Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu Kuhusu Haki za binaadamu Chapa
15/09/2009

Faslu ya Kwanza: Haki za Binaadamu katika Uislamu

Vigezo vya Haki za Binaadamu katika Uislamu
Misingi ya Haki za Binaadamu katika Utawala wa Kiislamu
Uislamu Ndio Unaodhamini Haki za Binaadamu

Nafasi ya Mwanamke na Haki za Binaadamu katika Uislamu

   Haki za Kisiasa za Mwanamke katika Uislamu
   Nafasi ya Mwanamke katika Jamii
   Kudhulumiwa Mwanamke katika Familia
   Suala la Kimsingi la Wanawake
   Uadilifu katika Hakizi za Binaadamu baina ya Mwanamme na Mwanamke

Upinzani wa Nchi za Magharibi Dhidi ya Uislamu kwa Madai ya ya Kutetea Haki za Binaadamu
Kutumia Nguvu na Kupinga Utumiaji Nguvu

Faslu ya Pili: Haki za Binaadamu katika Nchi za Magharibi

Faili Jeusi la Magharibi katika Suala la Haki za Binaadamu
Kutafuta Maslahi kwa Jina la Haki za Binaadamu
Mwanamke kwa Mtazamo wa Magharibi
Mambo Yanayothaminiwa katika Jamii ya Marekani
Uongo wa Madai ya Kutetea Haki za Binaadamu
Ulaya Mvunjaji Mkuu wa Haki za Binaadamu
Haki za Binaadamu kwa Mtazamo wa Uingereza

Faslu ya Tatu:Iran na Haki za Binaadamu

Haki za Binaadamu katika Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu

Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Jamhuri ya Kiislamu

   Haja ya Kuelimishwa Wananchi
   Vyombo vya Habari katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
   Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Mfumo wa Kibepari
   Sharti la Kuongezeka Idadi ya Vyombo vya Habari
   Jukumu Kuu la Vyombo vya Habari katika Utawala wa Kiislamu
   Haja ya Kusimamiwa Vyombo vya Habari

Kutochukua Misimamo ya Pupa ya Kisiasa katika Masuala ya Haki za Binaadamu
Kulindwa Haki za Binaadamu nchini Iran na Ulaya na Kinyume Chake

Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu Kuhusu Haki za binaadamu


Faslu ya Kwanza: Haki za Binaadamu katika Uislamu

Vigezo vya Haki za Binaadamu katika Uislamu

Dini tukufu ya Kiislamu, ni dini inayolinda na kupigania haki za binaadamu na matukufu ya Kiislamu, ni dini ya kueneza kuhurumiana na kupendana, ni dini ya kuleta na kudumisha udugu baina ya binaadamu na ni dini ambayo kigezo chake katika suala zima la haki za kijamii ni maneno yasemayo: "Hauwezi kutukuka uma ambao dhaifu ndani yake hapati haki yake kutoka kwa mwenye nguvu." Yaani haiwezi kupata maendeleo wala heshima jamii yoyote ile ambayo ndani yake mtu dhaifu asiye na uwezo hawezi kupata haki yake kirahisi kutoka kwa wenye nguvu. Huo ndio ujumbe wa Uislamu, na kwamba jamii ambayo watu wote wanapata haki zao sawa ndiyo jamii inayotakiwa na Uislamu. Leo hii ni ujumbe huo ndio unaoyavutia mataifa mbalimbali duniani. Lakini cha kujiuliza ni katika sehemu gani duniani leo hii inayoongozwa kwa mfumo huo? Ni demokrasia gani, ni fikra gani za kiliberali na ni haki gani za kibinaadamu zinazodaiwa kuweko leo hii zinazotekeleza jambo hilo? Leo hii mambo yote yanakwenda kinyume kabisa na jambo hilo.

Juu ya ukurasa

Misingi ya Haki za Binaadamu katika Utawala wa Kiislamu

Fikra ambayo inaonyeshwa leo hii na Jamhuri ya Kiislamu kwa walimwengu ni fikra mpya kabisa yenye misingi yake katika dini. Dunia, fikra na aidiliolojia za kimaada zilikuwa zimezoea kutenganisha mambo ya kisasa na fikra za kidini na kimaanawi na kujaribu kuwakinaisha watu waamini kwamba mambo hayo yanakinzana. Kitu chochote kinachohusiana na dini na umaanawi – kiwe cha Kiislamu au kisiwe cha Kiislamu – kilihesabiwa kuwa kimepitwa na wakati na ni kitu kinachorejesha nyuma maendeleo. Kila kitu walichosema ni kipya na cha kisasa, walikusudia kwamba kitu hicho lazima kiwe kinakinzana na kinapingana na dini na umaanawi. Huo ni ufahamu ghalati wa dini. Lakini leo hii hali inaonekana kinyume kabisa. Uadilifu wa kijamii unaoonyeshwa na Jamhuri ya Kiislamu na haki za binaadamu zinazofafanuliwa kwa njia nyepesi kabisa na Uislamu ni bora mno kuliko zile zinazoonyeshwa na demokrasia iliyozoeleka duniani leo. Uadilifu wa kijamii katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umepiga hatua kubwa ikilinganishwa na maeneo mengine duniani yanayodai kulinda na kutetea uadilifu wa kijamii. Haki za binaadamu na uhuru wa mtu binafsi nchini Iran umepiga hatua kubwa mno ikilinganishwa na zile nchi zinazodai zimeendelea kidemokrasia, na jambo hilo walimwengu wanaliona waziwazi.

Juu ya ukurasa

Uislamu Ndio Unaodhamini Haki za Binaadamu

Katika suala zima la demokrasia na haki za binaadamu ulimwengu wa Kiislamu hauna haja na nuskha iliyovurugwa ya Magharibi na ambayo inakiukwa mara kwa mara na watungaji wake. Demokrasia na haki za binaadamu ni miongoni mwa mambo yaliyopewa kipaumbele na umuhimu wa hali ya juu katika mafundisho ya Kiislamu. Uislamu ni mlinzi wa heshima na haki za binaadamu na ni mdhamini wa maadili bora na akhlaki njema. Uislamu ni dini ambayo wakati wote inalingania utulivu na amani. Kwa kweli ni uongo mbaya kabisa na ni ukosefu wa uadilifu kudai kuwa Uislamu unapinga haki za binaadamu, haki za raia na maisha ya salama katika jamii. Jambo hilo linatumiwa na wanaoshambulia hivyo Uislamu kwa ajili ya kuhalalisha dhulma na ukandamizaji wao dhidi ya mataifa ya Kiislamu.

