazaji wa Uistikbari daima na kwa kutumia mbinu za kuudhi wamekuwa wakiendesha propaganda dhidi ya Uislamu; wanazalisha filamu, wanatengeneza michezo ya Kompyuta, wanaendesha propaganda, wanaandika makala yote hayo dhidi ya Uislamu. Kwa nini wanapingana na Uislamu?! Hili ndilo suali kubwa na la kimsingi. Wao wenyewe wanasema kwamba, sisi tunapingana na Uislamu; kwani Uislamu unaleta vita, muaji na chuki! Kwa uwazi huu wanasema uongo na kueneza tuhuma katika anga ya fikra za waliowengi ulimwenguni.

Lakini ukweli wa mambo ni kuwa, leo Uistikbari ndio ambao unajaza na kueneza chuki ulimwenguni. Ni Wamarekani ndio ambao wanaleta vita Ulimwenguni. Ni wao ndio ambao wanakanyaga haki za mataifa mengine na kukiuka mipaka yao na kufanya mashambulio ya kijeshi dhidi ya ardhi za mataifa mengine. Huwandaa na kisha kuwachukua wanajeshi wao na kuwasafirisha kwa maelfu ya kilomita na kuwapeleka katika nchi hii na nchi ile, katika mipaka hii na kuvamia taifa lile. Katika historia ya miaka mia moja iliyopita vile vile kama nyinyi mutatazama, mutaona kuwa, vita vingi zaidi vilianzishwa na Wamagharibi. Watu wa Ulaya walianzisha Vita Viwili Vikuu vya Dunia. Vita vingi barani Asia, Afrika na Amerika ya Latini vilianzishwa na tawala hizi hizi za matajiri nchini Marekani. Ni wao ndio ambao wanaleta na kueneza chuki baina ya mataifa tofauti. Uislamu uko mbali na tuhuma hizi. Ugomvi sio juu ya hili-wanasema uongo hawa- ugomvi ni kuhusiana na hili kwamba, Uislamu unayaita mataifa ya Kiislamu katika mamlaka ya kujitawala na kujiamulia mambo yao; unayaita mataifa na kuyataka yazingatie izza na heshima yao; unayafundisha mataifa ya Kiislamu yatambue haki zake; yataka haki hizi na yasimame kukabiliana na wavamizi kwa ajili ya kutetea haki zao hizo. Uistikbari unapingana na huku kusimama kidete, unapingana na huku kujihami na kujitetea na unapingana na haya maarifa na utambuzi. Hivyo basi, ugomvi na mvutano baina ya Uislamu na Uistikbari uko katika hili.

Juu ya ukurasa

Sababu ya Uistikbari Kuwa na Uadui na Taifa la Iran

Iran ya Kiislamu, Iran ya Imam Khomeini (Quddisa Sirruh) , Iran ya Mapinduzi ya Kiislamu ni kituo na mhimili wa harakati kubwa ya Waislamu Ulimwenguni, na ndio maana imekuwa mhimili wa uadui. Hili badala ya kulihuzunisha na kulisononesha taifa la Iran, linalifurahisha; na badala ya kuwa Uirani uingiwe na woga na wahaka, unapata matumaini zaidi; kwani hili linaonyesha kwamba, taifa la Iran lina nguvu na lingali linahesabiwa kuwa ni tishio kwa maslahi ya Uistikbari, manufaa ya wezi na waporaji wa mali za mataifa. Uadui wa Uistikbari unalifanya taifa la Iran lizidi kuwa na uhakika zaidi kwamba, njia ambayo taifa hili limeichagua katika harakati ya kupeleka mbele mapinduzi, ujenzI wa nchi na jamii ni sahihi na ilikuwa na mafanikio. Kama taifa hili katika harakati yake dhidi ya manufaa ya maadui wa wanadamu na katika maslahi ya Mapinduzi na nchi ingekuwa sio njia sahihi, basi adui asingEkwa na uadui kiasi hiki na taifa hili la Kiislamu na asingeliandama taifa hili namna hii.