Amirul Muuminin Ali (AS) alimwandikia Malik Ashtar katika ile barua yake maarufu (ya 331 ndani ya Nahjul Balagha) akimpa miongozo ya jinsi ya kuamiliana na watu walioko chini yake na kumtaka asiwe mithili ya mbwa mwitu mkali mbele yao. Katika sehemu moja ya barua yake hiyo Imam Ali AS anasema: "Watu wako wa namna mbili ima atakuwa ni ndugu yako katika dini au ni binaadamu mwenzako." Hii ina maana kwamba kwa mtazamo wa Amirul Muuminin ni kuwa linapofika suala la kulinda na kutetea haki za binaadamu na za mtu aliyedhulumiwa, mtu anapaswa kutosema kwamba madhali huyu si Muislamu basi siwezi kumtetea kwani Waislamu na wasio Waislamu wana haki ya kutetewa. Angalieni ni jinsi gani Imam Ali alivyoweza kupeperusha bendera ya heshima na mantiki ya hali ya juu ya Uislamu kuhusiana na haki za binaadamu! Hata hivyo leo hii kuna watu duniani wanadai kutetea haki za binaadamu lakini ni wazi kuwa si wakweli katika maneno yao. Ni watu wa kujionyesha, ni wasema uongo, ni riya ya wazi wanayoionyesha kwani hata katika nchi zao wenywewe hawachungi haki za binaadamu sembuse tena katika maeneo mengine duniani! Maana halisi ya haki za binaadamu ni hiyo iliyoainishwa kwa uwazi kabisa na Amirul Muuminin Ali AS.

Uislamu unalinda hata haki za wahalifu. Katika Uislamu mtu hana ruhusa ya kumtukana na kumpa jina baya hata mtu aliyehukumiwa kifo. Uislamu unasema hukumu ya mtu huyo ni kifo, si kumtukana kwani kumtukana mtu huyo ni kumdhulumu, ni kumvunujia haki zake na inabidi jambo hilo lipigwe marufuku. Hivyo ndivyo unavyofunza Uislamu kuamiliana na mtu ambaye tayari ameshahukumiwa kifo seuze tena aliyehukumiwa kifungo tu, seuze tena mtuhumiwa anayetafuwa, seuze tena mtu ambaye kosa lake haliko wazi na halijathibitika bali anadhaniwa tu! Inabidi haki za binaadamu zichungwe kikamilifu kwa watu wote kama zilivyoainishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Juu ya ukurasa

Nafasi ya Mwanamke na Haki za Binaadamu katika Uislamu

Haki za Kisiasa za Mwanamke katika Uislamu

Uislamu umempa haki mwanamke ya kumiliki, kuunga mkono mtu anayetaka na kushiriki vilivyo katika nyuga muhimu za kisiasa na kijamii. Qur'ani tukufu inasema:

"Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana nao ahadi, na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi maghfira, Mwenye kurehemu."

Wanawake mbalimbali walikuwa wakienda kwa Bwana Mtume kumpa bay'a na kutangaza uungaji mkono na utiifu wao kwake, na Bwana Mtume hakusema kwamba waje wanaume tu kunibai na kutangaza utiifu wao na wanawake wasiende. Wala Bwana Mtume hakusema wanaume tu ndio wapewe nafasi ya kutoa maoni yao na chochote wanachoamua wanaume basi wanawake lazima wafuate. Hapana, bali alisema wanawake nao wapewe nafasi ya kutoa bay'a, wanawake nao washirikishwe katika maamuzi na wao wawe na nafasi ya kuukubali au kuukata utawala na mfumo wa kijamii na kisiasa uliopo. Wamagharibi wako nyuma na wamepitwa na Uislamu katika jambo hilo kwa miaka 1100.

Juu ya ukurasa

Nafasi ya Mwanamke katika Jamii

Kama nchi itafanikiwa kuwaelimisha wanawake kupitia mafundisho ya Kiislamu na maamrisho ya dini hiyo tukufu, basi maendeleo ya nchi hiyo pamoja na heshima na utukufu wake utaongezeka maradufu. Wanawake wanapojitokeza vilivyo na inavyotakiwa katika kila uwanja, maendeleo yanayopatikana ndani yake huwa maradufu. Sifa maalumu ya kujitokeza akinamama katika nyuga tofauti ni kwamba wakati mwanamke wa familia anapoingia uwanjani, maana yake ni kuwa mumewe na wanawe nao wako uwanjani. Lakini mwanamme anapojitokeza hali haiwi hivyo. Hivyo mwanamke anapokuja uwanjani huandamana na watu wa familia yake.

Juu ya ukurasa

Kudhulumiwa Mwanamke katika Familia

Kumzuia mwanamke asisome na wala kupata elimu na maarifa sahihi ni kumdhulumu. Ni dhulma kumuweka mwanamke katika hali ambayo atashindwa kupata elimu ya maadili yake, ya dini yake na elimu nyinginezo kutokana na wingi wa kazi na kuelemewa na mashughuli. Ni dhulma kumuweka mwanamke katika mazingira ambayo yatamzuia kutumia anachokimiliki kwa uhuru na mapenzi yake mwenyewe. Kama mwanamke atalazimishwa kuolewa yaani kama hatapewa nafasi yoyote ya kuamua ima kukubali au kukataa kuolewa, huko ni kumdhulumu. Ni dhulma kumnyima mwanamke haki yake ya kunufaika na mapenzi ya mwanawe iwe ni wakati yuko kwa mume au hata baada ya kutengana na mume. Kama mwanamke atakuwa na kipaji maalumu kama vile kipaji cha kielimu, kipaji cha uvumbuzi na ubunifu, au kipawa cha kisiasa na vipawa vinginevyo katika jamii na asipewe fursa ya kutumia vipaji vyake; hiyo nayo itakuwa ni dhulma dhidi yake.

Juu ya ukurasa

Suala la Kimsingi la Wanawake

Suala la kimsingi kuhusiana na mwanamke si kuanalia kwamba ana kazi au hana. Suala la kimsingi la mwanamke ni lile ambalo kwa bahati mbaya limefutwa na halishuhudiwi katika jamii za nchi za Magharibi nalo ni mwanamke kujihisi kuwa na utulivu na kujihisi yuko salama, na aone kuwa hakuna kitu kinachohatarisha usalama wake, hadhulumiwi katika jamii wala katika maisha yake mume na mke na wala nyumbani kwao.

Juu ya ukurasa

Uadilifu katika Hakizi za Binaadamu baina ya Mwanamme na Mwanamke

Uislamu ni dini inayounga mkono ukamilifu wa mwanaadamu. Katika Uislamu hakuna tofauti baina ya mwanamke na mwanamme. Mwanamke na mwanamme ni jinsi mbili za mwanaadamu. Hakuna tofauti yoyote baina yao katika upande wa ubinaadamu na katika upande wa ibada.

Lengo la Uislamu la kulinda haki za mwanamke ni kwamba mwanamke asidhulumiwe na wala mwanamme asijione ni mtawala wa mwanamke. Uislamu umeweka mipaka na haki maalumu katika familia. Mwanamme ana haki zake na mwanamke ana haki zake na haki hizo zimegawanywa kwa uadilifu na usawa wa hali ya juu.

Unachozingatia Uislamu ni maadili ya mtu, ni kipaji cha mtu, ni utendaji wa mtu jambo ambalo linazihusu jinsi zote mbili za mwanaadamu kulingana na maumbile ya kila mmoja wao. Uislamu unatambua vyema maumbile ya mwanamke kama unavyotambua vizuri pia maumbile ya mwanamme. Kitu kilicho muhimu katika Uislamu ni uadilifu yaani kuchunga uadilifu baina ya wanaadamu wa jinsia zote. Lililo muhimu katika Uislamu ni usawa hata kama katika baadhi ya mambo hukumu zinazohusiana na mwanamke ni tofauti na zile zinazohusiana na mwanamme kulingana na maumbile yao na sifa maalumu alizo nazo kila mmoja wao.

Juu ya ukurasa

Upinzani wa Nchi za Magharibi Dhidi ya Uislamu kwa Madai ya ya Kutetea Haki za Binaadamu

Lengo la maadui duniani – wawe ni wastakbari na mabeberu wanaoongozwa na Marekani au maadui wadogo wadogo – katika kila kona ya dunia la kuamua kuyapinga Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kwamba wanauchukia Uislamu. Wao ni maadui wa Uislamu kwani wanauona Uislamu unakwamisha malengo yao ya kupora mali za mataifa mengine. Wanaupinga Uislamu kwani wanajua kuwa Uislamu unakata miguu ya mbwa koko waliokusudia kukanyaga haki za nchi hii. Wanaupinga Uislamu wakidai hauheshimu haki za binaadamu lengo lao likiwa ni kuipaka maJuu ya ukurasae dini hiyo tukufu ya Mwenyezi Mungu. Wanafanya hivyo katika hali ambayo Uislamu uko mstari wa mbele katika kulinda na kutetea haki za binaadamu wote. Nini maana ya haki za binaadamu? Je Wapalestina waliofukuzwa majumbani mwao na Wazayuni makhabithi na kutelekezwa katika baridi hii kali ya kipindi cha baridi wao si binaadamu? Je wao hawana haki? Je neno haki za binaadamu linapoteza maana yake linapofika kwenye suala la Wapalestina? Kwani kipengee muhimu kabisa cha hati kuu ya haki za binaadamu – ambayo mabwana hawa wanakipigia domo – si kwamba kila mtu yuko huru nyumbani kwake na ana uhuru wa kuchagua maskani anayopenda? Kwani Palestina si nyumbani kwa Wapalestina? Je wanavyofanyiwa ni haki za binaadamu? Je Wapalestina si binaadamu? Ni nani leo hii asiyejua uongo mkubwa wa kijinai wa madai ya wanaotetea haki za binaadamu dunaini?

Juu ya ukurasa

Kutumia Nguvu na Kupinga Utumiaji Nguvu

Tab'ani "Kutumia nguvu na kupinga utumiaji nguvu" ni mambo mawili yanayokamilishana. Baadhi ya watu duniani ambao wanadai kutetea haki za binaadamu na kukabiliana na mateso, wanafanya unyama, mauaji na mateso makubwa kabisa dhidi ya binaadamu na kisha wanapiga domo la kupigania haki za binaadamu na wanadai wanapinga vitendo vya mateso! Ukweli wa mambo ni kuwa, katika kuamiliana na mambo baadhi ya wakati inatakiwa kutotetereka na ikibidi kutumiwa nguvu lakini kuna sehemu nyingine nyingi inabidi kutumia upole wa hali ya juu, huruma na heshima. Inabidi hali hizo zote mbili ziweko pamoja siku zote.