Juu ya ukurasa

Sababu ya Uadui wa Uistikbari na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Kwa nini kila mahala ambako kuna ishara za wito wa Imam Khomeini (Quddisa Sirruh) kuna nyoyo zenye kuvutiwa na harakati hiyo na kuchukuliwa hatua katika uwanja huo kwa ajili ya kufikiwa lengo hilo, Uistikbari huwa na mtazamo ulio dhidi ya mahala hapo? Sababu ya uadui huu unatokana na mambo kadhaa ambayo tutayabainisha hapa: Mosi, ni suala la kutotenganika dini na siasa na kutotenganika dini katika medani ya maisha. Kivitendo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imethibitisha na kuonyesha kwamba, dini ina nafasi katika medani ya maisha ya wanadamu na dini tukufu ya Kiislamu haikuja ili kuwafanya wanadamu wakae katika maeneo ya ibada na kujishughulisha tu na ibada. La hasha, kwani medani ya maisha ya mwanadamu, medani ya kisiasa na masuala muhimu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yapo katika sheria na hukumu takatifu za Kiislamu.

Suala la Pili, kutoathirika na matakwa na madola makubwa ya kibeberu. Kwa mtazamo wa Marekani na Waistikbari ni kuwa, moja kati ya uhaini mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni huu kwamba, haiathiriki na mtazamo wa Marekani na mfano wa Marekani kuhusiana na masuala mbalimbali Ulimwenguni. Mfano wadhiha ni suala la Palestina. Wamarekani na waitifaki wake, wametoa mashinikizo makubwa kwa nchi za Kiarabu na nchi nyingi za Kiislamu ili zifumbie macho na kulipuuza suala la Palestina; na la kusitikitisha ni kwamba, nchi nyingi zimeathirika na mashinikizo haya na zimeyakubali. Lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweka wazi na kubainisha msimamo wake katika sentensi moja ambapo, watu wote wa insafu na uadilifu duniani wanalikubali hilo. Sentensi hiyo ni hii kwamba, (( Palestina ni mali ya wananchi wa Palestina )).

Sababu nyingine ya uadui wa Uistikbari kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni maudhui hii kwamba: utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel unapaswa kufungasha virago vyake. Wayahudi wanaweza kubaki Palestina, lakini serikali katika ardhi za Palestina ni mali ya taifa la Palestina na Wapalestina na wao kama ilivyo kwa nchi nyingine wanaweza kumuacha hapo mtu yoyote wanayemtaka.

Suala jingine ni himaya na uungaji mkono wa kimaanawi na kisiasa wa Iran kwa watu wote ambao wako katika njia ya Uislamu na wanaofanya jitihada kwa ajili ya kuanzisha utawala wa Kiislamu. Kila mtu popote pale alipo Ulimwenguni, ambaye anafanya juhudi kwa ajili ya izza ya Uislamu, Iran humuunga mkono na kumpa himaya ya kimaanawi na kisiasa mtu huyo. Kuyatetea mataifa ya Kiislamu ni jambo ambalo linamchukiza adui.

Miongoni mwa masuala mengine ambayo adui wa Uistikbari humfanya akasirike na Jamhuri ya Kiislamu ni hili kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga utwishaji wa kiutamaduni wa Magharibi kwa mataifa ya Kiislamu. Utamaduni wa Kimagharibi ni utamaduni ambao sambamba na kuwa na nukta chanya una mambo hasi pia. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini juu ya suala la mabadilishano ya kiutamaduni. Taifa kama Iran au mataifa mengine ya Kiislamu yanapaswa kutazama tamaduni nyingine ulimwenguni na kile ambacho kwao wao kina faida na kinawafaa wakichukue na kustafidi nacho. Na kile ambacho si cha lazima na hakina faida kwao, basi wanapaswa kukitupilia mbali. Uistikbari wa dunia una uadui na chuki ya ndani kabisa ya ujudi wake kwa Uislamu na Mapinduzi. Na madhali taifa fulani halijaacha na kutupilia mbali misingi na dini yake na halijasilimu amri, basi maadui hawatoridhika. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwamba: ''Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao.'' Al-Baqarah 2: 120

Hivyo basi chuki ya Uistikbari ni kwa sababu ya itikadi, moyo wa kutaka kujitawala na nara ya (( ni kuikataa mashariki na kuikataa magharibi)) na kushikamana kikamilifu kwa wananchi wa Iran na dini tukufu ya Kiislamu. Chuki ya Uistikbari si yenye kwisha; pamoja na chuki ya hali ya juu ya adui dhidi ya taifa la Iran, lakini taifa hili kwa uwezo na kudura ya Mwenyezi Mungu lina matumaini kwamba, Inshallah litaweza kufikia malengo ya Kimwenyezi Mungu katika medani zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na hivyo kumlazimisha adui kurejea nyuma.