Juu ya ukurasa

Faslu ya Pili: Haki za Binaadamu katika Nchi za Magharibi

Faili Jeusi la Magharibi katika Suala la Haki za Binaadamu

Leo hii Wamagharibi wenye faili jeusi na mikono meusi kaitka suala la haki za binaadamu wanathubutu kutaka kuufundisha ulimwengu wa Kiislamu haki za binaadamu na haki za mwanamke na kutoa mwito wa amani! Watu ambao katika kipindi cha miaka 20 tu wamezusha Vita Viwili Vikuu vya Dunia na kuangamiza mamilioni ya watu; wale watu ambao wametengeneza bomu la Atomiki na kulitumia kuua maelfu kwa maelfu ya binaadamu na kuiweka katika hatari dunia nzima; wale watu ambao wamevamia nchi za bara la Afrika, Amerika ya Latini na Asia na kufanya jinai kubwa kubwa dhidi ya binaadamu jinai ambazo mwanaadamu kamwe hawezi kuzisahau – Hakuna Mhindi yeyote anayeweza kuisahau Uingereza, wala Mualegeria yeyote anayeweza kuwasahau Wafaransa na wala watu wa nchi nyinginezo – watu ambao wametengeneza, kuwatumia na kuwaandaa kwa silaha za kemikali watu kama Saddam Husain leo hii wanathubutu kujitokeza hadharani na kudai ni polisi wa dunia wanaopambana na silaha za kemikali! Mfano wa jambo hilo ni kama kumchukua mwendesha magendo mkubwa ukamfanya mkuu wa kupambana na magendo.

Juu ya ukurasa

Kutafuta Maslahi kwa Jina la Haki za Binaadamu

Leo hii vyombo vya propaganda vibaraka wa Wazayuni na Marekani au kwa maneno mengine vibaraka wa mabepari na waporaji wa kimataifa, ambapo mara nyingi vyombo vyao vya kifedha vinawadanganya na kuwafumba macho walimwengu, vinajilabu na kujigamba kwamba vinatetea demokrasia; wakati ambapo hakuna ukweli wowote unaotangazwa na vyombo hivyo. Vinadai kutetea haki za binaadamu; wakati ambapo vinafanya kinyume kabisa na ukweli wa mambo na hakuna lolote la haki vinalolisema. Kimsingi kitu ambacho hakimo kabisa katika malengo na akili za makampuni hayo na ambacho hawakiheshimu hata chembe ni haki za mataifa mengine; haki za binaadamu.

Juu ya ukurasa

Mwanamke kwa Mtazamo wa Magharibi

Angalieni, hadi karibuni kabisa mwanamke hakuwa na haki za kumiliki mali binafsi katika nchi za Ulaya na Magharibi. Mambo yalianza kuboreka pole pole mwanzoni mwa karne ya ishirini na pamoja na kupigwa makelele mengi na kutolewa madai haya na yale, lakini hadi leo wanawake hawana uhuru wa kuvaa mavazi wanayopenda kama vile Hijabu na kila leo upinzani dhidi ya vazi hilo unaongezeka. Madhara ya mchanganyiko usio na mipaka wa wanawake na wanaume umeshawashinda. Wanadai huko ni kumpa haki zake mwanamke, lakini wakati huo huo mwanamke wa Magharibi hadi karibuni kabisa hakuwa na haki ya kutumia anavyopenda mali yake mwenyewe! Yaani wakati mwanamke alipoolewa, utajiri wake mali zake na kila alichomiliki kilikwenda kwa mwanamme, yeye mwenyewe hakuwa na haki ya kutumia anavyotaka. Hali ilikuwa hivyo hadi mwanzoni mwa karne ya 20 ndipo wanawake wa nchi za Magharibi walianza pole pole kupewa haki ya kumiliki mali zao na haki ya kufanya kazi! Mambo hayo ni miongoni mwa haki za kimsingi kabisa za binaadamu lakini wanawake wa Ulaya na Marekani walinyimwa. Sisi inabidi tuwaulize maswali mengi Wamagharibi ambao katika kipindi cha miaka mingi ya huko nyuma hadi leo hii wamekuwa wakimdhalilisha mwanamke kiasi chote hiki.

Juu ya ukurasa

Mambo Yanayothaminiwa katika Jamii ya Marekani

Mnadhani ni mambo gani yanathaminiwa nchini Marekani? Wamarekani wameweka msingi ujulikanao msingi wa Kimarekani na wanasema ni msingi wa dunia nzima. Msingi huo ni uhuru wa mwanaadamu, uhuru wa kufikiri, heshima ya mwanaadamu, haki za binaadamu na vitu kama hivyo. Lakini cha kujiuliza ni kwamba hivi kweli hiyo ndiyo misingi ya Wamarekani?! Je hizo ndizo sifa ilizo nazo jamii ya Marekani leo hii?! Je hizo ndizo sifa ilizo nazo utawala wa Marekani?! Je utawala huo si ndio ule ulioundwa baada ya wenyeji wa nchi ya Marekani kuulizwa kwa umati? Ni utawala uliowaangamiza kabisa Wahindi wekundu! Je utawala huo na watu wenye nguvu ndani yake si ndio wale wale waliozivamia nchi za Afrika wakawafanya watumwa mamilioni ya watu wake wanawake kwa wanaume na kuamiliana nao kikatili mno kwa miaka nenda miaka rudi? Leo hii athari ya sanaa inayosikitisha na kuumiza kabisa ni ile yenye jina la "Kibanda cha Ami Tom" inayoonyesha maisha ya utumwa huko Marekani kisa ambacho labda kiliandikwa miaka 200 iliyopita na hadi leo bado ni maarufu. Huo ndio uhakika wa Marekani na utawala wake. Sifa ambazo Marekani imejionyesha kuwa nazo kwa walimwengu ni hizo na wala si uhuru wa mwanaadamu, na wala si usawa wa mwanaadamu, kwanza usawa gani huo wa mwanaadamu walio nao?! Hadi leo hii hawaamini usawa baina ya watu weusi na watu weupe. Hadi leo hii mtu kuwa na asili ya Wahindi wekundu ni dosari katika uteuzi wa nafasi za kazi. Wanadai misingi iliyowekwa na Marekani ni ya dunia nzima, ni mantiki ya aina gani hiyo wanayotumia? Mnasema kwamba misingi hii tuliyoweka sisi inabidi itumike duniani kote na kila anayekataa mwende mukamwangamize kwa bomu la Atomiki! Je hiyo ndiyo mantiki ya taifa huru?! Je mantiki hiyo ni mantiki ya utawala unaoamini kweli heshima ya mwanaadamu?! Hamuoni tabu kuwaambia uongo wanaadamu kiasi chote hicho?!

Juu ya ukurasa

Uongo wa Madai ya Kutetea Haki za Binaadamu

Ni nani asiyejua kwamba shaari na kaulimbiu ya kutetea haki za binaadamu na demokrasia inayopigwa na viongozi wa Ikulu ya Marekani White House ni uongo mtupu?

Utawala wa Marekani ambao umekuwa ukifanya mauaji mengi mno katika kipindi cha miaka mingi sasa umekuwa na uadui mkubwa pia na tawala huru za Asia, Afrika na Kusini Amerika, na umekuwa ukiziunga mkono tawala za kidikteta na za kupandikizwa. Marekani ndio utawala unaoongoza kwa kueneza silaha hatari katika pembe mbalimbali za dunia, unalea na kusaidia magaidi hatari zaidi duniani, ndio utawala ulioua raia wengi zaidi duniani, unapinga haki za kimsingi kabisa za taifa madhlumu sana la Palestina, unaupa misaada ya kila hali utawala katili zaidi duniani yaani utawala wa Kizayuni wa Israel, uliutetea na kuulinda utawala wa kijabari na kikatili wa Kipahlavi nchini Iran kwa makumi ya miaka, unalifanyia uadui na jinai kubwa taifa la Iran katika upande wa kiuchumi, kijeshi na kisiasa, hivi sasa unautuhumu mfumo wa wananchi ulio huru na unaojitegemea wa Iran kwamba unaunga mkono ugaidi na kuvunja haki za binaadamu pamoja na kudai unatengeneza na kuuza silaha!

Tangu mwaka 1945 hadi leo hii serikali ya Marekani imehusika na kupindua serikali 40 huru ambazo hazikuwa vibaraka wa Marekani na katika kesi 20 na kitu hivi, imetumia nguvu za kijeshi! Nguvu zote hizo za kijeshi zimekwenda sambamba na mauaji ya umati ya raia na mabalaa mengine makubwa. Tab'an kuna baadhi ya sehemu wamefanikiwa na kuna baadhi wameshindwa. Miongoni mwa matukio hayo ni mashambulizi ya mabomu angamizi ya Atomiki yaliyofanywa na Marekani nchini Japan mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, vita vya kikatili na umwagaji mkubwa wa damu vya Vietnam, ambavyo hatimaye Marekani ilishindwa na kulazimika kukimbia, mfano mwengine ni nchini Chile, Iran katika mapinduzi ya tarehe 28 Mordad (Agosti 19, 1953) – ambapo maafisa wa Marekani walikuja mjini Tehran na kuanza kupanga njama za mapinduzi hayo na baadaye kuzitekeleza. Baada ya hapo ni wao wenyewe wakatangaza jambo hilo na kueneza nyaraka zake. Kiujumla kuna mifano mingi ya uingiliaji kijeshi wa Marekani kwa nia ya kupindua tawala za mataifa mengine. Wanaofanya yote hayo ni makampuni makubwa ya kiuchumi, mapebari na makabaila wa Marekani, vyama vinavyopenda ukubwa, magenge yenye ushawishi mkubwa ya Kizayuni, watu mashuhuri wenye aibu za kifikra na kimaadili ambao ndio wanaoongoza mambo yote hayo. Hilo ni jalada zito sana lenye historia chafu mno. Hayo si mambo madogo. Watu hao hawajali kuangamiza watu, utajiri, uadilifu na majanga mengineyo. Hakuna moja kati ya mambo hayo linalowashughulisha. Tab'an wanatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuficha maovu yao kupitia propaganda kubwa za vyombo vyao vya habari. Wanazungumza kwa sauti kubwa kubwa ili kuandaa mazingira ya kuulazimisha ulimwengu usiguswe na maafa yao makubwa na waonekane ni watu wanaopenda amani, demokrasia na haki za binaadamu.

Wakati wa Urais wa Bush Baba, Wamarekani wenye asili ya Afrika waliendelea kufanyiwa dhulma ya waziwazi kiasi kwamba walilazimika kufanya uasi mkubwa katika baadhi ya majimbo ya Marekani kiasi kwamba wanajeshi wa nchi hiyo walilazimika kuingilia kati baada ya polisi kushindwa kukabiliana na uasi huo. Katika kipindi cha Rais wa baadaye, zaidi ya watu 80 wa kundi la David – ambalo ni kundi la Kikristo lililopinga siasa za Marekani – walichomwa moto hai katika nyumba waliyokuwa wamekusanyika kwa madai kuwa walikhalifu amri ya polisi iliyowataka watoke nje. Wanawake na watoto wadogo walikuwemo kwenye nyumba hiyo lakini hilo halikuishughulisha serikali ya Marekani na waliwachoma hai watu wote hao! Hivi ndivyo wanavyoheshimu haki za binaadamu! Wakati wa Urais wa Bush Mwana pia Wamarekani walivamia Afghanistan wakawamiminia mabomu ya kila namna wakazi wa kaskazini mwa nchi hiyo na kufanya unyama mwingine mwingi katika miji mingine ya nchi hiyo, waliwafyatulia risasi na kuwaua kwa umati watu wengi katika jela moja na habari yake ilipenya duniani lakini mabepari wa habari hawakuruhusu habari hizo zipate nguvu na kuwafikia vilivyo walimwengu. Uvunjaji wa haki za binaadamu ndani ya Marekani na ule unaofanywa na Wamarekani katika pembe mbalimbali duniani ni mkubwa zaidi kuliko nchi zote nyingine duniani, lakini pamoja na hayo wanapotosha ukweli wa mambo na kuwatuhumu watu wengine duniani likiwemo taifa la Iran na serikali na utawala wa Kiislamu nchini kwamba ndio unakanyaga haki za binaadamu! Bendera ya madai ya kutetea haki za binaadamu leo hii imebebwa na watu ambao wenyewe ndio wavunjaji wakuu wa haki hizo duniani.