Juu ya ukurasa

Sababu ya Uadui wa Uistikbari kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu

Baada ya kujitokeza mfumo wa Kiislamu nchini Iran ukiwa na msingi imara wa imani ya wananchi, ulimwengu ukawa umepata changamoto kubwa. Kwa nini? Kwa sababu mfumo huu kikawaida ungepigana na na kukabiliana na manyangumi hatari wa mifumo ya Kiistikbari duniani. Maana ya mapigano haya haikuwa hii kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataka kuingia vitani na Marekani, Uingereza au nchi fulani.

Wakati nchi fulani ya Kiislamu ikiwa na nafasi nyeti ya kijiografia na kwa kuwa na utamaduni mkubwa inapojitokeza katika medani na kutoa fikra na iko tayari kujitolea na kupigana kwa ajili ya kuhakikisha inabakia, dalili na ishara za mafanikio katika sura yake zinaonekana, ni jambo la kawaida kwamba, nchi hiyo huwa tishio kwa maslahi ya Uistikbari katika eneo lote la Mashariki ya Kati. Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndio maana vyombo vya Uistikbari wakati huo- ambapo katika upande mmoja ilikuweko kambi ya uliberali na katika upande mwingine Usoshalisti- kambi hizo zilianza kukabiliana na Mapinduzi ya Kiislamu. La kustaajabisha lilikuwa hili kwamba, wao wenyewe walikuwa wakihitalifiana kwa asilimia tisini katika mambo mengi, yaani walikuwa na hitilafu nyingi baina yao, lakini wakiwa na shabaha ya kuzima mwenge huu wa Mapinduzi na mmea huu ulioota (Mapinduzi ya Kiislamu) waliungana na kuweka kando hitilafu zao!

Juu ya ukurasa

Lengo la Mwisho la Uistikbari

Hii leo lengo kuu la Marekani na Uistikbari ni kuhakikisha kwamba, wanayalazimisha Mapinduzi, Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran ili liachane na misimamo yake. Itangaze kwamba, inaachana na mitazamo yake na inaachana na mitazamo ya Imam Khomeini (Quddisa Sirruh). Maadui wamekuwa wakitumia nguvu zao zote katika hili. Kwa nini? Ni kwa sababu adui anaona ujumbe na risala ya Imam Khomeini (Quddisa Sirruh) imeyaamsha mataifa ya Kiislamu. Yatazameni mataifa tofauti ulimwenguni na hususan Mataifa ya Kiislamu! Mutaona ni kwa kiasi gani yameathirika na risala ya Imam Khomeini! Uistikbari umefahamu kwamba, kama unataka kuyanyamazisha mataifa hayo ni kuyapotosha kutoka katika njia sahihi na yeye kukaa nafasi hiyo, njia pekee ni kuyafanya mataifa hayo yaone kwamba, Iran ya Kiislamu na Iran ya Imam Khomeini imeachana na njia yake ili watu wote wakate tamaa na hivyo kurejea katika njia yao. Uistikbari umelifahamu hili na ndio maana juhudi zake zote zipo katika hili. Uistikbari ukitumia nyenzo na suhula zake zote hii leo unapanga njama na mikakati ya kuifuta Jamhuri ya Kiislamu na kwa hakika huku sio kutia chumvi. Hili ndilo lengo la mwisho la adui. Hata hivyo maadui wamekuwa wakifanya mambo yao kisiasa, na kwa mipango ambayo imeratibiwa hatua kwa hatua.

Hatua ya kwanza ni kuitenganisha Jamhuri ya Kiislamui na malengo yake matukufu. Hatua ya pili ni kuitenganisha na nguvu yake (wananchi) yenye hamasa, vugu vugu na taasubi. Hatua ya tatu ni kuhakikisha kwamba, wanaleta pengo baina ya kamati hii ya utawala, baina ya serikali hii na viongozi hawa pamoja na matabaka ya wananchi. Hatua ya nne ni kuwaleta mabaradhuli, apige kelele na kuwapatia fedha mabaradhuli na majambazi ili wafanye kitu, kama viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu watakuwa katika mghafala watakuwa ni wenye kulegeza kamba na wasiwe wazingatiaji, hatua hizi nne zitapigwa na kufikiwa katika kipindi cha muda mfupi tu. Lakini kama viongozi watakuwa wako macho, watakuwa wazingatiaji na kama hawatokuwa katika mghafala, basi hatua yake ya kwanza tu miongoni mwa hatua hizi nne, haiJuu ya ukurasaigwa na kufikiwa hata katika kipindi cha karne moja.

Juu ya ukurasa

 
< Nyuma   Mbele >

^