Juu ya ukurasa

Ulaya Mvunjaji Mkuu wa Haki za Binaadamu

Serikali za Ulaya ndizo zinazoongoza kwa uvunjaji wa haki za binaadamu katika kipindi kizima cha karne iliyopita na kama mtu ataangalia historia ya Ulaya miaka mia moja nyuma zaidi ataona hali ni hiyo hiyo. Kwa uchache katika kipindi hiki cha miaka mia moja iliyopita, hawa mabwana wa Ulaya wamezusha vita viwili vikubwa duniani vilivyokuwa na uharibifu mkubwa. Ni watu wa Ulaya ndio waliozusha vita viwili vikubwa vya dunia katika kipindi cha karne mbili tu. Habari za vita hivyo viharibifu mno vilivyopelekea kushuhudiwa maafa makubwa ni za makumi ya miaka iliyopita, lakini katika zama zetu hizi pia mtu anaweza kujiuliza ni nani aliyepeleka viwanda vya silaha za kemikali huko Iraq na kusababisha maafa yasiyo na kifani? Majibu ni kuwa ni hizo hizo nchi za Ulaya. Ni nani anayeisaidia Israel ifanye jinai za kila leo kama si hizo hizo nchi za Magharibi?

Juu ya ukurasa

Haki za Binaadamu kwa Mtazamo wa Uingereza

Waingereza wanajitangaza kwa walimwengu kuwa wao ni watu wanaofanya mambo kwa usamehemu, subira na uvumilivu. Lakini walimwengu wameuona uvumilivu na usamehevu wa Waingereza hasaa huko nchini Iraq! Wamewashuhudia jinsi Waingereza walivyokuwa wakiingia katika nyuma za watu kwa mitutu ya bunduki, wakawapora wananchi maisha yao ya salama, wakawafanya watoto walizane kwa khofu. Wakati wananchi waliposhindwa kuvumilia na kuamua kuandamana katika miji mbalimbali ya Iraq kama vile Baghdad, Mosul na kwenye miji mingineyo, Waingereza hao hao wanaodai ni wasamehevu walijibu kwa kuwafyatulia risasi. Hiyo ndiyo demokrasia, usamehevu, kuwapenda raia na kulinda haki za binaadamu kunakoonyeshwa kivitendo na Waingereza! Mambo hayo inabidi yatiliwe maanani na watu wanapaswa kuyaelewe vyema.

Juu ya ukurasa

Faslu ya Tatu:Iran na Haki za Binaadamu

Haki za Binaadamu katika Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu

Haki za kweli za binaadamu zinaweza kupatikana tu katika kivuli cha Uislamu na ndani ya serikali ya Kiislamu. Ni Uislamu ndio unaosema:

Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. (Surat Yusuf (12):40).

Amri hii ya Mwenyezi Mungu inapinga utawala wowote ule wa kidhalimu. Hakuna mtu yeyote aliye na haki za kuwatawala watu ila ambaye ana sifa zilizokubalika na mwenye kukubaliwa na watu.

Uislamu unalinda haki za binaadamu. Hakuna dini yoyote inayompa heshima kubwa mwanaadamu kwa kiwango ambacho Uislamu unampa. Miongoni mwa misingi ya Kiislamu ambayo inasisitiziwa na Uislamu ni msingi wa heshima ya mwanaadamu. Haki za binaadamu zinaweza kulindwa vyema katika kivuli cha Uislamu. Ni Uislamu ndio ambao unalinda haki za binaadamu kutokana na hukumu na sheria zake katika kila kitu kama vile sheria za mahakamani, sheria za kuwalinda wananchi, sheria za uma na masuala ya kisiasa n.k. Hilo linatofautiana sana na zile sheria bandia za kulinda haki za binaadamu zinazodaiwa kupiganiwa leo duniani.

Nchi za Magharibi zinazota maneno ya uongo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu zikidai kuwa haiheshimu haki za binaadamu. Lakini nchi hizo zinapotoa madai hayo zinalenga moja kwa moja kwenye sheria na kwenye ile mipaka ya Kiislamu inayolindwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Qur'ani Tukufu inasema:

Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; (basi msiikiuke). Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. (at Talaaq (65):1).

Mtu yeyote anayechupa mipaka ya Mwenyezi Mungu basi mtu huyo anajiweka katika hali ya kukabiliana na Mwenyezi Mungu. Utawala wa Jamhuri ya Kiislamu unalinda na kuchunga haki za binaadamu na hausubiri Wamagharibi waje kuufundisha maana ya haki za binaadamu au kuunasihi uchunge haki hizo! Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran inalinda haki za binaadamu kutokana na amri za Uislamu na kwa sababu hilo ni katika misingi ya dini hiyo tukufu. Lakini kitu kinachodaiwa na Wamagharibi ni uongo na hila zilizo wazi. Wanatoa madai ya uongo ya eti kulinda haki za wanawake na haki za binaadamu! Mabeberu na wastakbari hao, wakandamizaji na waporaji hao duniani, watu baki wasiojali haki za mataifa mengine na waangamizaji wa mali za mataifa dhaifu, watu hao wanaozikalia kwa mabavu ardhi za nchi dhaifu, leo hii wanajitokeza kifua mbele wakidai wanatetea haki za binaadamu na haki za wanawake! Ni jambo lisiliopingika kwamba mataifa ya Kiislamu hayawezi kushughulishwa na ghilba za watu hao.

Ni sheria zilizojaa nuru za Uislamu ndizo ambazo leo hii licha ya kuweko mawimbi ya kila upande wa propaganda ghalati na potofu dhidi ya Uislamu, lakini mwanamme wa Kiislamu amepata fakhari ya kujitokeza kwa ushujaa na kwa uhuru kamili. Hizo ni miongoni mwa baraka za Uislamu. Malezi ya Kiislamu na kimapinduzi anayopata mwanamke wa Kiislamu ni jambo inalojivunia na kijifakharisha kwalo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Juu ya ukurasa

Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Jamhuri ya Kiislamu

Haja ya Kuelimishwa Wananchi

Mfumo wa wananchi – ambao unawashirikisha vilivyo wananchi – hauwezi kuwepo bila ya kuelimsihwa wananchi. Inabidi wananchi wake wawe na elimu ya kutosha. Inabidi wawe na elimu ya kutosha ya kuwawezesha kuchanganua vizuri mambo. Elimu katika mfumo kama huo ni mithili ya maji na hewa kwa mwanaadamu. Hivyo ndivyo ulivyo mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Kadiri elimu ya wananchi inavyopanda na kuongezeka, ndivyo mfumo huu wa utawala unavyozidi kunufaika. Hivyo mfumo huu unahitajia watu wawe na elimu.

Juu ya ukurasa

Vyombo vya Habari katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Vyombo vya habari katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu si kitu cha kujionyesha na kujilabu nacho. Hivyo miongoni mwa kazi za kimsingi zinazofanywa na mfumo huu ni kuongeza idadi ya vyombo vya habari, kuvifanya anuwai kwa anuwai na kuongeza ubora wake. Vyombo vya habari ni kitu cha lazima kwa jamii ya Iran na hakiepukiki. Jamii yoyote inayotaka kuishi vizuri haiwezi kujiweka mbali na vyombo vya habari. Vyombo vya habari navyo vina majukumu matatu makuu; jukumu la kukosoa na kusimamia, jukumu la kupasha habari za kweli na za wazi na jukumu la kutoa na kusambaza mitazamo na fikra katika jamii.

Wakati jamii inapokosa vyombo vya habari huru vyenye waandishi mahiri waliobobea, hupoteza vitu vingi vingine. Kuweko vyombo vya habari huru ni dalili za kupevuka taifa. Uhuru wa kuandika na kusema ni haki ya wazi ya wananchi na ya vyombo vya habari. Aidha jambo hilo halina shaka hata kidogo bali ni miongoni mwa vifungu vilivyo wazi vya Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu. Tab'an sambamba na jambo hilo la thamani, kuna mambo mengine muhimu ambayo hayapaswi kukanyagwa kwa madai ya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kalamu. Hapo ndipo unapoonekana umahiri wa vyombo vya habari. Huo ndio mwendo unaopasa kufuatwa.

Juu ya ukurasa

Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Mfumo wa Kibepari

Hakuna gazeti lolote barani Ulaya na Marekani ambalo halimilikiwi na mabapari! Ni gazeti gani la huko Ulaya na Marekani linalomilikiwa na watu wa matabaka ya kati na ya chini la kuweza kutumiwa uhuru wa gazeti kama hilo kuonyesha uhuru wa watu wa matabaka hayo? Magazeti ya Ulaya na Marekani yanamilikiwa na akina nani? Yanamilikiwa na mashirika makubwa ya kibepari. Yaani vyombo hivyo vya habari vipo kwa ajili ya kuwatetea mabepari na ndio maana tunaona wakati wowote vyombo hivyo vinapoamua kumchafua mtu vinamchafua na wakati wowote vinapotaka kumkuza na kumnyanyua mtu vinamnyanyua. Wanawaburuza wananchi kama bendera inavyofuata upepo. Sasa huo ndio tutasema ni uhuru?

Juu ya ukurasa

Sharti la Kuongezeka Idadi ya Vyombo vya Habari

Rasilimali kuu ya chombo chochote cha habari ni imani ya wananchi na imani hiyo inapatikana kwa kutilia maanani matukufu na itikadi ya walio wengi pamoja na kuchunga heshima na hadhi ya mfumo pamoja na kutangaza mambo sahihi na ya kweli. Kama vyombo hivyo vya habari vitakuwa chimbuko wa fikra huru, vitalinda maslahi ya nchi, vitafanya kazi kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi na kwa ajili ya manufaa ya dini kama inayosema Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu, basi kadiri idadi ya vyombo hivyo inavyoongezeka inakuwa ni jambo la kheri.

Juu ya ukurasa

Jukumu Kuu la Vyombo vya Habari katika Utawala wa Kiislamu

Jukumu kuu la vyombo vya habari katika utawala wa Kiislamu ni nafasi yake katika kutangaza na kulinda matukufu na malengo ya uma wa kimapinduzi wa Iran pamoja na kuongeza kiwango chao cha maarifa na utambuzi. Hivi sasa na hususan baada ya kufeli kikamilifu Umaksi, ubeberu wa Magharibi umeelekeza mashambulizi yake yote upande wa mataifa ya kimapinduzi kwa ajili ya kujizatiti kisiasa na kueneza fikra za kupinga mafundisho matukufu ya Mwenyezi Mungu. Wanatumia mbinu mbalimbali na wanachokilenga zaidi ni utamaduni wa mataifa hayo. Hivyo miongoni mwa ratiba kuu za vyombo vya mawasiliano ya uma zinapaswa kuwa ni kupambana vilivyo na mashambulizi hayo ya kiutamaduni ya Magharibi katika pande zake zote.

Juu ya ukurasa

Haja ya Kusimamiwa Vyombo vya Habari

Lengo letu la kuvipa nasaha mara kwa mara vyombo vya habari ni kwamba tunataka kuhakikisha kuwa vyombo hivyo vinaamiliana na masuala ya nchi kwa hisia za kuwajibika na kuhisi majukumu. Vinapaswa kuwa macho visije vikageuka kuwa chombo cha madui na kuanza kumrahishia kazi adui huyo. Jambo hilo ndilo analotaka adui litokee katika anga ya kifikra na kiutamaduni ya jamii. Anataka kupambana na wananchi kupitia vyombo vya habari vya ndani ya nchi. Hilo kwa kweli ni kosa kubwa. Na kama kuna chombo cha habari nchini kitafanya hivyo kwa makusudi na kwa kujua basi huo utakuwa ni usaliti mkubwa na kama kitafanya hivyo kwa kutojua litakuwa ni kosa kubwa. Inabidi watu wote wawe macho na wachunge matendo yao.

Hivyo kuvisimamia vyombo vya habari ni jambo la lazi na ni jukumu muhimu. Kama vyombo hivyo havitasimamiwa ni jambo lililo wazi kwamba havitaweza kutimia matakwa na malengo ya taifa. Kuna baadhi ya watu wanadhani kwamba fikra za walio wengi ni eneo huru lisilo na sheria zozote na wanadhani wako huru zifanya wanavyotaka fikra hizo za walio wengi! Lakini fikra za walio wengi si panya wa maabara ambaye kila mtu anamfanya anavyotaka, wakati wowote anaopenda. Watu hao wanajeruhi imani, hisia na matukufu ya watu kupitia uchambuzi ghalati wanaoutoa na na uvumi, uongo na matusi yao. Ni wazi kuwa jambo hilo si sahihi hata kidogo. Hivyo kusimamiwa vyombo vya habari ni jambo la lazima ili kuepusha madhara kama hayo.

Juu ya ukurasa

Kutochukua Misimamo ya Pupa ya Kisiasa katika Masuala ya Haki za Binaadamu

Masuala ya kiutamaduni na kisiasa ndiyo yanayolengwa zaidi leo hii na madola ya kibeberu. Utayaona madola hayo yanazusha makelele mengi kuhusu kadhia kama ya mwanamke, haki za binaadamu, demokrasia na harakati mbalimbali za ukombozi kwa nia ya kutoa mashinikizo na kuufanya upande wa pili uchukue misimamo ya pupa. Litakuwa ni kosa kubwa mtu kama watu watachukua misimamo na kuanza kusema maneno ya kutaka kuwaridhisha mabeberu katika kukabiliana kwao na makelele wanayoyazushwa. Huko ndiko kunakoweza kusemwa ni kuchukua maamuzi kwa pupa.

Watu hao ambao wenyewe hawajali chochote katika suala la haki za binaadamu – tab’an kwa maana halisi ya haki za binaadamu – wana haki gani ya kuwasakama wengine! Ajabu ni kuwa Marekani leo hii inadai inaongoza kampeni za kutetea haki za binaadamu! Kabla ya kuanzisha vita vyake, Marekani kwanza iliituhumu serikali ya Iraq kuwa inatumikia tawala zinazounga mkono ugaidi. Lakini katika miaka ya 1360 na 1361 (1981 na 1982) wakati wanamapambano shupavu wa Iran walipofanikiwa kumshinda adui na kumtoa katika mipaka ya nchi yao na wakati adui wa Kibaath alipoona ameshindwa na wanamapambano wa Kiirani, alianza kutumia silaha za kemikali na silaha za mauaji ya halaiki yaani alifanya jinai za kivita. Hapo hapo na bila ya kusita Marekani iliamua kuungana na kuisaidia Iraq ili iweze kutekeleza jinai zake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Wakati serikali ya wakati huo ya Iraq ilipokuwa inatumia silaha za kemikali dhidi ya hata raia wake yenyewe, ndio wakati huo huo ambao mabeberu waliitoa serikali ya Iraq katika orodha ya serikali zinazounga mkono ugaidi! Hiyo ndiyo maana wanayoijua mabeberu ya neno haki za binaadamu!

Muungaji mkono mkubwa zaidi wa uvunjaji wa haki za binaadamu ulioshuhudiwa duniani hadi leo hii ni tawala hizo hizo za kiistakbari kama vile Marekani. Lakini leo hii mabeberu hao wanajitokeza kifua mbele wakidai wanatetea haki za binaadamu na kuyataka mataifa mengine yawafuate wao! Huu kama si ubazazi ni kitu gani?! Ndio maana tukasema kama katika upande mwingine watatokezea watu waanze kuzungumzia haki za binaadamu kwa sura ya kutaka kuwaridhisha mabeberu hao, watakuwa wamefanya kosa kubwa sana. Huko ndiko kutakakoitwa kuchukua maamuzi ya pupa mbele ya adui. Hali ni vivyo hivyo katika suala la mwanamke. Baada ya kusimamishwa utawala wa haki, Alhamdulillah wanawake wa nchi ya Kiislamu ya Iran wameweza kupata nafasi yao ya kweli kwa kiwango kikubwa sana. Wamepata fursa za kujitokeza katika medani tofauti na kuonyesha uadhama wa moyo wa mwanamke wa Kiislamu. Huku uhakika ukiwa ni huo, mabeberu wanazuka na kuanza kueneza uvumi na maneno ya uongo kwamba eti haki za wanawake hazithaminiwi katika Jamhuri ya Kiislamu. Ulimwengu wa Magharibi unapaswa kuangalia uhalisia wa mambo yanavyojiri ndani ya Jamhuri ya Kiislamu. Wanapaswa kufuta mitazamo yao ghalati kuhusu masuala kama ya wanawake, haki za binaadamu, uhuru na demokrasia. Inawabidi warejee katika Uislamu na waone ni nini maana hasa ya maneno hayo. Taifa la Iran limeonyesha kwa wazi kuwa haliko tayari kurejea nyuma hata kwa hatua moja katika kukabiliana na maadui wanaopenda makuu, na hawako tayari kamwe kuachana na misingi ya dini yao ya Kiislamu kwa ajili ya kumridhisha adui. Kuwa na misimamo madhubuti kama hiyo ni jambo zuri sana.

Juu ya ukurasa

Kulindwa Haki za Binaadamu nchini Iran na Ulaya na Kinyume Chake

Kama leo hii kuna wasiwasi kuhusu suala la kukanyagwa haki za binaadamu – ambapo sisi nasi tuna wasiwasi sana na jinsi haki za binaadamu zisivyochunga katika nchi za Ulaya – basi tunapendekeza kwamba pande zote zitume wawakilishi huru katika kila upande. Watume kwetu wajumbe na sisi tutume kwao wajumbe wetu kwenda kutathmini hali ya haki za binaadamu katika jela za pande mbili, katika mahakama, katika vitendo vya wakuu wa serikali, miamala ya kijamii pamoja na katika haki za raia na kuona ni kiasi gani haki za binaadamu zinachungwa ndani yake. Pendekezo hilo ni la kimantiki, ni zuri sana na ni la mahala pake kabisa. Tunazitaka nchi za Ulaya zilikubali pendekezo hilo. Jambo hilo pia litaboresha uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Magharibi, na wasiwasi uliopo kati ya pande mbili utaweza kuondoka.

Juu ya ukurasa

 
< Nyuma   Mbele >

^